Tanzania: Utawala bora vs Rushwa

Tanzania: Utawala bora vs Rushwa

mgumu ndio maana kuanzia matangazo yangu ya leo na maandishi ya wiki ijayo, naongoza mapambano ya preemptive strike ili kuneutralize wanachotaka kufanya CCM na ni lazima tushinde. Mapambano haya ya kifikra, fikra zenye nguvu ni lazima zipenyezwe kwa haraka zaidi na kwa urahisi zaidi.

Nashauri muwapatie watu link ya hapa Jamboforums au kule kwenye KLH News.. bado hatujawafikia watanzania wengi.
 
i am very curious to know what will be the peoples reaction. Unajua nilitarajia kuwa mzee Kingunge ndio angesimama Kidete kukemea rushwa, labda yeye angempa JK mwanga,support na ground ya kuanza kushughulikia rushwa. Lakini kauli aliyotoa imenisikitisha sana. Wazee ambao tunaona kama ni kisima cha busara ndani ya CCM ( Kingunge na Malecela) wameonesha kuwa hakuna la maana. I really can not imagine CCM inaelekea wapi, Mwalimu aliposema "WAHUNI NYIE" nadhani alimaanisha zaidi ya wale tuliokuwa tukiwafikria.
sasa hivi viongozi wa CCM walio on the ground wanasema wazi kuna tatizo la rushwa, na wananchi tunaamini. Lakini huyu mzee kweli amevurunda heshima yake ndogo aliyobakia nayo kutokana na umri wake.
 
Mkjj

Maono yako yanweza kuwa kweli kwamba wapinzani walikosea na ccm wananafasi ya kuwapiga bao kirahisi.

kwa hali halisi iliyopo mtaani inaweza kuwa kinyume na unavyofikiri, watu mtaani wamepigika na wamekosa matumaini, jambo la msingi ni kuupenyeza kwa nguvu ujumbe wa wapinzani ili wanachi watambue kupigika kwao kunatokana na ubadhirifu wa chama na serikali yake.

Tusikate tamaa, mpaka kieleweke.

Ni kweli kabisa, wananchi wanaonyesha wazi kuelewa ukweli, CCM walizoea kupiga porojo watu wakawaelewa, kipindi hiki wana hali mbaya maana wananchi wamepata mwamko wa kuchambua mambo hasa baada ya kuona vile nchi inaliwa wakati wao maisha yakiendelea kuwa mabaya..matukio ya hivi karibuni ya maandamano ya wafanyakazi na mabango hayakutokana na taarifa ya Slaa, ni ishara wazi kuwa wananchi sasa wamechoka na wana uelewa mkubwa wa mambo, sio enzi za porojo, ni enzi za facts na wnanchi wanazo, kina Slaa wamesaidia kuwathibitishia wnanchi kuwa kile wanachohisi kinatendeka na kweli...
CCM waende tu huko vijijini, watatupatia picha halisi iliyoko huko na sisi tuifanyie kazi ...
 
abasp2bkopieranr6.jpg


Wakati tuko busy kuwapa kazi wageni sisi tuendelee kubaki na mbavu za mbwa kama hizi.
Ihali wao wanakwenda kujenga kwao.




ache22bkopierahd5.jpg


Wakati gas tunayo nyingi tumeendelea kuweka mikataba isiyo na manufaa kwa Taifa
Nani hasa wanao-sabotage kila kitu kwenye serikali?




acc0003fu6.jpg


Hata maji tu ni shida kwenye karne ya 21.


Pictres: Credit Mjengwa blog
 
Duuuu!
Inasikitisha sana jamani hao ndo abilia wa ndege ya mheshimiwa EL
Kaazi kweli kweli!

Shida ya ufisadi tuliyo nayo tanzania ni kubwa sana, kwasababu mafisadi wenyewe ndio washika makali!

Njia pekee ni hii tu ya kila mmoja kwa sasa kuwa mpiganaji wa kuwaamsha walio lala kwamba jamani kumekucha tujizatiti ama la twafa!
 
