Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 14,939
- 20,400
Baada ya maombi ya Tanzania kupata kibali kipya cha kuruhusu kupakia na kupakua mizigo kiitwacho Fifth Freedom Traffic Rights, ndege za ATCL sasa zimeruhusiwa kutua Nairobi.
Ndege za ATCL zikiwa njiani katika safari za kimataifa safari hii zitaruhusiwa kupakua na kupakia mizigo katika katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta.
Mapema leo asubuhi mamlaka ya usafiri nchini Tanzania ilitoa tangazo la barua kusitisha kutua kwa ndege za KQ katika viwanja vya ndege vya Tanzania (JNIA na KIA) baada ya mamlaka ya usafiri wa anga ya Kenya kuzuia ndege za ATCL kutua mjini Nairobi na kupakua na kupakia mizigo bila kufuata taratibu au kuwa na kibali cha kufanya hivyo.
Mamlaka hiyo ya Tanzania iliondoa vibali vya Third Right Freedom na kile cha Fourth Right Freedom ambavyo vinaruhusu shirika la ndege kusafirisha abiria na mizigo kupitia Nairobi kuelekea nchi ingine.
Baada ya mazungumzo kati ya pande hizi mbili mamlaka za Kenya zimetoa kibali cha Fifth Freedom Traffic Rights ambacho sasa kitaruhusu ndege za Tanzania zikiwa safarini kwenda Third Party Countries kutua Nairobi ili kupakua, na kupakia mizigo bila shida.
Hatua hii itairuhusu ATCL kuendelea na shughuli zake za kuhudumia mizigo na kuongeza mapato yake katika biashara hiyo ambapo itakuwa ikitumia ndege yake mpya ya mizigo.
Nini maana ya hizi Freedoms?
Kwa mujibu ICAO ambayo ni taasisi ya kimataifa ya umoja wa mataifa inoshughulika na usafiri wowote wa anga za kimataifa, hizi freedom rights mbili za kwanza ni kwa ajili ya transit ambapo mwenye ndege hulipa gharama za kutumia anga la nchi mwenyeji.
Rights ambazo zahusukupanga abiria na kushughulikia mizigo ztwa Traffic Rights.
Hivyo ICAO wametoa hizi freedoms ambazo zipo tisa lakini mbili za kwanza yaani First Freedom ambayo yaruhusu ndege kupita katika anga la nchi ingine bila kutua kwa kutumia anga yake. Second Freedom yaruhusu ndege ya nchi moja kutua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa nchi ingine kwa matengenezo au kujaza mafuta lakini bila kushusha abiria.
Third Freedom ni ile onoruhusu ndege kutoka nchi moja kwenda nchi ingine ikiwa na abiria au mizigo. Mfano ATCL ikitokea tanzania kwenda Kenya. Fourth Fredom ni ile inoruhusu ndege ilokwenda nchi ingine kurudi katika nchi ilokotoka ikiwa na abiria au mizigo.
Na Fifth Freedom Right ni kibali kinotolewa na nchi moja kwenda kwa nchi ingine kinoruhusu ndege za nchi ilopewa kibali kutua katika nchi mwenyeji na kisha kuruka tena kwenda katika nchi ya tatu au third country.
Zipo freedom rights zingine nne ambazo ama zaziruhusu ndege kutua, na kuondoka katika viwanja zaidi ya kimoja nai ile iitwayo Cabotage ambayo kama fifth freedom right ndege yatua na kufanya shughuli za kupakua na kupakia abiria au mizigo.
Hii ya Fifth Freedom Right yachochea ushindani na kuwawezesha wateja na wasafiri kuwa na uhuru wa kuchagua.