Tanzania: Utawala bora vs Rushwa

Tanzania: Utawala bora vs Rushwa

aah nimekupata kumbe huna imani na vyombo vya adala Tanzania? basi waambie hao Chadema wasiingie bungeni maana wao ndio wanapita kuwaambia wananchi au na wao wanajali matumbo yao?

kaazi, hata hivyo mambo yamo kwenda jana sio leo tumo tunapiga hatua.

Mbona hiyo kazi ya kuwaambia unaiweza kabisa wewe... au nayo unataka kumwachia mzee wenu alokaribia kufa kwa uzee Kingunge!
 
Nani anamshauri Mzee Ngombale?.Sidhani kama anastahili kabisa kuingia ktk Vurugu hili.Yeye pia ni mchafu mno,na kuingia kwake hapa kutetea hawa Mafisadi kutasababisha nae awekwe wazi.Jamani waungwana mnaoonana na huyu Mzee,mwambieni kuwa bado ana "Heshima miongoni mwetu"si ustaarabu wala utamaduni wetu kumchungulia mkubwa akikaa vibaya!,sasa Mzee, si kuchunguliwa tu!,anatulazimisha kumvua nguo hadharani.Hatutaki kufika huko.Mzee waachie vijana wako wa propaganda kuwatetea akina JK,BMW na EL Lakini sio wewe,You know better than that!!!!
 
Mwawado.. hata mimi nimeuliza watu wa nyummbani.. nimjibu mzee huyu au tumwachilie inawezekana ni uzee na ujiko unamsumbua. Maana kati ya watu ambao sitaki kulumbana nao ni wazee kama hawa.. but then wakati mwingine wanatulazimishe kufanya mambo haya kwa shingo upande.
 
Viongozi CCM kuzunguka nchi nzima kujibu hoja za wapinzani
Abdallah Bawazir na Muhib Said

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimepanga kutumia viongozi wake wa kitaifa hadi matawi kueleza ukweli wa shutuma zilizotolewa na Mbunge wa Karatu, Dk Wilbroad Slaa, dhidi ya viongozi wa serikali na chama.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Aggrey Mwanri, alisema ili kujisafisha na tuhuma hizo, viongozi wa chama hicho kuanzia ngazi ya taifa hadi matawi, watazunguka nchi nzima kueleza ukweli wa suala hilo ili kuisafisha serikali na CCM.

�Chama chetu kina mtandao mkubwa, tutatumia njia ya kujisafisha kwa kuwaeleza wananchi ukweli. Viongozi wetu watazunguka nchi nzima kuzungumza na wananchi ili wazipuuze kauli za wapinzani ambao wao wenyewe wamedai kuwa nia yake ni kuwafanya wananchi wakichukie serikali ya chama hicho, jambo ambalo hatulikubali,� alisema.

Alipotakiwa na waandishi wa habari kueleze kama tuhuma zilizotolewa hazina ukweli ni kwanini chama hicho kisichukuwe hatua za kisheria, alisema chama chake hakina mpango wa kwenda mahakamani.

�Tunaamini kuwa Watanzania wanaheshimu utawala wa sheria, hivyo kama kuna mtu yoyote mwenye ushahidi kuhusu tuhuma za ubadhirifu au rushwa katika vyombo vya umma, basi aupeleke ushahidi huo katika vyombo vya dola kama Takukuru, polisi, Usalama wa Taifa na vinginevyo,� alisema.

Katika tamko hilo alisema chama hicho pia kinaunga mkono kauli ya serikali iliyotolewa hivi karibuni na Waziri Nchi, Ofisi ya Rais ( Siasa na Uhusiano wa Jamii), Kingunge Ngombale-Mwiru kuhusiana na tuhuma za Dk Slaa.

Akisoma tamko la CCM kuhusiana na tuhuma hizo za wapinzani Mwanri, alidai kuwa chama hicho kimebaini kuwa nia ya vyama vya upinzani ni kutaka kukichafua na kukichonganisha na wananchi, jambo ambalo halitakivumilia.

�Shabaha ya vyama vya upinzani ni kuichafua serikali ya CCM mbele ya umma ili kujitafutia umaarufu wa kisiasa nchini. Wanataja majina ya viongozi hadharani bila ya kuwa na ushahidi wowote , kinachosikitisha anatajwa hata Rais aliyechaguliwa na asilimia 80.2 ya wananchi kutokana na imani waliyonayo kwake. Jambo hili halikubaliki hata kidogo,� alisema Mwanri.

