Leo nmekutana na bango kwenye bajaji linapicha ya mdada halafu juu ya maandishi imeandikwa...

MAPENZI YA MAMA,
BUSARA ZA BABA..
Bado naendelea kutafakari jamaa alimaanisha Nini... Mwenye kujua anaweza kunisaidia maana yake...
 
... hivi ukivaa barakoa kumkinga jirani yako mwenye kinga ya mashaka kama unavyodai itakupunguzia nini? S hata maandiko yanasema mpende jirani yako? Kwa kuwa kinga yako ni imara hata humjali aliye dhaifu? Kwamba bora afe tu yanihusu nini? Hebu fikiria mara mbili rafiki; kila mwanadamu anahitaji kuishi!
Usitumie vibaya maandiko. Utafiti gani wa kisayansi unasema barakoa ni kinga? Kama barakoa ni kinga, huyo jirani aliyeivaa maana yake ana kinga kamili, sasa kwa nini umlazimishe asiyetaka avae?

Kumpenda jirani ni kwenye mvaa barakoa tu? Biblia inasema watendeeni wengine vile ninyi mngepaswa kutendewa. Wewe hupendi kulazimishwa kutovaa barakoa ila unamlazimisha mwingine kuvaa. Je huu sio unafiki na ufarisayo?

Lazimisheni watu kuvaa barakoa, ila msisingizie sayansi wala maandiko. Vyote haviko upande wenu. Semeni tu wazi sababu ni nini!
 
Hahaha, umekubali Sasa, au Waziri unaishi kama bendera kufuata upepo. Kujivukiza na formula ya dawa za mitishamba zimepotea. Lile tanuru la Kujivukiza pale muhas bado lipo.Ulijivukiza na baby yako ulimaanisha nini!?
 
... hivi ukivaa barakoa kumkinga jirani yako mwenye kinga ya mashaka kama unavyodai itakupunguzia nini? S hata maandiko yanasema mpende jirani yako? Kwa kuwa kinga yako ni imara hata humjali aliye dhaifu? Kwamba bora afe tu yanihusu nini? Hebu fikiria mara mbili rafiki; kila mwanadamu anahitaji kuishi!
Sasa Kama kinga yangu ni nzuri, huo ugonjwa wa kumwambukiza jirani nitautoa wapi?
 
COVID-19 kama magonjwa mengine ya virusi linapewa uzito usiostahili kwa sababu ambaye hachukui hatua za kujikinga au kuambukiza anaonekana wazi.

Lakini COVID-19 ni tofauti na HIV, ugonjwa ambao hadi sasa haujapata chanjo, ni wa siri, haujapewa nguvu ileile. Mwathilika wa HIV hajulikani na kuambukizana ni kwa tendo linalofanyika kisiri.

Ushauri, uhai uko mikononi mwa kila mtu kuchukua tahadhali.
 

Serikali ya Tanzania imeagiza wananchi kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa corona kwa kuvaa barakoa sehemu zenye mikusanyiko, ili kujikinga na wimbi la tatu lililoibuka katika mataifa mbalimbali.

Wakuu wa mikoa na wilaya wameagizwa kuhakikisha wanatimiza agizo hilo kwa kuzishirikisha kamati za afya ya msingi na kwamba watapimwa kulingana na utendaji wao.

Pamoja na hatua mbalimbali ambazo Tanzania imeanza kuchukua, Shirika la Fedha Duniani (IMF) limethibitisha kwamba litaipatia Tanzania mkopo wa dharura wa takribani dola milioni 574, itakapokamilisha mambo muhimu, ikiwemo utoaji wa takwimu kuhusu maambukizi ya virusi vya corona.

Akizungumza Juni 12 , Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamiii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Dorothy Gwajima aliagiza pia wananchi kuchukua tahadhari kwa kurejesha utaratibu wa kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka na matumizi ya vitakasa mikono ‘sanitizer’.

Alisema Tanzania inazungukwa na nchi nyingi Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla na kwamba inapokea wageni wengi kutoka nchi mbalimbali.

“Kamati iliyoundwa na Rais ilisema tupo salama, ila Mei 17 mwaka huu Brazil, India na nchi nyingine zilikuwa zinapigwa na wimbi la tatu la ugonjwa huu. Kwa hiyo wakasema hata sisi lazima tujitahadharishe na tujizatiti ili kuhakikisha wimbi hili haliingii kwetu, hivyo tusiliruhusu,” alisema Dk Gwajima.

Dk Gwajima alisema utaratibu wa kuvaa barakoa unapuuzwa, hali ambayo ni hatari, kwani Tanzania imezungukwa na nchi ambazo tayari zinapigwa na wimbo la tatu, ikiwemo Uganda na Congo.

Alisema Wizara pamoja na wataalamu katika viwanja vya ndege, mipakani pamoja na wananchi wanaotoka na kuingia wanaendelea kuchukua tahadhari.

“Tunashuhudia watu wamesongamana na hawavai barakoa, sasa wanatupatia kazi sisi mawaziri wa afya, viongozi wa Serikali kupambana na hali hii, sijasema ukienda shambani kulima uvae barakoa kwa kuwa huwezi kuvaa saa 24, lakini kuna mazingira ukishafika unaona kabisa hapa pana msongamano hewa haizunguki vizuri vaa,” alisema.

