TANZIA Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kusini Unguja "Mzee Kichupa" afariki Dunia

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,734
6,292
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimepokea kwa mshtuko, majonzi na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ramadhan Ali Abdallah Maarufu (Mzee Kichupa) kilichotokea Jumanne 27 Julai, 2021 katika Hospital Kuu ya Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar.

E7TIM3cXEAEGI7b.jpg

1627387673340.png
 
Unguja. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Kusini Unguja, Ramadhan Abdalla Ali amefariki dunia nyumbai kwake visiwani Zanzibar.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu leo Jumanne Julai 27, 2021, Katibu wa Itikadi na Uenezi Zanzibar, Catherine Nao amesema kifo cha mzee huyo sio tu pigo ndani ya chama pekee bali Taifa kwa ujumla.

“Amefariki kweli taratibu za mazishi zinapangwa na familia lakini anatarajiwa kuzikwa kesho,” amesema Nao.

Nao amemwelezea mwenyekiti huyo kwamba alikuwa ni hazina, mbali na nafasi yake ya uenyekiti wa chama lakini alikuwa mzee anayefahamu na kuchanganua mambo mengi.

Kwa mujibu wa Nao, Mzee Ali alikuwa mwalimu wa kisiasa ambaye walimtumia katika madaraka ya itikadi kuwaelewesha vijana, wakina mama ilipotoka Afro Shiraz na kwa nini yalifanyika mapinduzi visiwani humo “kwahiyo alikuwa hazina kubwa sana.”

Screenshot_20210727-151919_Facebook.jpg
 
Serikali ya CCM isipotubu itaisha yote. Hivi ndani ya miaka hii 2 mmepoteza Viongozi lukuki na bado mnaendeleza chuki zenu za wazi kwa upinzani .
Adui yetu ni ufukara na ujinga na si CCM au chadema
 
Back
Top Bottom