TANZIA: Kada wa CCM Peter Kalihose afariki dunia

TANZIA: Kada wa CCM Peter Kalihose afariki dunia

Dah! bado nachelewa kuamini haya maneno yenu!!…………………………
 
Alifikiri akitukana atapata furaha hakuipata kaamua kujitoa uhai.tuangalie ndugu zetu wenye tabia hizi za ajabu lzima kuna matatizo fulani. Wana CCM wote wanataka wapate vyeo wasipopata stress za ajabu zinawapata. Poleni. Mbona maisha bila vyeo yapo tu na ni mazuri?
 
Mungu aipumzishe nafsi yake kwa amani.

Kumbu kumbu zangu zinaonyesha huyu alikuwa ni Miongoni mwa wale waliokashifu Sana afya ya Mzee Lowassa. Lakini kwa kuwa Mungu si mwanadamu yeye ametangalia na Lowassa yu ngali Hai.

Funzo kwetu tuliobaki, siasa zisitutoe utu wetu.
Kumbeee... Sir God anawapunguza mdogomdogo
 
Matendo yetu ya hapa duniani yanatokana na uhai ambao mungu anatupatia inapotokea mungu kaondoa pumzi yake kinywani mwetu basi huwa ni mwisho wa mtembeo wetu kwenye sura ya dunia hivyo ni vyema tusijihesabie haki kisa aliyetangulia mbele yetu alitenda vibaya

Kufeli kwa aliyembele yako hakukuthibitishii ushindi uliye nyuma yake,Yeye alishindwa kutumia busara zake vizuri,haina maana nyie mlioitumia wakati huo mtaitumia wakati wote,kuweni wastaarabu hizo post zake za FB zilishapita,kuzibandika hapa tena ni utoto kwa nini alivyokuwa hai hamkuzibandika ili naye angelipata wasaa wa kuzitetea hoja zake.
Tutazibandika ili liwe fundisho kwa wenye tabia kama yake.
 
mimi sio muumini wa siasa za kutukanana mitandaoni,ila jamaa alikuwa anakera sana hajui kujenga hoja zaidi ya matusi.
any way Mungu amsamehe makosa yake yote,apumzike kwa amani akisubiri ufufuo wa mara ya pili.
bwana alitoa na bwana ametwaa
 
Huyu jamaa ni ndugu yangu na hivi ninavyoongea mwili bado haujafika Kasulu.

Inavyosemakana (bado hatujathibitisha wanandugu mapaka tuuone mwili wake ndio tutalithibitisha hilo) amejichoma visu mwilini kwa lengo la kujitoa uhai kwa sababu maisha ni magumu kwa upande wake.
Hizi habari za kujidhuru kwa kisu zimetolewa na mwanamke aliyekuwa akiishi naye huko Uganda.

Mara kwa mara alikuwa anapiga simu kwa kaka yake anaitwa Majaliwa Andrea Kalihose akimlalamikia kuwa maisha yamempiga sana kiasi anakosa hata namna ya kusonga mbele.
Pia kuna kipindi alikoswa koswa kuuawa na watu wasiojulikana baada ya kumkimbiza muda mrefu alinusurika baada ya kuingia kwenye vichaka.

Kabla ya hapo alikuwa ni mfanyakazi wa serikalini ila alivyoingia bwana Pombe madarakani alimtumbua huyu bwana kwa ubadhirifu katika ofisi yao. Baada ya hapo akaenda Uganda kutafuta maisha kwa njia nyingine.

Nikipata muda nitawapa update kwa jinsi tutakavyoupokea mwili wake.

Hii mbona haijakaa sawa. Post yake ya mwisho (Desemba 2016) iliyopo hapa inaonyesha jamaa alivyokuwa mpiganaji wa CCM dhidi ya upinzani na ufisadi "wanaouendekeza". Lini alikutwa mbadhirifu hadi kutumbuliwa na Magufuli? Halafu inawezekana kuwa alikuwa mgonjwa wa akili? Ni habari ya kushangaza hii; haiunganiki vizuri.
 
Apandacho mtu ndicho atakachovuna,
even you, even me .Kuna maisha baada ya siasa na baada ya kifo
 
Kwa matusi haya huna budi kutangulia huko!! .. yaani utukane halafu umwombe Mungu huyo huyo akubariki? Mungu hadhihakiwi.
 
So sad, Peter Kalihose nimemfahamu tukiwa form 2, baada ya yeye kuhamia shuleni kwetu.

Alikuwa ana akili sana, maana nakumbuka alikuwa anawafundisha jamaa wa Form 4 mwaka huo huo na hata wakati tuko form 3 aliendelea na utaratibu wake wa kuwafundisha jamaa waliokuwa form 4 masomo kama physics, hesabu, chemistry na biology.

Form 4 alichaguliwa kwenda Shinyanga Sekondari na aliendelea kukimbiza darasani kwa sababu ya uelewa mkubwa wa mambo aliokuwa nao.

Bahati mbaya hakuweza kuendelea na shule kwa sababu ya kuumwa mara kwa mara, muda mwingi alikuwa anautumia hospitali zaidi ya darasani.

Form six alimalizia shule moja ya Dar es Salaam, degree yake amefanyia Tumaini Iringa.

Ni moja ya watu niliokuwa ninaukubali uelewa wake kuanzia mambo ya shule mpaka yasiyo ya shule.

RIP Bro.
 
Back
Top Bottom