Uchambuzi: Kwanini serikali ipo sahihi kupiga ban ndege za Kenya

Labani og

JF-Expert Member
Sep 15, 2020
15,776
24,211
Kumekuwa na tension kubwa kutokana na katazo la serikali yetu kwa shirika la ndege la Kenya KQ kurusha ndege zake za abiria kuja Tanzania

Kumekuwa na hisia mseto juu ya hili, lakini mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

Nafafanua ifuatavyo: Kwenye dunia ya Aviation kuna kitu kinaitwa Chicago convention au Convention on International Civil Aviation.

Chicago convention ndio ilizaa wakala anga kimataifa ICAO (International Civil Aviation Organization)
ICAO ndio inaratibu na kusimamia sheria zote za huduma ya anga kama vile anga la kuruka, usajili wa ndenge, usalama nk

Chicago convention ilisainiwa kwa mara ya kwanza na majimbo 52 tarehe 7 December 1944 mjini Chicago, Illinois na ikaanza kutumika mwaka 1947

Turejee barua
Barua inaongelea kitu kinaitwa "Freedom traffic Rights"
Haya sio mataa ya barabarani kama ambavyo

Hizi ni HAKI za matumizi ya Anga, viwanja vya ndege, kubeba abiria, mizigo au vifurushi (mailings)

Zipo HAKI 9 kwenye Chicago convention
1st Freedom traffic Right

Haki ya kuruka kwenye anga la kigeni bila kutua

2nd Freedom traffic Right

Haki ya kutua kwa matengenezo au kujaza mafuta kwenye kiwanja cha ndege kisicho cha anga lako.

3rd

Haki ya kuruka kutoka kwenye kiwanja nchini kwako kwenda kiwanja cha ugenini

4th Freedom Traffic Right

Haki ya kuruka kutoka kiwanja cha ugenini kwenda kiwanja chako

5th Freedom Traffic Right

Haki ya kuruka kwenye nchi mbili za kigeni kwa safari inayoanzia na kuishia nchini kwako

Tusiendelee na haki nyingine kwani barua imetaja haki No. 3, 4 na 5. Serikali ya Tanzania ilikuwa imetoa ombi kwa serikali ya Kenya kuingiza ndege zake zote za mizigo zilizo chini ya Air Tanzania nchini humo kupitia mgongo wa 5th Freedom Traffic Right
 
Serikali hizi mbili zikasign Memorandum of understanding Nov 26 2016 (president Uhuru era) Hatujui kilichotokea katika serikali mpya ya rais Ruto hadi kukataa ombi hili la Tanzania. Hapa ndipo watu wanachanganya mambo

Wanahisi ni kama vile Tanzania inawablackmail wakenya kwa kuzuia ndege zao kwa kuwa tu wakenya wamekataa ombi letu. Si sawa kufikiri hivi.

Ingawa Tanzania imelifanya hili kama OMBI lakini ina HAKI ya kupeleka ndege zake za mizigo nchini Kenya na kubeba mizigo kutoka Kenya kwenda mataifa mengine kisha kurudi Tanzania kupitia mkataba wa Chicago.

Kenya haikuwa na haki ya kukataa ombi letu ambalo ni HAKI Kwa kuwa Kenya imevunja 5th Freedom Traffic Right, si vibaya nasi tukiwavunjia 3rd na 4th Freedom Traffic Rights ambazo inawapa haki Kenya (3rd) Kuruka kutoka kwao kuja Kwetu na (4th) Kuruka kutoka kwetu kwenda kwao Uamuzi wetu umewatega wakenya kuiangalia upya HAKI yetu.
 
wacheza ngumi walioendelea huwa wanafanya ujasusi kwa mpinzani wake,akijua mpinzani wake ni mbovu wa taya,mbavu,tumbo au bega anakomaa kupiga makonde palepale kwenye ubovu mpaka apatoneshe.

Kenya ni mbovu kwenye tumbo akianzisha battle ni kupiga ngumi za kutosha tumboni mpaka atainua mikono mbwa huyu.
 
Ukisoma ile Notice ya TAA utaona wanataka ATCL iondokee Kenya kwenda nchi zingine (third party countries). Nadhani shida iko hapo. Ngoja tuone kama wataelewana ndani ya hizi siku 3.
Kenya washapaniki tyr
 
wacheza ngumi walioendelea huwa wanafanya ujasusi kwa mpinzani wake,akijua mpinzani wake ni mbovu wa taya,mbavu,tumbo au bega anakomaa kupiga makonde palepale kwenye ubovu mpaka apatoneshe.

Kenya ni mbovu kwenye tumbo akianzisha battle ni kupiga ngumi za kutosha tumboni mpaka atainua mikono mbwa huyu.
Kwamba hawajui kuusoma udhaifi wa mpinzani
 
Je kuna ndege ya Kenya inaanzia Safari TZ kwenda nchi nyingine? Yaani kwenda nchi ya tatu?

Nijuavyo mimi inaruhusiwa Kuanzia nchi yako kwenda nchi nyingi na sio Kuanzia nchi isiyo yako kwenda nchi isiyo yako.

Ndege yetu ya mizigo haina mizigo ya kutosha kutoka TZ kwenda nje. Wanataka wa bebe mizigo ya Kenya kwa Mfano kwenda China. Kuna mizigo ya kutosha kutoka China kuja TZ. Hapo ndio mwanzo wa tatizo.
 
Asante mkuu kwa ufafanuzi
Kuna tatizo lipo mahali ngoja tuendelee kufuatilia.
 
Je kuna ndege ya Kenya inaanzia Safari TZ kwenda nchi nyingine? Yaani kwenda nchi ya tatu?

Nijuavyo mimi inaruhusiwa Kuanzia nchi yako kwenda nchi nyingi na sio Kuanzia nchi isiyo yako kwenda nchi isiyo yako.

Ndege yetu ya mizigo haina mizigo ya kutosha kutoka TZ kwenda nje. Wanataka wa bebe mizigo ya Kenya kwa Mfano kwenda China. Kuna mizigo ya kutosha kutoka China kuja TZ. Hapo ndio mwanzo wa tatizo.
Hilo lilishakubaliwa na serikali za kenya zilizopita...na mikataba ilisainiwa ...but serikali ya Ruto imekaza ,...
 
Back
Top Bottom