TANZIA: Kada wa CCM Peter Kalihose afariki dunia

TANZIA: Kada wa CCM Peter Kalihose afariki dunia

Mzee lowassa alitukanwa sana lakini kwa busara zake hakujibu chochote. Sasa mungu ameamua kutoa makucha dhidi ya hao watukanaji. Kama ulimtukana lowassa basi chonga kabisa jeneza la kukuzikia. Huyu ndiye alimtukana sana lowassa mwache afe tu na wengine watafuata
 
Hivi mbona kila kifo cha kada wa ccm kinahusishwa na kumkashifu lowassa. Kwani lowassa ni mtoa roho acheni kumsingizia ujinga mzee wa watu. Kifo ni Mungu tu anaeamua. Hakuna mpinzani ambaye hakuwa anamwita lowassa fisadi na ni kashfa kubwa ila leo mnatumia mgongo wa lowassa kusimanga watu. Acheni hizo bana. Na wewe unaeshangilia utakufa tu hata kesho hata kama haujamkashifu mtu. Acheni kazi ya Mungu ifanywe na Mungu. Rip Peter
 
Kuna mtu ameeleza hapa kwamba marehemu amejichoma kisu kwenye baadhi ya sehemu za mwili wake kutokana na maisha magumu aliyokumbana nayo huko nchini Uganda. Nimejiuliza sana kwamba licha ya marehemu kutumika na CCM kuwatusi viongozi wa upinzani akiwemo Edward Lowasa, bado hakulipwa chochote hata anaamua kujiua? CCM waache tabia ya kuwalaghai wanachama wao.
 
Taarifa bado wana ndugu hawacomfirm watu wanaanza kuandika rip hii ni kutiliana gundu asee
Huyu jamaa ni ndugu yangu na hivi ninavyoongea mwili bado haujafika Kasulu.

Inavyosemakana (bado hatujathibitisha wanandugu mapaka tuuone mwili wake ndio tutalithibitisha hilo) amejichoma visu mwilini kwa lengo la kujitoa uhai kwa sababu maisha ni magumu kwa upande wake.
Hizi habari za kujidhuru kwa kisu zimetolewa na mwanamke aliyekuwa akiishi naye huko Uganda.

Mara kwa mara alikuwa anapiga simu kwa kaka yake anaitwa Majaliwa Andrea Kalihose akimlalamikia kuwa maisha yamempiga sana kiasi anakosa hata namna ya kusonga mbele.
Pia kuna kipindi alikoswa koswa kuuawa na watu wasiojulikana baada ya kumkimbiza muda mrefu alinusurika baada ya kuingia kwenye vichaka.

Kabla ya hapo alikuwa ni mfanyakazi wa serikalini ila alivyoingia bwana Pombe madarakani alimtumbua huyu bwana kwa ubadhirifu katika ofisi yao. Baada ya hapo akaenda Uganda kutafuta maisha kwa njia nyingine.

Nikipata muda nitawapa update kwa jinsi tutakavyoupokea mwili wake.
 
NimefurAhi huyu f[emoji1] ala kufa!

Una swali lingine??
Huyu jamaa ni ndugu yangu na hivi ninavyoongea mwili bado haujafika Kasulu.

Inavyosemakana (bado hatujathibitisha wanandugu mapaka tuuone mwili wake ndio tutalithibitisha hilo) amejichoma visu mwilini kwa lengo la kujitoa uhai kwa sababu maisha ni magumu kwa upande wake.
Hizi habari za kujidhuru kwa kisu zimetolewa na mwanamke aliyekuwa akiishi naye huko Uganda.

Mara kwa mara alikuwa anapiga simu kwa kaka yake anaitwa Majaliwa Andrea Kalihose akimlalamikia kuwa maisha yamempiga sana kiasi anakosa hata namna ya kusonga mbele.
Pia kuna kipindi alikoswa koswa kuuawa na watu wasiojulikana baada ya kumkimbiza muda mrefu alinusurika baada ya kuingia kwenye vichaka.

Kabla ya hapo alikuwa ni mfanyakazi wa serikalini ila alivyoingia bwana Pombe madarakani alimtumbua huyu bwana kwa ubadhirifu katika ofisi yao. Baada ya hapo akaenda Uganda kutafuta maisha kwa njia nyingine.

Nikipata muda nitawapa update kwa jinsi tutakavyoupokea mwili wake.
 
Eeeeeh mwenyezi Mungu mlehemu sawa sawa na matendo yake aliotenda hapa duniani, kama alizingua nawe mzingue..
 
Mnashangilia mno kama kweli ni marehemu apumzike kwa amani..... Ila mambo yenu sio poa huko mbeleni tuendako wajanja watajilinda ila sie waropokaji ndio shida....... Tunajifanya wastaarabu kweli humu Jf kumbe ni sawa na firauni tu hatuna tofauti........ But there is something wrong to observe this kind of ruthless behaviors..... Mtu amefariki basi muda wake umeisha duniani, hata muongee wee hawasikii nyie tena ila tunajengeana chuki tu humu.....
 
Nimeshtushwa na taarifa za kifo cha Ndugu Peter Kalihose, mwanachama na kada hodari wa CCM mitandaoni ambaye alikua akikisaidia sana chama chake hasa kwenye propaganda. Lakini kifo cha Peter kitupe somo sisi tuliobaki hai.

Pamoja na umahiri wa Peter katika kujenga hoja lakini alikua bingwa wa kuattack personality. Matusi aliyoyatoa kwa Lowassa mengine hayaandikiki. Aliwahi kumuita mgonjwa, dhaifu, na marehemu mtarajiwa. Bahati mbaya hakuna kiongozi wa CCM aliyemkemea dhidi ya lugha hizo za matusi.

