Viongozi wakuu wa CHADEMA siyo maskini wala matajiri; wana amani na fikra huru. Kuna la kujifunza kwao

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,106
CHADEMA ina viongozi ambao siyo matajiri sana na siyo maskini sana. Siyo mafisadi wala hawana nafasi yakupata kipato kisicho halali. Wanafamilia sawa na viongozi wa CCM na wanavaa na kula kama wenzao wa chama tawala.

Pamoja na kuwa na kipato cha haki ila wako huru kueleza hisia zao kisiasa, kimaendeleo na kitaifa kwa kutumia akili na upeo waliopewa na Mungu.

Ni kundi lilitojiondoa kwenye kutawaliwa na lisilo na jambo lakuwafanya wamwabudu kiongozi. Fikra huru walizonazo unaweza ukatamani na wewe uwe na ndugu jamaa na marafiki anayeishi kwa haki na jasho lake.

Haya maisha ya posho yaliyopo CCM yamewafanya watu kutofanya kazi badala yake wanategemea sana kuelekezwa mipaka ya ifikiri. Tumeua talent za vijana wengi kwa kutegemea zidumu fikra za aliye juu. Hata akikosea tunashangilia, akipatia vivyo hivyo.

Natamani tuna watu katiba ya wana chadema wengi kwa kesho nzuri ya Tanzania. Hawa watu wanaotuaminisha kila kitu hatuwezi hadi wawekezaji wanatudumaza kufikiri. Wanatengeneza kizazi cha kuajiriwa kuliko kujiajiri. Mzazi mwongoze mwanao kujitegemea
 
Back
Top Bottom