Duh! halafu hiyo nyumba ya mbavu za mbwa iko katikati ya mji!
Na huko majuu nako wazee wamemtuknuku JK kwa kuondoa umaskini...
 
Viongozi CCM kuzunguka nchi nzima kujibu hoja za wapinzani
Abdallah Bawazir na Muhib Said

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimepanga kutumia viongozi wake wa kitaifa hadi matawi kueleza ukweli wa shutuma zilizotolewa na Mbunge wa Karatu, Dk Wilbroad Slaa, dhidi ya viongozi wa serikali na chama.


Nimesoma na kuielewa vizuri sana the PDF Doc. Kama hayo yaliyoandikwa humo ndani na vielelezo vilivyotolewa vipo, iweje huyu bwana aseme ni uongo? Ama hawajasambaziwa copy za hivyo vielelezo? Sidhani kama wangesema ni tuhuma za kutunga baada ya kupatiwa nakala.

Hawa wanadugu wanaona mambo yameanza kuwaendea kombo. Wameona wananchi wamepoteza imani kwao wanataka waanza kuwazoa tena kwa ahadi hewa. Na habari hizi zimekuja wakati muafaka kabisa kabla wananchi hawajasahu ufisadi unaoendelea CCMuni. Watu kupeana rushwa wao kwa wao kama salamu ya asubuhi halafu wanaseama watajisafishsa kwa wananchi jamani. Shame on all of you

another thing and why cant these people stick to what they say ama hawasikilizanagi wako busy kula rushwa. Correct me if am wrong people, according to the statement anna Makinda gave to the press zitto alitolewa bungeni kwa kutumia lugha chafu na sio kwa kusema uongo?

amani itahatarishwa na nini hapa? Labda nyinyi mafisadi muamue kuleta udikteta katika hii nchi ili kuwazuia watu kama hawa kusema maovu yenu katika kuhujmu taifa hili la wapenda amani. lakini kwa hatua ya wapinzani kusema waliyoyasema NAAAAAAAAAAAAH amani itakuwepo tele. Halafu ingekuwa bora sana kama wangeacha kutumia kisingizio hichi cha kupotea kwa amani. Amani itapotea pale tu wananchi watakapokosa haki zao na wakaamuua kuzidai kwa nguvu.

Hebu niambieni fedha zitakazotumika si ni kodi za watanzania ama mtasema ni fedha za chama si ndio? GOD BLESS THE POOR MAJORITY OF THIS COUNTRY.
 
mgumu ndio maana kuanzia matangazo yangu ya leo na maandishi ya wiki ijayo, naongoza mapambano ya preemptive strike ili kuneutralize wanachotaka kufanya CCM na ni lazima tushinde. Mapambano haya ya kifikra, fikra zenye nguvu ni lazima zipenyezwe kwa haraka zaidi na kwa urahisi zaidi.

Nashauri muwapatie watu link ya hapa Jamboforums au kule kwenye KLH News.. bado hatujawafikia watanzania wengi.

Mwanakijiji nipo na wewe, bila ya watanzania wengi kujua kinachoendelea fikira kubadilika haitatokea cha muhimu ni kusambaza info kadri tunavyoweza na kuwashawishi wao nao wasambaze kadri wawezavyo. Long live Jambo Forums.
 
Lets face it, hivi tulitarajia waseme nini? kwamba ni kweli wao wala rushwa! Give me a break!
 
Jamani ukweli ni kuwa Salva Ndio kampotosha huyu mzee wa watu kwa kujidai kuwa ameingia na mbio za kuwajibu wale wote wanaoichafua ikulu.

Kingunge hana facts na ameziomba muda huu na kapewa .

Kama ni kweli bado ni msafi basi baada ya kupewa facts aseme ukweli wa kile anachokiamini.
 