Leo Peter ametangulia amemuacha yule aliyemuita marehemu, maiti inayotembea, mgonjwa, na dhaifu akizidi kuimarika na kujenga chama chake. Ni vizuri tuishi tukijua maisha ya hapa duniani ni ya muda tu na siku moja sote tutatoweshwa. Hatuna mji udumuo hapa. Lakini jiulize utakapoondoka utaacha alama gani nyuma yako? Alama utakayoiacha itafuatana na matendo yako.

Usijivunie uzima ulionao. Uzima na ugonjwa ni majaliwa ya Mwenyezi Mungu. Kama wewe ni mzima mshukuru Mungu na waombee walio wagonjwa. Katika malezi yangu nilifundishwa kila nisalipo nisisahau kuwakumbuka wagonjwa, yatima na wajane. Sio kuwadharau, kuwadhihaki, wala kuwapuuza. Huenda Peter alijiona ana nguvu kuliko Lpwassa, ni imara kuliko Lowassa, ana afya bora kuliko Lowassa akasahau kuwa aliyempa afya hiyo ni Mungu, tena kwa neema tu.

Simlaumu Peter, ya kwake yamepita na hatuna lolote la kubadilisha aliyosema. Tunachopaswa kujifunza kupitia Peter ni kwamba katika maisha yetu tusijivunie uzima tulionao, wala tusiwadhihaki tunaoona wana afya zilizodhoofu. Mpaji wa yote ni Mungu mwenyezi. Ayubu aliwahi kudhoofu mwili akabakia mifupa, akapoteza mali na watoto wake wote. Lakini hakufa. Waliokua na afya walikufa wakamuacha. Baadae Mungu akamnyanyua Ayubu na kumpa afya bora, mali na watoto wengine.

Tusiruhusu siasa kujenga chuki baina yetu. Sisi sote ni watanzania, tuulinde utaifa wetu. CCM, Chadema, ACT, CUF haiwezi kuwa muhimu kuliko utu wako na utaifa wako. Heshimu kila mmoja bila kijali ni wa chama chako au lah. Tujifunze kuwa na siasa za kujadili masuala badala ya kuattack personality.

Tukiwa na siasa za kujadili issues hatuwezi kuwa maadaui kwa wafuasi wa vyama vingine. Tutafanya siasa, tutabishana na kushambuliana kwa hoja, lakini nje ya siasa tutaheshimiana na kushirikishana mambo mbalimbali. Mimi ni mwanachama hai wa Chadema kwa miaka 9 sasa lakini nina ndugu na marafiki wengi ambao wapo CCM na vyama vingine. Wengine mawaziri, wengine wabunge, wengine viongozi wa kada mbalimbali na wwngine wanachama wa kawaida. Nje ya siasa tunakula pamoja, tunafurahi pamoja, tunashirikiana na kusaidiana.

Majuzi gari yangu ilipasuka tairi nikiwa mbele kdg ya Kibaigwa, na sikua na Spear tyre, nikampigia simu rafili yangu ambaye ni mwanaCCM na ni kiongozi wa serikali, akatuma gari ikaniletea spear tairi kutoka Dodoma. Siasa haipaswi kutufanya maadui, siasa haipaswi kutujengea chuki, dharau, au dhihaka dhidi ya wengine. Nje ya siasa sisi sote ni binadamu wenye usawa na tunastahili kuheshimiwa utu wetu.

By the way hapa duniani sote tutapita na hakuna atakayeishi milele. Rafiki yangu Dr.Christopher Cyrilo anapenda kusema hakuna atakayeondoka hapa duniani akiwa hai (Nobody will leave this world alive). Sote tutakufa siku moja, sote tunapita, sote ni mavumbi. Lakini je ukifa utaacha nini kwa waliobaki duniani? Watakukumbuka kwa lipi?

Kwa heri Peter. Upumzike kwa amani. Safari yako hapa duniani imefikia tamati. Sisi tuliobaki kwenye safari hii ni jukumu letu kujitathmini na kujipima kwa matendo yetu. Mungu atujalie kuwa na mwisho mwema.!

Malisa GJView attachment 455068
Hiv dhaifu aliyoitamka Peter ina utifauti na aliyoisema Mbowe..?
Yericko aliposema Lowasa anapigania siku tu aondoke kwa ugonjwa wa KIHARUSI ni tofauti na alkvyosema Peter au kwa kuwa hakutaja ugonjwa..?
Acheni unafiki nyie binadamu.
 
Upumzike kwa amani.. Hongera wanasiasa wa upinzani kwa kuendelea kufanya siasa kwenye kifo cha mwenzetu, linapokuja swala la kifo siasa tuweke pembeni
Sasa mbona mlikuwa watabiri wa vifo vya wapinzani.Any way R.i.p kada.
 
Umeongea ukweli mtupu kabisa, na wale wanaokashifu afya za wenzao kana kwamba wao wataishi milele na hawataugua sijui tuwaweke upande gani wa wanasiasa au wapiga domo. Ila mwisho wa yote tuwe tunaweka akiba ya maneno tunapozungumzia jambo lolote linalohusu viumbe wa Mwenyezi -Mungu.
Wakati mnamuita Lowasa ni maiti uliwahi kumkanya huyu Peter Kalihose?
Kwakweli sijaguswa wala kusikitishwa na kifo cha mtu huyu, huo ndio ukweli unafki kwangu mwiko
 
Aliwazalo mjinga ndilo litakalomtokea

Alimtukana Mamvi siyo!!! kamwe usimtakie adui yako maovu else hayo maovu utaanza kuyaonja wewe au immediate generation yako, hence take precaution. This is termed as a 'curse'(laana) na inawatafuna wengi sana bila wao kujua!
 
Back
Top Bottom