Mwenyekiti CCM Mkoa wa Tanga Achangia Milioni 10 Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mwembeni

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

KOMREDI RAJABU ABDURRAHMAN ACHANGIA MILIONI 10 UJENZI WA ZAHANATI KIJIJI CHA MWEMBENI

"Katika kuitekeleza ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 nimechangia Tsh 10,000,000/ (milioni kumi) kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati katika Kijiji cha Mwembeni, Kata ya Madanga wilayani Pangani" - Komredi Rajabu Abdu Rrahman, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Rajabu Abdurrahman (MNEC) ameungana na Kamati ya siasa mkoa kukagua miradi ya maendeleo ya Wilaya ya Pangani ikiwa ni sehemu ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa CCM 2020-2025.

Katika ziara hiyo, Mbunge wa Jimbo la Pangani, Mhe. Jumaa Aweso (Waziri wa Maji) amechangia matofali 2,000 na mifuko 100 ya Saruji huku viongozi wengine waandamizi wakichangia kwa sehemu zao.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Zainab Abdallah amesema kwa upande wa Serikali watasimamia kuhakikisha Zahanati inajengwa kwa ubora na viwango na kukamilika kwa wakati.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-01-28 at 14.19.21.jpeg
    WhatsApp Image 2024-01-28 at 14.19.21.jpeg
    51.7 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-01-28 at 14.19.22.jpeg
    WhatsApp Image 2024-01-28 at 14.19.22.jpeg
    58 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-01-28 at 14.19.23.jpeg
    WhatsApp Image 2024-01-28 at 14.19.23.jpeg
    35.9 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-01-28 at 14.19.23(2).jpeg
    WhatsApp Image 2024-01-28 at 14.19.23(2).jpeg
    59 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-01-28 at 14.19.24(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-01-28 at 14.19.24(1).jpeg
    41.3 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-01-28 at 14.19.24.jpeg
    WhatsApp Image 2024-01-28 at 14.19.24.jpeg
    61 KB · Views: 2
Back
Top Bottom