Maisha kwa watanzania wote sasa hivi yamekuwa magumu bila kujali huyu ccm, cuf, chadema, tlp n.k. Hii dozi ya awamu ya nne imempata kila mtu barabara kama chanjo ya ndui vile. Kwa hiyo tunachohitaji watanzania ni mtu wa kututoa hapa jangwani tulipo atakayetupeleka kwenye nchi ya ahadi. Sidhani kama hawa mafisadi watapata nafasi nyingine ya kutuongoza, waacheni tu waje kuzunguuka nchi nzima ndipo wataamini kweli watanzania tumechoka kudanganywa.Ila tu wawe "fair" waturuhusu tuwape ujumbe kupitia mabango yetu.
 
Maisha kwa watanzania wote sasa hivi yamekuwa magumu bila kujali huyu ccm, cuf, chadema, tlp n.k. Hii dozi ya awamu ya nne imempata kila mtu barabara kama chanjo ya ndui vile. Kwa hiyo tunachohitaji watanzania ni mtu wa kututoa hapa jangwani tulipo atakayetupeleka kwenye nchi ya ahadi. Sidhani kama hawa mafisadi watapata nafasi nyingine ya kutuongoza, waacheni tu waje kuzunguuka nchi nzima ndipo wataamini kweli watanzania tumechoka kudanganywa.Ila tu wawe "fair" waturuhusu tuwape ujumbe kupitia mabango yetu.

Oh,
Tatizo wanatumia ule udahifu wetu wa kusahau, pia wanatumia kule kupifgika kwetu, wanakuja na vi elfu 5 na kutuhadaa!

Nadhani kazi kubwa inabidi iwe juu yetu, hasa kufikisha ujumbe kule vijijini kwamba visenti mkiletewa kuleni tu ila fanya kweli kwenye masanduku ya kura!. Tumechoka jamani!

Hata wakenya wanavo tubeza na kutucheka pengine ni haki yao, kwani siye tumejaliwa kila kitu ardhi nzuri, madini, mito maziwa mbuga za wanyama, vyote hivyo lakini tumechoka mbaya!! Kisa ufisadi wa CCM,

Jamani watz amukeni twafa!
 
Kingunge tayari chenge amezikubali tuhuma wewe unapinga unataka kutuambia kitu gani?
 
Kingunge tayari chenge amezikubali tuhuma wewe unapinga unataka kutuambia kitu gani?

Hivi huoni kigugumizi na kujikangaya mara tuna puuza, mara tunaenda mikoani kujieleza kwa wanannchi ni kwamba ni aibu tupu!!

Kwani nondo za Siraha zimeenda shule, na utangulizi wake uko makini sana kisheria!. Ingekuwa hazina ukweli nadhani sasa hivi wangeisha mfikisha segerea! Sasa wamebaki kuweweseka tu, kwa kukatumia hako kazee ambako kameisha fikia 'negative growth' hata uwezo wake wa kufikiri ushakuwa choka mbaya!

Hapa inabidi watz tuamke tuishinikize serikali ijibu tuhuma moja baada ya nyingine na siyo propoganda, TUMECHOKA!
 
Jamani Mseee Kingunge ana semaje na hizi new Developments za Mkataba wa Buzwagi Kuvuja, na Hiyo Paper ya Dr Silaaa.
Nafikiri waandishi wa habari wamfuate ili wapate opinion ya Serekali ukitilia maanani Jk hayupo na Yeye ndio Mshauri wake wa Mambo ya Kisiasa (Zima Moto wa JK)
 
CCM bado wapo katika usingizi wa pono, hawana habari kwamba kulipambazuka masaa kadhaa yaliyopita. Ari mpya, nguvu mpya, speed mpya n.k. ilikuwa babaisha bwege sasa wanaona matunda yake.
 
CCM bado wapo katika usingizi wa pono, hawana habari kwamba kulipambazuka masaa kadhaa yaliyopita. Ari mpya, nguvu mpya, speed mpya n.k. ilikuwa babaisha bwege sasa wanaona matunda yake.

Labda kasi itaongezeka baada ya check up ya Afya New York/France
 
SERIKALI imetoa taarifa kujibu shutuma za rushwa kwa viongozi na watendaji wakuu wa serikali zilizotolewa na Mbunge wa Karatu kwa kupitia CHADEMA Dk. Wilbrod Slaa hivi karibuni.

