Tanzia: Nimefiwa na mwanangu

Tanzia: Nimefiwa na mwanangu

Pole ndugu yetu, hicho kichanga hakajafanya makosa yoyote hapa duniani Mungu atakaingiza peponi mojakwamoja. Hakana maswali ya kuulizwa kama sisi.
 
Familia ya bwana Makamee inatoa pole za dhati kwako Bwana Rweye na kila aliyeguswa na msiba huu"
Kachanga hakana hata dhambi moja ametangulia kwenda kula mema peponi.
Kwakua mtoto ni faraja na huongeza furaha ktk ndoa basi tumeombe Mwenyezimungu akupe badala-AMIN
 
Pole sana mkuu! RIP kichanga, hakika Mungu amempokea malaika wake!
 
jana nilifiwa na mwanangu wakati mama ake akiwa katika hatua za kujifungua, ni maumivu sana lakini naamini ni mapenzi yake mungu.
Ninawashukuru wote waliofika kunijulia hari,waliotoa pole zao na nyote kwa pamoja, mimi sina cha kuwalipa ila ninamwomba baba mwenyezi awape rehema zake na awabariki sana!
Amina.

pole sana mkuu.
 
Hii hali hasa ukiwa ndio ujauzito wa kwanza huchanganya sana wanandoa......zaidi pressure huwa kubwa mama anapopata tena ujauzito muda wote unahisi ile hali inaweza kujirudia..........inabidi wanandoa kuwa wamoja sana kipindi hiki baada ya kupoteza mtoto ili kurudisha matumaini na kuondoa ile hofu kwamba inaweza kutokea tena.......
Rweye pole sana lakini hasa mtie moyo wife ili hali hii isilete madhara kwake kisaikolojia.
 
Last edited by a moderator:
Pole Sana Ndugu, Ila Kwetu Ni Mwiko Kulia Kama Umefiwa Na Kichanga Ambacho Hakijazidi Siku Mbili Yaani Amezaliwa Tu Na Kufa. Ailaze Mahali Pema Peponi

Usilete mambo ya kwenu hapa! Hapa ni Jforums tunaungana kama familia moja.kwani anaelia ktk kufiwa anapanga kua sasa nilie au inakuja automatic kutokana na msukumo wa hisia?
 
Kwetu,wanazika upenuni mwa nyumba,tena akina mama watupu!! Pole sana ndugu yetu!!

Na wewe pia usitusimulie mambo ya mila za kwenu hapa"
mwenzetu kafiwa tumfariji kwa maneno mazuri.
Tukisema kila mtu aanze kusimulia mila za kwao kuna wengine watasema wao hua hawaziki wanatupa porini.
 
Pole sana Rweye. Pole pia kwa mama-mtoto. Mungu akupeni ujasiri na ustahimilivu ktk kipindi hiki kigumu.
RIP Kichanga.
 
Last edited by a moderator:
Rweye Pole sana Mungu muumba mbingu na nchi awapeni faraja hasa mama kwa kuondokewa na mtoto mliyetarajia kumlea kwa mapenzi mema. Kila nafsi itaoja mauti.
 
Last edited by a moderator:
Pole sana sana, I can feel the pain too

Kweli mkuu ,saa 12asubuhi jana simu inaita nikajua shemeji yenu atakuwa na furaha kunambia nitoe jina la mtoto ila niliisikia sauti kama mtu aliye ndotoni,nikahisi utumbo unakatika ndani ...kumbe yet my son was dead.
 
Sorry to hear about that sad news mate! Mungu akupewewe na mama nguvu ktk muda huu mgumu mgugu yangu!!
 
Back
Top Bottom