chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 20,691
- 25,830
Kwa taarifa tulizonazo ni kwamba ndugu na rafiki yetu Peter Kalihose hatunaye tena.
Peter Kalihose kwa taarifa za awali zinadai kuwa kilichomuua ni Ugonjwa wa Kisukari huko Kampala nchini Uganda.
Taarifa za awali zinadai pia kuwa mwili utasafirishwa toka Uganda hadi Kasulu mkoani Kigoma.
Tunaendelea kufuatilia zaidi kupata habari za uhakika za Kada huyu machachari wa Chama cha mapinduzi.
Njia yetu ya kumrudia Mola ni Moja tu kwake leo kesho kwetu....
Rest in Peace Peter.

Huyu jamaa ni ndugu yangu na hivi ninavyoongea mwili bado haujafika Kasulu.
Inavyosemakana (bado hatujathibitisha wanandugu mapaka tuuone mwili wake ndio tutalithibitisha hilo) amejichoma visu mwilini kwa lengo la kujitoa uhai kwa sababu maisha ni magumu kwa upande wake.
Hizi habari za kujidhuru kwa kisu zimetolewa na mwanamke aliyekuwa akiishi naye huko Uganda.
Mara kwa mara alikuwa anapiga simu kwa kaka yake anaitwa Majaliwa Andrea Kalihose akimlalamikia kuwa maisha yamempiga sana kiasi anakosa hata namna ya kusonga mbele.
Pia kuna kipindi alikoswa koswa kuuawa na watu wasiojulikana baada ya kumkimbiza muda mrefu alinusurika baada ya kuingia kwenye vichaka.
Kabla ya hapo alikuwa ni mfanyakazi wa serikalini ila alivyoingia bwana Pombe madarakani alimtumbua huyu bwana kwa ubadhirifu katika ofisi yao. Baada ya hapo akaenda Uganda kutafuta maisha kwa njia nyingine.
Nikipata muda nitawapa update kwa jinsi tutakavyoupokea mwili wake.