TANZIA Tanzia: Mbunge wa Viti Maalumu, Martha Umbulla(CCM) afariki dunia

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
19,422
2,000

Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) afariki dunia​

Thursday January 21 2021​

Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Manyara, Martha Umbulla amefariki dunia Januari 21, 2021 katika Hospitali ya HCG Mumbai, India alikokuwa akipatiwa matibabu.

Martha Jachi Umbulla (amezaliwa 10 Novemba 1955) ni mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa Chama cha kisiasa cha Chama Cha Mapinduzi (CCM). Amechaguliwa kuwa mbunge wa Viti maalum vya wanawake kwa mara ya kwanza 2015 – 2020 na 2020 - 2021

===
Umbulla.jpg


1611225621207.png

Dar es Salaam. Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Manyara, Martha Umbulla amefariki dunia Januari 21, 2021 katika Hospitali ya HCG Mumbai, India alikokuwa akipatiwa matibabu.

Kifo cha mbunge huyo aliyezaliwa Novemba 10, 1955 kimetangazwa leo Alhamisi Januari 21, 2021 na Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai.

“Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Martha Umbulla. Natoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, wabunge na wananchi wa Mkoa wa Manyara. Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu.”

“Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya marehemu inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi amina,” amesema Ndugai.

====
RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI
Dar es Salaam. Rais John Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa Spika Job Ndugai kufuatia kifo cha mbunge wa viti maalum CCM, Martha Umbulla kilichotokea usiku wa kuamkia leo Alhamisi Januari 21, 2021 nchini India.

Taarifa iliyotolewa leo na mkurugenzi wa mawasiliano ya rais Ikulu, Gerson Msigwa inaeleza kuwa kiongozi mkuu huyo wa nchi amepokea kwa masikitiko taarifa za mbunge huyo aliyekuwa Mumbai, India kwa ajili ya matibabu.

“Ametuma salamu za rambirambi kwa Ndugai, familia ya Martha, wabunge wote, wananchi wa Mkoa wa Manyara na wote walioguswa na kifo hicho.”

“Umbulla alikuwa mpole, mchapakazi na mpenda maendeleo. Nazikumbuka jitihada zake za uongozi akiwa mkuu wa Wilaya na akiwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” amesema Rais Magufuli.

Amewaomba wanafamilia wote wawe na moyo wa uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi kigumu cha majonzi na amemuombea Martha apumzike mahali pema peponi.

 

Lusungo

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
21,644
2,000
Martha Umbula mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Manyara amefariki dunia.

Amefariki huko India alikokua kwenye matibabu.

Spika amethibitisha!
 

mdudu

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
3,948
2,000
Sipika hawezi kuchagua masalia mengine ya Covid 19 ili azibe nafasi?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom