Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,828
- 13,585
HOTUBA YA MHE. DKT. DOTO BITEKO, NAIBU WAZIRI MKUU NA WAZIRI WA NISHATI, AKIMWAKILISHA MHE. RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA UFUNGUZI WA JUKWAA LA 16 LA UNUNUZI WA UMMA LA AFRIKA MASHARIKI NA UZINDUZI WA MFUMO WA KIELEKTRONIKI WA UNUNUZI WA UMMA (NEST), TAREHE 9 SEPTEMBA 2024 KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA KIMATAIFA, ARUSHA
Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema kwa kutujalia uhai, siha njema, amani katika nchi yetu na kutuwezesha kukutana leo katika Jukwaa hili la Ununuzi wa Umma kwa nchi washirika wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Pili, ninapenda kuwasilisha kwenu salamu kutoka kwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye mlimualika kuwa mgeni rasmi katika siku hii muhimu ya leo. Alitamani sana kuwapo hapa, lakini kutokana na majukumu mengine ameniagiza nije nijumuike nanyi kwa niaba yake katika ufunguzi wa Jukwaa hili na uzinduzi wa Mfumo wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (NeST). Vile vile, nichukuwe wasaa huu kumpongeza Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), Wizara na wote waliohusika na maandalizi mazuri ya Jukwaa hili. Hongereni sana.
Ndugu Washiriki; mniruhusu kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, niwashukuru pia wadau wa sekta hii ya ununuzi wa umma kutoka nchi wanachama wa Jumuiya yetu ya Afrika Mashariki na wengine kwa mwitikio wenu mkubwa wa kuhudhuria Jukwaa hili. Hii inaonesha kwamba sekta hii ambayo hutumia takriban asilimia sabini ya bajeti za Serikali zetu ina mshikamano na mnafanyakazi kwa pamoja katika Jumuiya yetu ya Afrika Mashariki, hii inaonyesha kwamba, Wizara ya Fedha na ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki zinafanya kazi kwa karibu na wadau wake.
Ndugu Washiriki; Nimefurahi kusikia mazuri mengi kuhusu Jukwaa hili tangu kuanzishwa kwake mwaka 2008 pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana. Nimeambiwa kuwa hii ni mara ya 16 mnakutana ili kubadilishana ujuzi na uzoefu pamoja na kujadili masuala muhimu yanayohusiana na ununuzi wa umma kwenye nchi zetu za Afrika Mashariki. Natumaini pia mtapata fursa ya kujadili na kuoanisha mifumo ya kidigitali ya ununuzi wa umma ambayo pia kwetu ni muhimu katika kufanikisha masuala ya pamoja kwenye ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Ndugu zangu, Serikali yetu ya Tanzania imefanya mageuzi makubwa ya kisheria katika ununuzi wa umma ambayo yalianza Mwaka 2001 kwa kutungwa kwa sheria ya kwanza ya Ununuzi wa Umma. Baada ya changamoto kadhaa, zilipelekea mabadiliko ya Sheria ya mwaka 2004, na kuanzisha Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA). Serikali kupitia PPRA kama chombo cha Udhibiti wa Ununuzi wa Umma ililenga kufanya mageuzi na kuboresha usimamizi wa ununuzi wa umma, kuhakikisha thamani ya fedha, uwazi, na uwajibikaji, ufanisi na uadilifu katika ununuzi na ugavi na kujenga uwezo katika ununuzi na ugavi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ndugu Washiriki; Sisi wote tutakuwa mashahidi ni kwa kiasi gani shughuli za udhibiti wa ununuzi wa umma zimekuwa zikiimarika kutokana na usimamizi mzuri wa Wizara ya Fedha na PPRA. Nimefurahi pia kujulishwa kwamba maboresho mengi ya mara kwa mara yaliyofanyika kwenye Sheria, Kanuni na taratibu zetu za Ununuzi wa Umma yamekuwa yakitumia uzoefu uliopatikana kupitia Jukwaa hili. Ninawapongeza sana.
