Tarehe 30 mwezi wa 9 kila mwaka ni siku ya utafsiri duniani. Hivi hapa ni vitabu kumi vilivyotafsiriwa zaidi duniani na nchi kumi zinazotafsiri zaidi

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,224
12,729
Siku hii ilianzishwa kumuenzi St. Jerome. Huyu alikuwa mtu wa mwanzo mwanzo kutafsiri biblia. Tarehe 30/9 ni siku yake ya kufa. Utafsiri umechangia sana katika kusambaza maarifa duniani. Hata vitabu maarufu na vilivyopendwa na wengi Tanzania kama Alfu Lela Ulela, Hekaya za Abunuwasi, Mashimo ya mfalme Sulemani ni tafsiri. Hapa ni orodha ya vitabu vilivyotafsiriwa zaidi duniani.

1. Biblia. Zaidi ya lugha 3000
2. The Little Prince. Zaidi ya lugha 500(Tafsiri yake ya kiswahili ipo, Bwana Mdogo)
3. The adventures of Pinocchio. Zaidi ya lugha 250(Kiswahili Yaliyompata Pinokyo)
4. Dao De Jing(Tao Te Ching). Zaidi ya lugha 250
5. The Communist Manifesto. Zaidi ya lugha 200 (kiswahili Ilani ya Ukommunisti)
6. Alice's Adventures in Wonderland. Lugha 174(kiswahili Elisi katika nchi ya ajabu)
7. Grimm's Fairy Tales. Lugha 170
8. Steps to Christ. zaidi ya lugha 160. Bila shaka kuna tafsiri yake ya kiswahili.
9. Don Quixote. Zaidi ya lugha 140.
10. Andersen's Fairy Tales. Zaidi ya lugha 130. (Moja ya hekaya yake kwa kiswahili ni Vazi jpya la mfalme)

Hizi ndizo nchi kumi zinazotafsiri zaidi vitabu. Nchi na Idadi ya vitabu walivyotafsiri.
1Germany269,724
2Spain232,853
3France198,574
4Japan130,496
5USSR (to 1991)92,734
6Netherlands90,560
7Poland77,716
8Sweden73,230
9Denmark70,607
10China67,304
 
Naomba pidfs ulizonazo A vitabu ulivyo orodhesha hapo. Swahili version itapendeza sana
 
Kumbe wayunani ni maarufu tu kwa sababu habari zao zimeanfikwa sana na watu wengine ila wao wenyewe hawapo kwenye top 10?
Maghayo mkaldayo unasemaje
 
mada nzuri 💯. Hapa kWetu ni taasisi gani zinazijihusisha na tafsiri?
 
mada nzuri 💯. Hapa kWetu ni taasisi gani zinazijihusisha na tafsiri?
Hapa kwetu ni mmoja mmoja sana. Kuna sisi Pictus Publishers wenye vitabu kama Tajiri wa Babeli, Bwanq Mdogo, Ilani ya Ukommunisti, Lulu, Nchi ya Wasioona, Kiongozi, Sanaa ya Vita nk. Kuna huyu Prof anaitwa Ida Hadjivayanis. Ametafsiri kama Elisi katika Nchi ya Ajabu na Mwaka huu katafsiri Peponi(Kutoka kitabu cha mtanzania mshindi wa Nobel Abdulrazak Gurnah, kiitwacho Paradise). Walter Bgoya, mkurugenzi wa Mkuki na Nyotw alitafsiri Mwana Mdogo wa Mfalme.

Nadhani tunahitaji kuwa na Taasisi rasmi ya serikali inayofanya na kusaidia kazi hii.
 
Back
Top Bottom