TANZIA: Kada wa CCM Peter Kalihose afariki dunia

So sad, Peter Kalihose nimemfahamu tukiwa form 2, baada ya yeye kuhamia shuleni kwetu.

Alikuwa ana akili sana, maana nakumbuka alikuwa anawafundisha jamaa wa Form 4 mwaka huo huo na hata wakati tuko form 3 aliendelea na utaratibu wake wa kuwafundisha jamaa waliokuwa form 4 masomo kama physics, hesabu, chemistry na biology.

Form 4 alichaguliwa kwenda Shinyanga Sekondary na aliendelea kukimbiza darasani kwa sababu ya uelewa mkubwa wa mambo aliokuwa nao, bahati mbaya hakuweza kuendelea na shule kwa sababu ya kuumwa mara kwa mara, muda mwingi alikuwa anautumia hospital zaidi ya darasani.

Form six alimalizia shule moja ya Dar es Salaam, degree yake amefanyia Tumaini Iringa.

Ni moja ya watu niliokuwa ninaukubali uelewa wake kuanzia mambo ya shule mpaka yasiyo ya shule.

RIP Bro.

Aah! Kumbe naye alikuwa anauguaga!! Kwa hiyo uchungu wa maradhi aliufahamu!!
 
Aliyemtukana Mbunge Godbles Lema...kumuita Chizi.

Na ukawa kuwaita Manyumbu

Pamoja na Lowasa...kumuita....mfu mtarajiwa.....AFARIKI DUNIA GHAFLA.
 
Enyi Wazungu, WAMAREKANI

1. Mmewageuza Ndugu zetu kuwa Nyumbu (Bila ubishi tunekubali)

2. Mmeingia Mikataba ya kuwaoa ndugu zetu (nyumbu wa kiume) bila ubishi tumekubali muwachukue hata bila mahali

3. Mmewageuza hao nyumbu kuwa vyombo vyenu vya propaganda dhidi ya tawala halali zilizocchaguliwa kidemokrasia barani afrika (bila ubishi tumekubali, japo hatutakubali kutawaliwa na nyumbu)

4. Mmewageuza nyumbu hao kuwa vifaa vya kuandaa ujio wenu wa kujaribu kutawala tena bara letu na kutwaa rasilimali zetu ambazo hamkujua awali kwamba tunazo (tumekubali muwatumie lkn mjue hamtafanikiwa maana tumejiandaa)

Sasa tunawaambia, endeleeni na yote, ikibidi hata hizo dola 460milioni wapatieni mabibi zenu wa unyumbuni lakini mjue kwamba, KAMWE hamtafanikiwa katika MAJARIBIO YENU...na kwa kuanzia, kibaraka wenu wa Hizbu ataisikia Ikulu yetu ya Visiwani kwenye vyombo vya habari na Sheria ya Mitandao itaimalishwa zaidi ili kudhibiti kabisa harakati za nyumbu mitandaoni....mfikishieni salaam Trump.

WASALAAM
Ndicho mlichobaki nacho kuongea vitu kama wendawazimu.
Hiso zote ni laana ya kula rambirambi za wafiwa
Mmkosa weledi, mmehishiwa hoja, mmeshindwa kutatua kero watu sasa mmekimbilia kumtukana.
Mmemudhi mchinja mbwa wazimu umewarudia
 
Jamaa mzinguaji ndo maana biblia inasema mtu akifa matendo yake yanamfuata simu hukumu ila tuchunge ndimi zetu vinywa vyetu tuvifungue kwa mazuri
 
Nimeshtushwa na taarifa za kifo cha Ndugu Peter Kalihose, mwanachama na kada hodari wa CCM mitandaoni ambaye alikua akikisaidia sana chama chake hasa kwenye propaganda. Lakini kifo cha Peter kitupe somo sisi tuliobaki hai.

Pamoja na umahiri wa Peter katika kujenga hoja lakini alikua bingwa wa kuattack personality. Matusi aliyoyatoa kwa Lowassa mengine hayaandikiki. Aliwahi kumuita mgonjwa, dhaifu, na marehemu mtarajiwa. Bahati mbaya hakuna kiongozi wa CCM aliyemkemea dhidi ya lugha hizo za matusi.

Leo Peter ametangulia amemuacha yule aliyemuita marehemu, maiti inayotembea, mgonjwa, na dhaifu akizidi kuimarika na kujenga chama chake. Ni vizuri tuishi tukijua maisha ya hapa duniani ni ya muda tu na siku moja sote tutatoweshwa. Hatuna mji udumuo hapa. Lakini jiulize utakapoondoka utaacha alama gani nyuma yako? Alama utakayoiacha itafuatana na matendo yako.