Ndugu washiriki, Serikali zenu zinatambua kwamba fedha nyingi zinazotengwa kwenye bajeti kila mwaka zimekuwa zikitumika kupitia ununuzi wa umma. Kwa kuzingatia hilo, Serikali imekuwa makini kuhakikisha kuwa fedha hizo zinazotumika kupitia ununuzi wa umma zinapata usimamizi makini. Aidha, Kupitia Kifungu cha 7 cha Sheria ya Ununuzi wa Umma Sura ya 410 ya Mwaka 2023, Serikali pia imeipa Wizara ya Fedha jukumu la kuhakikisha kuwa inaandaa Sera ya Taifa na Mkakati wa Usimamizi wa Mnyororo wa Ugavi ili kuhakikisha ununuzi na shughuli zote zlizofunganishwa katika mnyororo wa ugavi zinazofanyika kwenye taasisi za umma zinazingatia Sera hiyo na mikakati tutakayojiwekea. Nimefurahi kujulishwa kuwa, mpo kwenye hatua nzuri, Mheshimiwa Waziri, hakikisha unalisimamia hili kwa karibu sana.
Ndugu washiriki; Natambua kwamba Kupitia Sheria ya Ununuzi wa Umma Sura 410, Serikali imeboresha yafuatayo:
Serikali imeboresha mfumo wa kisheria na kuweka miundo ya utawala kwa taasisi zinazoshughulikia shughuli za ununuzi zinazotekelezwa na taasisi za umma. Sheria hii pia imeanzisha Mamlaka ya Rufaa ya Ununuzi wa Umma (PPAA) kwa ajili ya kutatua malalamiko yanayohusiana na ununuzi.
Ndugu Washiriki; Naamini kuwa Mamlaka zote za Ununuzi wa Umma kutoka nchi Wanachama wa Jumuiya yetu ya Afrika Mashariki wanaoshiriki kwenye Jukwaa hili nao wana malengo yanayofanana na haya tuliyo nayo hapa Tanzania. Kutokana na malengo ya uanzishwaji wa mamlaka hizi, natoa wito kwa Mamlaka zote kuhakikisha kuwa mnasimamia malengo mliyoyaweka ili kuhakikisha tija na ufanisi unapatikana katika usimamizi wa sekta hii ili huduma kwa wananchi iendelee kupatikana kwa wakati na kwa ufanisi.
Ndugu Washiriki, nimefurahishwa na kauli mbiu ya Jukwaa hili la 16 ambayo ni;
“Utumiaji wa Mifumo ya Kielektroniki kwa Ununuzi wa Umma Endelevu”
Kwa miaka mingi, viongozi katika eneo hili la Afrika Mashariki wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo endelevu katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Tumefanya kazi kubwa ili kuhakikisha kuwa hali za kisiasa, kisheria, kiuchumi na kijamii zinachangia kupunguza umaskini, kutengeneza nafasi za kazi, ulinzi wa mazingira na maendeleo ya wanawake na vijana.
Tunapotumia fedha za umma kununua bidhaa, huduma au miradi katika nchi zetu, tunapaswa pia kufahamu hitaji la maendeleo endelevu na ustawi wa Ushirikiano baina ya nchi zetu za Afrika Mashariki. Hii ina maana kwamba, mifumo yetu ya ununuzi kwa nchi za EAC zinapaswa kuhakikisha zinajengwa kwa lengo la kuleta manufaa ya muda mrefu kwa wananchi wetu. Kwa hivyo ningependa kuwataka mhakikishe mnakuza viwango vya kikanda vya ununuzi endelevu ambavyo vitaimarisha usawa wa kijamii, maendeleo ya kiuchumi, na uendelevu wa mazingira.