Alisema Serikali imeshatoa miongozo, kilichobaki ni utekelezaji, wananchi wachukue tahadhari.

Dk Gwajima alisema kazi ya kuelimisha wananchi inatakiwa ifanyike kuanzia ngazi za chini za wakuu wa wilaya kwa wakuu wa mikoa si kazi ya waziri peke yake au katibu mkuu.

Alisema kuna ulegevu katika kutoa elimu kwa wananchi, huku akisema mapema wiki hii Wizara imepanga kuitisha kikao pamoja na wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya.

“Kule waliko wana kamati zao zinazoitwa kamati za afya ya msingi, ambazo mwenyekiti wake ni mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya, wao wanatakiwa waite sekta zote zilizopo pale iwe ni elimu, kilimo, maji wajadili na kupeana kazi juu ya miongozo ambayo Wizara tumekuwa tukiitoa ili kufikisha elimu kwa wananchi,” alisema Dk Gwajima.

Chanzo: Mwananchi
Naina endicata ya lockdown ipo around... B.514 usd usilete mchezo... Tutaelewa tu...
 
🤔 Si ni huyu huyu alikuwa anasema tunywe Mizizi.
Kuna mkopo pesa za dharura kwenye Corona, wameambiwa waonyenyeshe kwanza kua wanashughurika na Covid-19 ndio wapewe.
Ndio sababu unawaonaona wananuka jasho kwa kuzifukuzia hizo hela.
Tuna serikali ya kiuni uni mno.
CCM imefeli sana kuongoza hii nchi
 
Hivi ni daktari gani hapa Tanzania anayeweza kuwaambia watanzania kwa ujasiri kuwa barakoa kwa uhakika inamkinga mtu dhidi ya kirusi cha corona. Hata barakoa za N95 hazina uwezo wa kuchuja virusi kwa asilimia 100! Surgical masks hazikutengenezwa kwa ajili ya kumlinda mvaaji dhidi ya virusi!! Kwa nini tunadanganyana mchana kweupe?
Huko ulaya na marekani na India karibuni wote wanaokutwa na maambukizi mapya kila siku ni wavaaji wa barakoa, na theluthi moja ya wanaokutwa na maambukizi mapya wamechanjwa chanjo ya kuwakinga na corona !!
Hakuna aliyethubutu hadi sasa kuweza kusema kuwa chanjo ya corona inamkinga mtu asiambukizwe virusi vya corona. Wenyewe wanasema "vaccine breakthrough infection" yaani maambukizi yanayopenya kwenye kinga ya chanjo. Wamelazimika kusema eti chanjo inapunguza watu WALIOAMBUKIZWA kulazwa hospitali kwa kuzidiwa na corona!
Huo ni uongo maana hata bila chanjo ni asilimia ndogo sana ndio wanaolemewa na corona kiasi cha kulazwa. Wengi wanapata corona bila hata kuonesha dalili zozote za ugonjwa, na wao wenyewe huwasema kama "Asymptomatic cases"!! na wengine huishia kupata mafua na kikohozi tu ambacho hujiishia chenyewe au huisha kwa kujifukizia au kwa kutumia limao na tangawizi! To most people, corona virus is just part of the NORMAL FLORA!!

Pori jipya nyani wale wale.
 
Nilikuwa sijui kama ulidungwa mimba na Mbowe!! Hongera Sana!!
sheed.png
 
Hiyo mimba uliyodungwa na mwendazake itakutoa roho kwa siku lazima umtaje mara 62!

Mdude alikamatwa na cocaine za mbowe akizisambaza mikoa ya nyanda za juu kusini
Sasa hapa Mbowe anahusika nini,yaani ukilitaja jina lake tu mimaji mwaaaa.
 
Wanambukizana wenyewe kwa wenyewe wasiojielewa...waliovaa hawaambukizwi....ila ukienda kwenye mikusanyiko vaa barakoa kuwalinda wengine.
Kama hamtozuia mikusanyiko na kutegemea kuvaa barakoa basi hayo ndio matumizi yasiyo sahihi ya barakoa, watu wakishavaa barakoa hujiona wako safe na kuacha kuzingatia hizo tahadhari zengine kama kunawa mikono au kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima.
 
Kama hamtozuia mikusanyiko na kutegemea kuvaa barakoa basi hayo ndio matumizi yasiyo sahihi ya barakoa, watu wakishavaa barakoa hujiona wako safe na kuacha kuzingatia hizo tahadhari zengine kama kunawa mikono au kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima.
Hv mikusanyiko isiyo yalazima ni yap? Na hyo c.19 ipo wap? Na matumiz sahihi ya barakoa ni yapi... Na zipi zenye ubora?? Je mbinu za mwanzoni zilizotufikisha happy zimefell au tunaintroduce wazojipya??
 
Dear my President and CiC, naomba uachane na hizi covid politics. Siyo nzuri kwa taifa na kwako pia. Zitaleta unnecessary social unrest kama tukianza kuzishadidia ili tupewe pesa. JPM na upuuzi wake wote, alifanya maamuzi sahihi kwenye corona. Leo tunaweza hata kuendesha nchi kwa sababu ya uamuzi wake. Angalia mambo nje ya box. Covid ni suala la usalama wa nchi. All the best.
 
Back
Top Bottom