Usijivunie uzima ulionao. Uzima na ugonjwa ni majaliwa ya Mwenyezi Mungu. Kama wewe ni mzima mshukuru Mungu na waombee walio wagonjwa. Katika malezi yangu nilifundishwa kila nisalipo nisisahau kuwakumbuka wagonjwa, yatima na wajane. Sio kuwadharau, kuwadhihaki, wala kuwapuuza. Huenda Peter alijiona ana nguvu kuliko Lpwassa, ni imara kuliko Lowassa, ana afya bora kuliko Lowassa akasahau kuwa aliyempa afya hiyo ni Mungu, tena kwa neema tu.

Simlaumu Peter, ya kwake yamepita na hatuna lolote la kubadilisha aliyosema. Tunachopaswa kujifunza kupitia Peter ni kwamba katika maisha yetu tusijivunie uzima tulionao, wala tusiwadhihaki tunaoona wana afya zilizodhoofu. Mpaji wa yote ni Mungu mwenyezi. Ayubu aliwahi kudhoofu mwili akabakia mifupa, akapoteza mali na watoto wake wote. Lakini hakufa. Waliokua na afya walikufa wakamuacha. Baadae Mungu akamnyanyua Ayubu na kumpa afya bora, mali na watoto wengine.

Tusiruhusu siasa kujenga chuki baina yetu. Sisi sote ni watanzania, tuulinde utaifa wetu. CCM, Chadema, ACT, CUF haiwezi kuwa muhimu kuliko utu wako na utaifa wako. Heshimu kila mmoja bila kijali ni wa chama chako au lah. Tujifunze kuwa na siasa za kujadili masuala badala ya kuattack personality.

Tukiwa na siasa za kujadili issues hatuwezi kuwa maadaui kwa wafuasi wa vyama vingine. Tutafanya siasa, tutabishana na kushambuliana kwa hoja, lakini nje ya siasa tutaheshimiana na kushirikishana mambo mbalimbali. Mimi ni mwanachama hai wa Chadema kwa miaka 9 sasa lakini nina ndugu na marafiki wengi ambao wapo CCM na vyama vingine. Wengine mawaziri, wengine wabunge, wengine viongozi wa kada mbalimbali na wwngine wanachama wa kawaida. Nje ya siasa tunakula pamoja, tunafurahi pamoja, tunashirikiana na kusaidiana.

Majuzi gari yangu ilipasuka tairi nikiwa mbele kdg ya Kibaigwa, na sikua na Spear tyre, nikampigia simu rafili yangu ambaye ni mwanaCCM na ni kiongozi wa serikali, akatuma gari ikaniletea spear tairi kutoka Dodoma. Siasa haipaswi kutufanya maadui, siasa haipaswi kutujengea chuki, dharau, au dhihaka dhidi ya wengine. Nje ya siasa sisi sote ni binadamu wenye usawa na tunastahili kuheshimiwa utu wetu.

By the way hapa duniani sote tutapita na hakuna atakayeishi milele. Rafiki yangu Dr.Christopher Cyrilo anapenda kusema hakuna atakayeondoka hapa duniani akiwa hai (Nobody will leave this world alive). Sote tutakufa siku moja, sote tunapita, sote ni mavumbi. Lakini je ukifa utaacha nini kwa waliobaki duniani? Watakukumbuka kwa lipi?

Kwa heri Peter. Upumzike kwa amani. Safari yako hapa duniani imefikia tamati. Sisi tuliobaki kwenye safari hii ni jukumu letu kujitathmini na kujipima kwa matendo yetu. Mungu atujalie kuwa na mwisho mwema.!

Malisa GJ
tmp_3362-FB_IMG_1483703448933536511259.jpg
 
Mungu aipumzishe nafsi yake kwa amani.

Kumbu kumbu zangu zinaonyesha huyu alikuwa ni Miongoni mwa wale waliokashifu Sana afya ya Mzee Lowassa. Lakini kwa kuwa Mungu si mwanadamu yeye ametangalia na Lowassa yu ngali Hai.

Funzo kwetu tuliobaki, siasa zisitutoe utu wetu.
Hata huyu pia alimkashifu lowasa
 
Attachments

  • 1483703571484.jpg
    1483703571484.jpg
    44.8 KB · Views: 75
Aah! Kumbe naye alikuwa anauguaga!! Kwa hiyo uchungu wa maradhi aliufahamu!!

Mkuu linapokuja swala la kifo naamini mizaha inawekwa pembeni, hii ni safari yetu sote mkuu.

Hata hivyo kila mtu ana maoni na uhuru wa kuandika chochote ili mradi havunji sheria.
 