Nao Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), umesema unaunga mkono kauli ya Kingunge na kusema wanaamini tuhuma hizo zimejaa upotoshaji wenye lengo la kujenga chuki dhidi ya serikali, kuwapaka matope viongozi na kuhatarisha amani.

Taarifa ya UVCCM iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana ilieleza kuwa kitendo cha kutunga tuhuma za uongo na kisha kuanzisha kampeni maalum ya kuzizungumza ili kuwafanya wananchi waziamini imekuwa ikifanywa na wapinzani kwa muda mrefu sasa.

"Mfano hai ni tukio la hivi karibuni la kusema uongo bungeni lililofanywa na Zitto kuhusiana na mkataba wa mradi wa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi. Alishindwa kuthibitisha madai yake akasimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge kwa kusema uongo.

Ni wapi mtu muongo akaitwa shujaa? Hizi ni propaganda za wapinzani kuficha ukweli, alisema sehemu ya taarifa hiyo iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Amos Makalla na kuongeza:

"Kwa hulka hiyo UVCCM haishangazwi na hatua nzima ya umoja wa wapinzani ya kuja na madai mengine dhidi ya viongozi wa CCM, serikali na taasisi zake".
Source-MWANANCHI
 
Sasa CCM wameishiwa kama wameanza copy and paste. Ukiona hivyo wanakaribia kuumbuka na kizee chao Kingunge
 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Aggrey Mwanri, alisema ili kujisafisha na tuhuma hizo, viongozi wa chama hicho kuanzia ngazi ya taifa hadi matawi, watazunguka nchi nzima kueleza ukweli wa suala hilo ili kuisafisha serikali na CCM.

Hivi unawezaje kujisafisha wakati umekubali 3% na kuwapa mafedhuli 97%. CCM naona wanaota ndoto za mchana ambazo matokeo yake huwa mabaya.
 
Mwawado.. hata mimi nimeuliza watu wa nyummbani.. nimjibu mzee huyu au tumwachilie inawezekana ni uzee na ujiko unamsumbua. Maana kati ya watu ambao sitaki kulumbana nao ni wazee kama hawa.. but then wakati mwingine wanatulazimishe kufanya mambo haya kwa shingo upande.

Mkijiji,
kayataka mwenyewe mpeni dozi ya uhakika teh teh, ndo kumkoma nyani kumbe unapendwa umri hapa? mpeni tu...x 3!
 
waungwana wa JF,Ile Document ya Dr Slaa ipo kwenye pdf.Ni vyema isambazwe kwa kila mwenye access ya e-mail ili watu waione kama ile ya Uizi wa BOT.Kwa kuiona doc hiyo Wazalendo watachuja ukweli na Uongo!!!
 
Mie leo nimehakikisha hard copy kumi na kitu hivi, zimetolewa kupelekwa huko kunako ambako mtandao haufiki!

Jamani uki print hata copy 10 ukazituma kule kijijini ni jambo jema pia. Tuungane kieleweke! Vinginevyo hawa mafisadi wanaimaliza nchi aisee!!
 
Kuna makala kwenye Mwananchi (hapa nilipo shambani siwezi kuingia kule) inayoelezea maneno ya Mwanri na inathibitisha nilichokisema hapo nyuma (jana) kuwa CCM wana mkakati wa kujibu hoja kwa kupuuzia. Katika habari hiyo wanasema wamekusudia kwenda nchi nzima kujibu mashambulizi na tuhuma za wapinzani. Kuna mtu anaweza kuiweka hapa makala hiyo ya Mwananchi?
 
Huna point kabisa wewe.

Wapinzani wanachafua heshima ? Heshima za akinanani?
Wizi kwenu ni kazi halali ya kujiajiri?

Wezi wa Fedha za Umma na Majambazi wa silaha nani anaua watu wengi zaidi kwa pamoja?
 
Maelezo ya Mwanri hayo hapo MKJJ kama yalivyoripotiwa na Gazeti la Mwananchi.