Taarifa hiyo iliyotolewa Ijumaa Sept. 28, 2007 na Waziri ya Habari, Utamaduni na Michezo Mh. Muhammad Seif Khatib (pichani) imesema shutuma hizo hazina msingi wowote na zinastahili kupuuzwa.

"Tafsiri pekee na mantiki ya kutolewa kwa tuhuma hizi wakati huu ni kuwa hili ni jaribio la kuwavunja moyo wananchi kuhusu manufaa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005," imeeleza.

Imesema kwmba Serikali inapinga vitendo vya rushwa nchini "kwa nguvu zake zote" na kama Dk. Slaa na wenzake wana lengo la kupiga vita rushwa basi tuhuma hizo wangezifikisha katika vyombo vinavyohusika ili zishughulikiwe.


Dk. Slaa, akiwaongoza wanasiasa wenzake kadhaa wa kambi ya upinzani, walitoa tamko hadharani Septemba 15 mwaka huu kwenye viwanja vya Mwembeyanga, wilaya ya Temeke, mkoani Dar es Salaam, kuwatuhumu viongozi kadhaa wa umma kuwa wanashiriki vitendo vya rushwa.

Kufuatia tuhuma hizo, gazeti la kila wiki la MwanaHalisi linalotolewa jijini Dar es Salaam, limekuwa likisambaza tuhuma hizo bila ya kutafuta ukweli wake, taarifa imesema.

Taarika kamili ya Serikali inatarajiwa kuchapishwa ikiwa ni tangazo katika magazeti kadhaa ya kila siku Jumamosi Sept. 29, 2007.

Taarifa imesema Serikali ya Tanzania wakati wote imekuwa ikitekeleza mipango na mikakati mbalimbali ya kupambana na rushwa, awamu ya kwanza ya mwaka 1997/2004 na awamu ya pili mwaka 2005/2010.

Imenukuu Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005, Ibara ya 110, inayoelezea mapambano dhidi ya rushwa na tamko la Rais Jakaya Kikwete dhidi ya rushwa katika hotuba yake ya kuzindua Bunge Desemba 29, 2005.

Serikali imeanzisha Ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwenye Wilaya zote nchini, imeshughulikia taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na inashirikisha wananchi katika mapambano dhidi ya rushwa, imesema.

"Serikali isingebuni na kutekeleza mikakati hii kama isingekuwa na nia ya dhati ya kupambana na tatizo la rushwa [WINDOWS-1252?]nchini…Serikali haikutarajia kwamba watakuwepo miongioni mwetu watakaotumia fursa hizi kuibua taarifa za uzushi kwa lengo la kuchafua majina ya wenzao ili kujipatia umaarufu wa kisiasa wasioustahili," imeongeza.

Taarifa imesema Serikali inaelewa kwamba Dk. Slaa na wenzake ni miongoni mwa viongozi walioshiriki katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 wakitegemea kushinda lakini walishindwa na wananchi kuichagua CCM.

Imesema wananchi wanayaona mafanikio mengi katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kwamba wanachokitafuta wale walioshindwa ni kile walichokikosa na hivyo wanajaribu kuwahadaa na kuwachanganya wananchi.

"Serikali ya Awamu ya Nne ni imara na iko makini kutekeleza ahadi zake zote ilizowaahidi wananchi wakati ilipokuwa inawaomba ridhaa ya kuingia madarakani.

"Hivyo ni vyema wananchi wakatambua kwamba wapinzani hawa hivi sasa wanatapatapa na wanataka kutuondoa katika lengo letu la kuwaletea maisha bora Watanzania," imeongeza.
 
ADMINI: TAFADHALI, Ili kuwapo na mtiririko mzuri na kutokana na mitandao yetu ya BONGO kuwa pole pole sana... Hii iunganishwe kule katika, "Majibu ya serikali ya Kihuni" pia Kilio cha Mwanahalisi iliyowekwa na Ngurumo nayo iunganishwe na ile ya KILIO CHA MWANAHALISI ambayo tayari inachangiwa toka jana.
 
Back
Top Bottom