Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,798
- 12,240
Tukianza na Rais yeye anafikiri kuna watu wanamdharau kwa kuwa yeye ni mwanamke. Mawazo haya amekuwa nayo hata kabla hajaapishwa kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Na mara baada ya kuapishwa hotuba yake rasmi kama Rais alitamka kwa msisitizo kuwa yeye ni Rais mwanamke! Hali iliyoashiria kuwaonya wale waliomuona kama ni mwanamke na siyo kiongozi! Kutokana na fikra hizo alizonazo amekuwa akifanya maamuzi yasiyo sahihi anapokosolewa kisiasa na katika utendaji wake na viongozi hasa wa upinzani! Hili ameonyesha wazi kwa jinsi anavyoshughulikia suala la Mbowe kuwa anamdharau. Lakini pia ameonyesha jinsi anavyohamaki akikosolewa na viongozi wenzake ndani ya CCM.
Kiongozi wa pili mwenye matatizo haya ni Spika Ndugai ambaye anaona anashambuliwa katika mitandao ya jamii na pia kudharaulika na viongozi wenzake kwa sababu eti yeye ni MGOGO kwa kabila. Kwamba angekuwa anatoka kabila jingine yasingemkuta hayo madharau! Kutokana na hili na kwa kuwa anataka kuonyesha kuwa na wagogo wanaweza amekuwa akifanya na kuamua mambo kinyume cha Katiba na kuvunja sheria. Mambo haya aliyaonyesha kwa namna alivyoendesha bunge la serikali ya awamu ya tano kwa kuwanyanyasa wabunge wa Chadema kwa kuwafukuza hovyo kadri alivyojisikia. Aidha ameendeleza jambo hili la kuvunja Katiba na sheria kwa namna anavyoendelea kuwalea wabunge wasio na chama maarufu civid-19. Kwa sasa udhaifu wake wa fikra umepelekea aanze kukabiliana na wanachama wenzake wa CCM.
Wa tatu ni Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Juma ambaye baada ya kugundua hatoshi katika nafasi hiyo ameamua kujinyenyekeza kwa serikali, badala ya kulinda Katiba na sheria za nchi kwa kutenda na kuamua kwa haki masuala ya kisheria anafanya vile serikali inavyotaka! Hii ni hatari kubwa kwa mustakabali wa Taifa kwani mahakama sasa imekuwa chombo cha kugandamiza wananchi! Uhuru wa mahakama umetekwa na serikali na sasa muhimili yote mitatu ya dola; serikali, mahakama na bunge inashirikiana kuvunja Katiba na sheria! Viongozi wanafanya na kuamua wanavyotaka wenyewe bila kuheshimu katiba na sheria.
Wananchi tumebaki na jambo moja tu la kufanya, nalo ni kuendelea kupiga kelele na kuwazomea viongozi hawa kwa kadri tutakavyoweza hadi watakapojirekebisha kwani hatuna namna nyingine ya kufanya. Midomo yetu ndiyo silaha yetu!