Abdallah Bawazir na Muhib Said

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimepanga kutumia viongozi wake wa kitaifa hadi matawi kueleza ukweli wa shutuma zilizotolewa na Mbunge wa Karatu, Dk Wilbroad Slaa, dhidi ya viongozi wa serikali na chama.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Aggrey Mwanri, alisema ili kujisafisha na tuhuma hizo, viongozi wa chama hicho kuanzia ngazi ya taifa hadi matawi, watazunguka nchi nzima kueleza ukweli wa suala hilo ili kuisafisha serikali na CCM.

�Chama chetu kina mtandao mkubwa, tutatumia njia ya kujisafisha kwa kuwaeleza wananchi ukweli. Viongozi wetu watazunguka nchi nzima kuzungumza na wananchi ili wazipuuze kauli za wapinzani ambao wao wenyewe wamedai kuwa nia yake ni kuwafanya wananchi wakichukie serikali ya chama hicho, jambo ambalo hatulikubali,� alisema.

Alipotakiwa na waandishi wa habari kueleze kama tuhuma zilizotolewa hazina ukweli ni kwanini chama hicho kisichukuwe hatua za kisheria, alisema chama chake hakina mpango wa kwenda mahakamani.

�Tunaamini kuwa Watanzania wanaheshimu utawala wa sheria, hivyo kama kuna mtu yoyote mwenye ushahidi kuhusu tuhuma za ubadhirifu au rushwa katika vyombo vya umma, basi aupeleke ushahidi huo katika vyombo vya dola kama Takukuru, polisi, Usalama wa Taifa na vinginevyo,� alisema.

Katika tamko hilo alisema chama hicho pia kinaunga mkono kauli ya serikali iliyotolewa hivi karibuni na Waziri Nchi, Ofisi ya Rais ( Siasa na Uhusiano wa Jamii), Kingunge Ngombale-Mwiru kuhusiana na tuhuma za Dk Slaa.

Akisoma tamko la CCM kuhusiana na tuhuma hizo za wapinzani Mwanri, alidai kuwa chama hicho kimebaini kuwa nia ya vyama vya upinzani ni kutaka kukichafua na kukichonganisha na wananchi, jambo ambalo halitakivumilia.

�Shabaha ya vyama vya upinzani ni kuichafua serikali ya CCM mbele ya umma ili kujitafutia umaarufu wa kisiasa nchini. Wanataja majina ya viongozi hadharani bila ya kuwa na ushahidi wowote , kinachosikitisha anatajwa hata Rais aliyechaguliwa na asilimia 80.2 ya wananchi kutokana na imani waliyonayo kwake. Jambo hili halikubaliki hata kidogo,� alisema Mwanri.

Nao Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), umesema unaunga mkono kauli ya Kingunge na kusema wanaamini tuhuma hizo zimejaa upotoshaji wenye lengo la kujenga chuki dhidi ya serikali, kuwapaka matope viongozi na kuhatarisha amani.

Taarifa ya UVCCM iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana ilieleza kuwa kitendo cha kutunga tuhuma za uongo na kisha kuanzisha kampeni maalum ya kuzizungumza ili kuwafanya wananchi waziamini imekuwa ikifanywa na wapinzani kwa muda mrefu sasa.

"Mfano hai ni tukio la hivi karibuni la kusema uongo bungeni lililofanywa na Zitto kuhusiana na mkataba wa mradi wa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi. Alishindwa kuthibitisha madai yake akasimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge kwa kusema uongo.

Ni wapi mtu muongo akaitwa shujaa? Hizi ni propaganda za wapinzani kuficha ukweli, alisema sehemu ya taarifa hiyo iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Amos Makalla na kuongeza:

"Kwa hulka hiyo UVCCM haishangazwi na hatua nzima ya umoja wa wapinzani ya kuja na madai mengine dhidi ya viongozi wa CCM, serikali na taasisi zake".
Source-MWANANCHI
 
Ngoja nijinukuu hapa kidogo:

Ngoja niwaambie kitu. Baada ya Ofisi ya Waziri Mkuu kukurupuka kujibu hoja ya "kupaa" na baada ya Maelezo kukurupuka na kujibu suala la "kuitwa wasanii" CCM wameamua kutumia njia nyingine kabisa nayo ni kupuuza. Kwa siku za karibuni angalieni na mtaona kuwa hawajibu hoja tena isipokuwa kutoa kauli za "kupuuzia". Hili la kina Dr. Slaa ni mwanzo tu.