Upumzike kwa amani.. Hongera wanasiasa wa upinzani kwa kuendelea kufanya siasa kwenye kifo cha mwenzetu, linapokuja swala la kifo siasa tuweke pembeni
yeye alifanya siasa kwa kuwaita walio hai 'watarajiwa', hapo unasemaje? acheni Mungu aitwe Mungu jamani.
 
Mshahara wa dhambi ni mauti...bali tu hujaelewa kuwa ni adhabu? Ila fisiemu mlivo na ujasiri na upofu utakanusha hata maandiko matakatifu!
Kwahiyo watu wote duniani wana dhambi? Kwa sab kila mtu atakufa
 
Sense kwa amani ya bwana ila huko mbinguni asisahau kutushtakia kwa mungu kuhusu haya Matamko ya serikali ya magu.RIP KADA
 
Hii mbona haijakaa sawa. Post yake ya mwisho (Desemba 2016) iliyopo hapa inaonyesha jamaa alivyokuwa mpiganaji wa CCM dhidi ya upinzani na ufisadi "wanaouendekeza". Lini alikutwa mbadhirifu hadi kutumbuliwa na Magufuli? Halafu inawezekana kuwa alikuwa mgonjwa wa akili? Ni habari ya kushangaza hii; haiunganiki vizuri.
Mkuu sikulazimishi kuamini ninachokiandika ila huo ndio ukweli.

Jamaa alichanganyikiwa baada ya Pombe kushika nchi ila hakupenda kujionesha kuwa upande wa upinzani sijui kwa ajili ya kuona aibu .

Kwa sababu hawa ndugu zangu wapo wawili walipata huo mtihani mmoja alikimbilia kusoma Arusha mpaka leo yupo huko yeye alikuwa kahama ila sitotaja ofisi gani. Yeye pia alitamani kuacha kazi watu walimshauri aombe kibali ili akasome hapo kabla vibali vya kwenda kusoma havijaanza kuzuiwa.Ila huyu wa pili yeye ndio alikuwa timu Lowasa kabisa sasa kwa ile hofu tu ya kudhindwa bosi wake alizidi kukonda.

So subiri tukipata mwili na report ya kifo nitawapa habari kamili wala msiwe na shaka wandugu.
 
Ndicho mlichobaki nacho kuongea vitu kama wendawazimu.
Hiso zote ni laana ya kula rambirambi za wafiwa
Mmkosa weledi, mmehishiwa hoja, mmeshindwa kutatua kero watu sasa mmekimbilia kumtukana.
Mmemudhi mchinja mbwa wazimu umewarudia
Mkuu, huo ujumbe ni wa huyo marehemu nimeutoa kule Face book kwake!
 
Nimeshtushwa na taarifa za kifo cha Ndugu Peter Kalihose, mwanachama na kada hodari wa CCM mitandaoni ambaye alikua akikisaidia sana chama chake hasa kwenye propaganda. Lakini kifo cha Peter kitupe somo sisi tuliobaki hai.

Pamoja na umahiri wa Peter katika kujenga hoja lakini alikua bingwa wa kuattack personality. Matusi aliyoyatoa kwa Lowassa mengine hayaandikiki. Aliwahi kumuita mgonjwa, dhaifu, na marehemu mtarajiwa. Bahati mbaya hakuna kiongozi wa CCM aliyemkemea dhidi ya lugha hizo za matusi.

Leo Peter ametangulia amemuacha yule aliyemuita marehemu, maiti inayotembea, mgonjwa, na dhaifu akizidi kuimarika na kujenga chama chake. Ni vizuri tuishi tukijua maisha ya hapa duniani ni ya muda tu na siku moja sote tutatoweshwa. Hatuna mji udumuo hapa. Lakini jiulize utakapoondoka utaacha alama gani nyuma yako? Alama utakayoiacha itafuatana na matendo yako.

Usijivunie uzima ulionao. Uzima na ugonjwa ni majaliwa ya Mwenyezi Mungu. Kama wewe ni mzima mshukuru Mungu na waombee walio wagonjwa. Katika malezi yangu nilifundishwa kila nisalipo nisisahau kuwakumbuka wagonjwa, yatima na wajane. Sio kuwadharau, kuwadhihaki, wala kuwapuuza. Huenda Peter alijiona ana nguvu kuliko Lpwassa, ni imara kuliko Lowassa, ana afya bora kuliko Lowassa akasahau kuwa aliyempa afya hiyo ni Mungu, tena kwa neema tu.