Tofauti na ulimwengu ulioendelea kiviwanda, uingiaji wa bidhaa kutoka nchi za nje kuja katika nchi za EAC ni mkubwa sana. Hii inamaanisha kuwa, bidhaa na huduma ambazo sekta ya umma katika kanda hutumia mara nyingi huagizwa kutoka nje. Kwa kuwa nchi za EAC ni soko kubwa, tunahitaji kujenga uwezo katika Jumuiya hii ili kuzalisha bidhaa zinazohitajika kabla ya kufikiria kuagiza kutoka nje ya ukanda huu. Manufaa haya yanaweza kupatikana kupitia ushirikiano wa nchi wanachama wa EAC, na maendeleo ya Viwanda vyetu ambayo ndiyo injini ya uchumi wetu, lakini pia thamani bora ya pesa kuhusiana na bidhaa na huduma zinazonunuliwa.
Aidha, Serikali imeendelea kudhibiti matumizi ya fedha zinazopelekwa kwenye kila Fungu kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo mifumo ya kielektroniki ili kuleta tija na ufanisi unaostahili katika utekelezaji wa Bajeti ya Fungu husika. Kutokana na azma hiyo, mnamo mwaka 2019 Serikali ilianzisha Mfumo wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (Tanzania National e-Procurement System – TANePS) ambao ulikuwa ukisimamiwa PPRA. Hata hivyo, kutokana na changamoto nyingi za kimfumo, Serikali kupitia Wizara ya Fedha, iliamua kujenga Mfumo mpya wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (National e-Procurement System of Tanzania –NeST).
Ndugu Washiriki; Nimefurahishwa na hatua ya sasa ambayo ilipelekea ujenzi wa NeST kufanywa na vijana wetu wa Tanzania, lakini pia nimedokezwa hapa kuwa nchi nyingi za EAC zimeanza kuutamani huu mfumo wa NeST, nafurahi kuona kwamba kupitia jukwaa hili tunaweza kubadilishana uzoefu katika mambo mbalimbali ikiwemo mifumo. Ninapenda kutoa pongezi kwa watumishi wote kutoka taasisi mbalimbali za Serikali, na hasa Wizara ya Fedha, PPRA na e-GA ambao wameshiriki katika kujenga mfumo huo. Ni wazi kuwa matumizi ya mifumo ya kielektroniki yanayoendelea kuhamasishwa yana faida kubwa kama ambavyo tumeweza kuona mara baada ya Serikali ya Tanzania kuanza kutumia mfumo wa NeST. Faida hizo ni pamoja na:
Ndugu Washiriki; pamoja na jitihada za Serikali kujenga NeST, inashangaza kuona kuwa kuna baadhi ya taasisi za umma hazitumii NeST katika shughuli za ununuzi. Ninatoa maelekezo kwa Mheshimiwa Waziri kwa kushirikiana na Mamlaka nyingine kama vile Msajili wa Hazina, kuhakikisha kwamba wote ambao wamepewa majukumu ya kuongoza taasisi za umma kuhakikisha wanatumia NeST. PPRA iwasilishe kwangu taarifa ya wote ambao watakaidi maagizo haya. Ninawaelekeza pia Mawaziri na Makatibu Wakuu wote kuhakikisha kuwa Taasisi Nunuzi zilizopo kwenye Mafungu yenu, pamoja na Taasisi zote za umma, zinautumia mfumo wa NeST katika ununuzi wote unaotumia fedha za umma.
Ndugu zangu, nimefurahi kusikia pia kuwa mfumo wa NeST umeongeza uwazi, uwajibikaji na kuleta thamani ya fedha katika ununuzi. Ni wazi kuwa Mfumo huu utaleta faida nyingine nyingi kama vile kuimarisha utawala bora, kuongeza wigo wa ununuzi na kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa. Ni matarajio yangu na ya Serikali kwamba mtaendelea kuuboresha mfumo wa NeST mwaka hadi mwaka, ili watumiaji wavutiwe na kuweza kuongeza thamani ya fedha katika ununuzi wa umma. Natarajia pia nyie mtakuwa vinara wa mifumo ya ununuzi ya kidigitali katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki.