Chochote ambacho kitasemwa na wananchi watawala wetu watajibu kwa kejeli na kudharau, hawataenda mahakamani kudai defemation, hawataandika makala kujibu tena, watawatumia kina Kingunge, Makamba na wapambe wao kutoa kauli za kejeli na kupuuzia.. mtasikia kauli kama "hao ni wapinzani hawana jingine la kufanya", "wana haki ya kutoa maoni yao na huo ndio uzuri wa demokrasia" Kitu pekee ambacho hawatafanya ni kujibu hoja kwa hoja.
Now, sisi wakosoaji tunabadili mwelekeo pia, mwelekeo ambao utawalazimisha wajibu hoja.

ndugu zangu haya ni mapambano ya kifikra na kuliko mapambano ya kisheria au ya kupigana ngumi, haya ya sasa, ushindi wake hautokei mezani. Kabla ya kushinda kwenye sanduku la Kura ni lazima tushinde kwenye mioyo ya watu.

Kosa kubwa walilolifanya wapinzani katika ziaza zao hasa kuanzia ile ya kwanza Jangwani, ni kutotoa mwaliko wa wana CCM waliochoshwa kurudisha kadi. Nilisema toka mwanzo wangefanya hivyo lakini majibu yalikuwa "hili ni suala la Taifa na si suala la kisiasa". Sasa CCM watawaonesha maana ya siasa ni nini. Watakapopita CCM mikoani mtaona jinsi watakavyofanya sombasomba wa upinzani and this time it'll be with a vengeance!

Laiti ningekuwa Chief Strategist ya Muungano wa Upinzani.....
 
�Shabaha ya vyama vya upinzani ni kuichafua serikali ya CCM mbele ya umma ili kujitafutia umaarufu wa kisiasa nchini. Wanataja majina ya viongozi hadharani bila ya kuwa na ushahidi wowote , kinachosikitisha anatajwa hata Rais aliyechaguliwa na asilimia 80.2 ya wananchi kutokana na imani waliyonayo kwake. Jambo hili halikubaliki hata kidogo,� alisema Mwanri.

Hivi uongo mwingine jamani angalau wachukue muda kuufikiria! Rais Kikwete hakuchaguliwa kwa asilimia 80.2 ya "wananchi"....
 
Huu ni upuuzi.

Safari yao ya kujikosha huko mitaani itakubalika tu wakienda na Fedha au Polisi.

Wakienda mikono mitupu na nguvu ya ushawishi sithani kama watapata mafanikio.

Nawatakia safari njema katika kazi yao nzima ya kueneza Uongo.
 
Ngoja nijinukuu hapa kidogo:

ndugu zangu haya ni mapambano ya kifikra na kuliko mapambano ya kisheria au ya kupigana ngumi, haya ya sasa, ushindi wake hautokei mezani. Kabla ya kushinda kwenye sanduku la Kura ni lazima tushinde kwenye mioyo ya watu.

Kosa kubwa walilolifanya wapinzani katika ziaza zao hasa kuanzia ile ya kwanza Jangwani, ni kutotoa mwaliko wa wana CCM waliochoshwa kurudisha kadi. Nilisema toka mwanzo wangefanya hivyo lakini majibu yalikuwa "hili ni suala la Taifa na si suala la kisiasa". Sasa CCM watawaonesha maana ya siasa ni nini. Watakapopita CCM mikoani mtaona jinsi watakavyofanya sombasomba wa upinzani and this time it'll be with a vengeance!

Laiti ningekuwa Chief Strategist ya Muungano wa Upinzani.....

Mwanakijiji,

Hilo sio kosa. Huu mtindo wa kurudisha kadi ni wa kizamani kaisa wala si mkakati unaopaswa kuigwa na wapinzani. Kumbuka katika ziara hii wapinzani "walialikwa" hawakujiopeleka. Watu sasa wameshagundua kwamba CCM imekwisha, na ikitoa mshiko wanachukua, jukwaa wanapanda, Makamba akiondoka wanarejea na maisha yao ya kila siku. Mi naona hii ni mbinu safi kwa upinzani kwa sababu CCM inaufadhili kwa kuchukua infiltrators.

Wewe mwenywe ndiwe unasema ni mapambano ya fikra. Acha fikra zifanye kazi, wenye njaa washibe, lakini elimu imeshazama. Siri imo mioyoni mwa wananchi maana wanaona nani ananunua imani yao na nani anawaeleza ukweli unaotetea maisha yao. Acha wananchi wavune! Bahati mbaya uko mbali na Bongo, kazi iliyofanywa na wapinzani huku ni kubwa sana ni kama mvua ya masika ambayo haiwezi kukaushwa na jua la siku moja (ziara za CCM) hata kama ni kali kiasi gani.
 