Simlaumu Peter, ya kwake yamepita na hatuna lolote la kubadilisha aliyosema. Tunachopaswa kujifunza kupitia Peter ni kwamba katika maisha yetu tusijivunie uzima tulionao, wala tusiwadhihaki tunaoona wana afya zilizodhoofu. Mpaji wa yote ni Mungu mwenyezi. Ayubu aliwahi kudhoofu mwili akabakia mifupa, akapoteza mali na watoto wake wote. Lakini hakufa. Waliokua na afya walikufa wakamuacha. Baadae Mungu akamnyanyua Ayubu na kumpa afya bora, mali na watoto wengine.

Tusiruhusu siasa kujenga chuki baina yetu. Sisi sote ni watanzania, tuulinde utaifa wetu. CCM, Chadema, ACT, CUF haiwezi kuwa muhimu kuliko utu wako na utaifa wako. Heshimu kila mmoja bila kijali ni wa chama chako au lah. Tujifunze kuwa na siasa za kujadili masuala badala ya kuattack personality.

Tukiwa na siasa za kujadili issues hatuwezi kuwa maadaui kwa wafuasi wa vyama vingine. Tutafanya siasa, tutabishana na kushambuliana kwa hoja, lakini nje ya siasa tutaheshimiana na kushirikishana mambo mbalimbali. Mimi ni mwanachama hai wa Chadema kwa miaka 9 sasa lakini nina ndugu na marafiki wengi ambao wapo CCM na vyama vingine. Wengine mawaziri, wengine wabunge, wengine viongozi wa kada mbalimbali na wwngine wanachama wa kawaida. Nje ya siasa tunakula pamoja, tunafurahi pamoja, tunashirikiana na kusaidiana.

Majuzi gari yangu ilipasuka tairi nikiwa mbele kdg ya Kibaigwa, na sikua na Spear tyre, nikampigia simu rafili yangu ambaye ni mwanaCCM na ni kiongozi wa serikali, akatuma gari ikaniletea spear tairi kutoka Dodoma. Siasa haipaswi kutufanya maadui, siasa haipaswi kutujengea chuki, dharau, au dhihaka dhidi ya wengine. Nje ya siasa sisi sote ni binadamu wenye usawa na tunastahili kuheshimiwa utu wetu.

By the way hapa duniani sote tutapita na hakuna atakayeishi milele. Rafiki yangu Dr.Christopher Cyrilo anapenda kusema hakuna atakayeondoka hapa duniani akiwa hai (Nobody will leave this world alive). Sote tutakufa siku moja, sote tunapita, sote ni mavumbi. Lakini je ukifa utaacha nini kwa waliobaki duniani? Watakukumbuka kwa lipi?

Kwa heri Peter. Upumzike kwa amani. Safari yako hapa duniani imefikia tamati. Sisi tuliobaki kwenye safari hii ni jukumu letu kujitathmini na kujipima kwa matendo yetu. Mungu atujalie kuwa na mwisho mwema.!

Malisa GJView attachment 455068
siku zote nawaambia watu pumzi inawasumbua unakuta mtu anazungumza mambo ambayo dah !!!unajiuliza hivi huyu ni binadamu mwenye damu ama ni kiumbe cha sayari nyingine ama maana hajui alitendalo.pumzi s yako hujui inaeza kata sa ngapi bado mtu anajitutumua.Eee Mungu uturehemu sawasawa na wingi wa fadhili zako.Laiti tungekua tunayajua maisha baada ya pumzi kukata nahiisi dunia ingekua better place lakini na huku kutokujua pia bado haitupi nafasi ya kuogopa mhhhhhhh hii kali!!!!!!!!!
 
Mkuu sikulazimishi kuamini ninachokiandika ila huo ndio ukweli.

Jamaa alichanganyikiwa baada ya Pombe kushika nchi ila hakupenda kujionesha kuwa upande wa upinzani sijui kwa ajili ya kuona aibu .

Kwa sababu hawa ndugu zangu wapo wawili walipata huo mtihani mmoja alikimbilia kusoma Arusha mpaka leo yupo huko yeye alikuwa kahama ila sitotaja ofisi gani. Yeye pia alitamani kuacha kazi watu walimshauri aombe kibali ili akasome hapo kabla vibali vya kwenda kusoma havijaanza kuzuiwa.Ila huyu wa pili yeye ndio alikuwa timu Lowasa kabisa sasa kwa ile hofu tu ya kudhindwa bosi wake alizidi kukonda.

So subiri tukipata mwili na report ya kifo nitawapa habari kamili wala msiwe na shaka wandugu.

Inaonekana umefurahia sana kifo cha jamaa, maana dah.

Haya mkuu, ila ni kwetu sote.
 
Back
Top Bottom