Ndugu Washiriki; Katika Jumuiya yetu ya Afrika Mashariki (EAC), tunajua vyema haja ya kuwa na mifumo imara ya kidigitali katika nchi zetu kwa lengo la kuendeza ustawi wa uchumi kwenye nchi zetu. Katika dunia hii ya kidigitali na kadiri ushirikiano unavyokuwa, nchi zetu zitaendelea kufaidika zaidi ikiwa tutaendeleza matumizi ya digitali kwenye shughuli zetu za kiuchumi. Ili kuyafikia haya, ni muhimu kuwa na ushirikiano katika nchi zetu, ikiwa ni pamoja na Usimamizi wa Fedha za Umma ambapo ununuzi wa umma una jukumu muhimu. Ninafurahi kwamba Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki imehudhuria Jukwaa hili na ninaiomba ihakikishe masuala ya pamoja ununuzi wa umma yanajadiliwa kwenye vikao vya Jumuiya yetu kwenye ngazi mbalimbali kwa ustawi wa nchi zetu. Ni matarajio yangu kuwa Jukwaa hili litakuja na maazimio yenye lengo la kuoanisha masuala haya katika muktadha wa Ushirikiano wa nchi za EAC.
Ninawashukuru na kuwapongeza washiriki wote kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi. Nimejulishwa na kufurahi kusikia sehemu kubwa ya washiriki hawa watatembelea mbuga zetu za Wanyama za Ngorongoro na kujionea vivutio mbalimbali vya kitalii ambavyo viko kwa wingi nchini Tanzania. Niungane na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Paul Makonda kuwakaribisha nchini washiriki wote kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na kutoka nchi nyingine ambao mmehudhuria hapa Hongera sana kwa uamuzi huo na Karibuni Tanzania mjionee vivutio vyetu vya utalii.
Baada ya kuyasema hayo, ninapenda kuchukua fursa hii kuwatakia mijadala na mashauri yenye manufaa yatakayochochea mageuzi zaidi katika ununuzi wa umma. Sasa ninapenda kutangaza kuwa Jukwaa hili limefunguliwa rasmi.
Asanteni Sana kwa kunisikiliza.

- Uboreshaji wa Mifumo ya Kidijitali, Serikali imeanzisha na inaboresha mifumo mbalimbali ya kidigitali katika taasisi za umma, kama vile Mfumo wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (TANePS) na National e-Procurement System of Tanzania (NeST), ili kuboresha taratibu za ununuzi na kuongeza ufanisi.
- Kuajiri na kuwajengea uwezo Wafanyakazi, Serikali imeajiri na kuwajengea uwezo wafanyakazi wa ununuzi katika taasisi za umma. Aidha, imetengeneza chombo cha kitaalama ambacho ni Baraza la Usimamizi wa Taaluma za Ununuzi (PSPTB), kwa ajili ya kusimamia taaluma na mienendo ya wafanyakazi katika sekta hii.
- Kuboresha upatikanaji wa Zabuni kwa Watanzania, Serikali imeweka masharti kwenye Sheria ya Ununuzi wa Umma, kutenga asilimia 30 ya bajeti ya ununuzi kwa ajili ya kununulia bidhaa na huduma kutoka kwa makundi maalum kama vile vijana, wazee, wanawake, na watu wenye mahitaji maalum. Sambamba na kuwapa kipaumbele Makandarasi wazawa na kuwajengea uwezo wa mara kwa mara.
Ndugu Washiriki; Naamini kuwa Mamlaka zote za Ununuzi wa Umma kutoka nchi Wanachama wa Jumuiya yetu ya Afrika Mashariki wanaoshiriki kwenye Jukwaa hili nao wana malengo yanayofanana na haya tuliyo nayo hapa Tanzania. Kutokana na malengo ya uanzishwaji wa mamlaka hizi, natoa wito kwa Mamlaka zote kuhakikisha kuwa mnasimamia malengo mliyoyaweka ili kuhakikisha tija na ufanisi unapatikana katika usimamizi wa sekta hii ili huduma kwa wananchi iendelee kupatikana kwa wakati na kwa ufanisi.