Kichwa maji, kwenye siasa kuna vitu vinavyoitwa symbols! CCM imeweza kufanikiwa sana katika mikakati ya kisiasa kwa kutumia symbols yaani alama/ishara. Wanapokimbiza mwenge, wanapokata utepe, wanapovaa rangi zao za kijani na njano, n.k vyote ni alama mara nyingi havihusiani kabisa na kile kinachofanyika.

Sasa kiasili sisi waafrika ni watu wa alama na ishara (fikiria kwa undani kauli hiyo). CCM walipoanza mtindo wa kuzoa wapinzani na kuwapa nafasi mbalimbali n.k wanachezea ishara na alama. Ishara hizo zinasema kimsingi, "njoo CCM, mambo yako yatakuwa pouwa". Sasa utakuta mtu ambaye hana msimamo na ambaye anachotaka ni manufaa ya kwake na ya familia yake anajikuta hana jinsi isipokuwa kurudi CCM.

Sasa, upinzani wa kweli hauhitaji watu wa namna hiyo lakini unaweza kutumia alama/ishara pia kutimiza malengo yake. Mbinu hii ya kutumia hoja za mpinzani wako na matendo ya mpinzani wako kujenga hoja zako inaitwa "political triangulation". Ni mbinu iliyomsaidia Clinton kupata Urais.

CCM wanafahamu hilo na ndicho watakachokifanya. Watazunguka nchi nzima kama wapinzani ila zaidi, watazungumzia waliyozungumza wapinzani kwa kubeza, na wataanza kuzoa wenyeviti wa wilaya wa vyama vya upinzani n.k ili kuonesha kuwa wananchi wamekubali. Hivyo.... wakati kina Zitto na wenzake wanapiga hoja za "hii ni mali ya Taifa"... CCM kiujanja itakuwa inasema hii "ni mali ya Taifa ambalo linaongozwa na CCM, na CCM ndiyo wenye dhamana ya kulinda mali hiyo siyo wapinzani".

Kwa mtu wa kawaida, Chama kinachoongoza na chenye uwezo wa kulinda mali hiyo ni chaguo bora zaidi kuliko chama kisichoongoza na ambacho hakina uwezo wa kulinda mali isipokuwa kinasema kitalinda mali hiyo.

Hivyo, kimkakati na kisiasa, Wapinzani walikosea kutotumia nafasi ile kuwaalika wana CCM waliochukizwa na kitendo cha wabunge wao kumfungia Zitto. Nafasi hiyo imepotea na CCM watakaporudi watakuja na hoja ya kusema "wapinzani hawana mpango na hawana uwezo wa kufanya walichosema". Ni sisi mmetuamini na ni sisi tutawaletea Tanzania yenye neema... wakiwa wamevaa nguo zao za kijani na njano, huku TOT ikiburudisha, na nyimbo za CCM nambari one zikirindima.... utaona mazingaombwe ya hali ya juu yakitokea!!
 
Mwanakijiji you are right. wapo viongozi fuata upepo na wapo viongozi wenye dhamira ya kweli ktk upinzani. na ili kuwajua ni katika vipindi kama hivi kuelekea uchaguzi. ni vizuri wakajionyesha sasa kuliko wakijionyesha karibu na uchaguzi. Lakini pia in the long run wapinzani wa kweli na wanaokerwa na hali hii watabakia upinzani. Ni suala la kujipanga upya na inawezekana.

By the way, tuendelee ku circulate emails kwa marafiki zetu ili na wao waujue ukweli
 
Mkjj

Maono yako yanweza kuwa kweli kwamba wapinzani walikosea na ccm wananafasi ya kuwapiga bao kirahisi.

kwa hali halisi iliyopo mtaani inaweza kuwa kinyume na unavyofikiri, watu mtaani wamepigika na wamekosa matumaini, jambo la msingi ni kuupenyeza kwa nguvu ujumbe wa wapinzani ili wanachi watambue kupigika kwao kunatokana na ubadhirifu wa chama na serikali yake.

Tusikate tamaa, mpaka kieleweke.
 
Back
Top Bottom