Ndugu Washiriki, nimefurahishwa na kauli mbiu ya Jukwaa hili la 16 ambayo ni;
“Utumiaji wa Mifumo ya Kielektroniki kwa Ununuzi wa Umma Endelevu”
Kwa miaka mingi, viongozi katika eneo hili la Afrika Mashariki wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo endelevu katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Tumefanya kazi kubwa ili kuhakikisha kuwa hali za kisiasa, kisheria, kiuchumi na kijamii zinachangia kupunguza umaskini, kutengeneza nafasi za kazi, ulinzi wa mazingira na maendeleo ya wanawake na vijana.
Tunapotumia fedha za umma kununua bidhaa, huduma au miradi katika nchi zetu, tunapaswa pia kufahamu hitaji la maendeleo endelevu na ustawi wa Ushirikiano baina ya nchi zetu za Afrika Mashariki. Hii ina maana kwamba, mifumo yetu ya ununuzi kwa nchi za EAC zinapaswa kuhakikisha zinajengwa kwa lengo la kuleta manufaa ya muda mrefu kwa wananchi wetu. Kwa hivyo ningependa kuwataka mhakikishe mnakuza viwango vya kikanda vya ununuzi endelevu ambavyo vitaimarisha usawa wa kijamii, maendeleo ya kiuchumi, na uendelevu wa mazingira.
Tofauti na ulimwengu ulioendelea kiviwanda, uingiaji wa bidhaa kutoka nchi za nje kuja katika nchi za EAC ni mkubwa sana. Hii inamaanisha kuwa, bidhaa na huduma ambazo sekta ya umma katika kanda hutumia mara nyingi huagizwa kutoka nje. Kwa kuwa nchi za EAC ni soko kubwa, tunahitaji kujenga uwezo katika Jumuiya hii ili kuzalisha bidhaa zinazohitajika kabla ya kufikiria kuagiza kutoka nje ya ukanda huu. Manufaa haya yanaweza kupatikana kupitia ushirikiano wa nchi wanachama wa EAC, na maendeleo ya Viwanda vyetu ambayo ndiyo injini ya uchumi wetu, lakini pia thamani bora ya pesa kuhusiana na bidhaa na huduma zinazonunuliwa.
Aidha, Serikali imeendelea kudhibiti matumizi ya fedha zinazopelekwa kwenye kila Fungu kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo mifumo ya kielektroniki ili kuleta tija na ufanisi unaostahili katika utekelezaji wa Bajeti ya Fungu husika. Kutokana na azma hiyo, mnamo mwaka 2019 Serikali ilianzisha Mfumo wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (Tanzania National e-Procurement System – TANePS) ambao ulikuwa ukisimamiwa PPRA. Hata hivyo, kutokana na changamoto nyingi za kimfumo, Serikali kupitia Wizara ya Fedha, iliamua kujenga Mfumo mpya wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (National e-Procurement System of Tanzania –NeST).
Ndugu Washiriki; Nimefurahishwa na hatua ya sasa ambayo ilipelekea ujenzi wa NeST kufanywa na vijana wetu wa Tanzania, lakini pia nimedokezwa hapa kuwa nchi nyingi za EAC zimeanza kuutamani huu mfumo wa NeST, nafurahi kuona kwamba kupitia jukwaa hili tunaweza kubadilishana uzoefu katika mambo mbalimbali ikiwemo mifumo. Ninapenda kutoa pongezi kwa watumishi wote kutoka taasisi mbalimbali za Serikali, na hasa Wizara ya Fedha, PPRA na e-GA ambao wameshiriki katika kujenga mfumo huo. Ni wazi kuwa matumizi ya mifumo ya kielektroniki yanayoendelea kuhamasishwa yana faida kubwa kama ambavyo tumeweza kuona mara baada ya Serikali ya Tanzania kuanza kutumia mfumo wa NeST. Faida hizo ni pamoja na:
Kupungua kwa gharama za kufanya ununuzi kwa wazabuni na Serikali.
kuondokana na matumizi ya karatasi.
kuongezeka kwa kasi ya ununuzi.
kupungua kwa makosa katika Ununuzi na kuboresha utoaji huduma kwa wananchi.