Tanzania kujipatia faida ya asilimia 60 nayo Uganda ikipata asilimia 40 kutokana na uwekezaji wa mafuta

unamfokea nani sasa mimi magufuri?
Vitu vingine ukiwa na akili huwezi kukubali labda uwe mpumbavu tuu!!! Hivi unakuba tutapata 60% wakati mafuta niya Uganda??? Hivi huwa mnafikiri kwa kutumia kiungo gani??? Hivi kwann watz wajinga hivi??? Yani mafuta ni ya Uganda ila kupitia tuu Tz tupate60%??? Je hiyo 60% ni yann??? Ya nn!??
 
"kubwa" ktk mradi huoo si hizo asilimia 60 kwa 40 ,bali ni ajira zitakazopatikana kwa vijana wenzangu watz watafutaji na wapambanaji wataajiliwa...
Yani mafuta yao halafu wakupe 60% ??? Hivi huwa mnafikiria kwa kutumia kiungo gani cha mwili??? Yan hata mtoto wanga wa std two lazima ahoji !!! Lakini MTU mzima anakubali hili poor you!!!
 
Hio 60% ya Toll Charges...60% ya gharama ya ushafirishaji wa mafuta mafuta sio kununua au kuuza mafuta...hio ya kuuza mafuta ni biashara ingine kati ya Uganda na Total....
Ni km Leo ijegwe Express road kutoka Dar mpaka Moro ambayo kupitisha roli la mafuta unalipia then mapato ya ile toll fees igawane mikoa hio road inapopitia...habari ya mafuta Muuzaji alikuuzia bei gani au unaenda kuyauza bei gani mikoa haihusiki hapo...uhusika wetu ni km wa hio mikoa
 
"kubwa" ktk mradi huoo si hizo asilimia 60 kwa 40 ,bali ni ajira zitakazopatikana kwa vijana wenzangu watz watafutaji na wapambanaji wataajiliwa...
Hivi huyu Jiwe anatuonaje?? Yaani huu uongo wa mchana wa kazi gani?? Yaani mwenzako atumie rasilimali fedha na watu wake kuchimba kisha kutafuta masoko halafu ww bila aibu eti upewe 60%?? Kisa bomba limepitia kwenye nchi yako?? Na hao vijana 90,000 wanafanya kazi gani kulinda au bomba lile linapitia kwenye mabega yao?? Ndege wafananao huruka pamoja(wote madikteta).
 
Hivi huyu Jiwe anatuonaje?? Yaani huu uongo wa mchana wa kazi gani?? Yaani mwenzako atumie rasilimali fedha na watu wake kuchimba kisha kutafuta masoko halafu ww bila aibu eti upewe 60%?? Kisa bomba limepitia kwenye nchi yako?? Na hao vijana 90,000 wanafanya kazi gani kulinda au bomba lile linapitia kwenye mabega yao?? Ndege wafananao huruka pamoja(wote madikteta).

Sent using Jamii Forums mobile app
Kabla ya kutoka povu heb jielimishe kwanza kwa kutafuta information sahihi na km umeshindwa uulize tusaidiane taarifa
 
Hio 60% ya Toll Charges...60% ya gharama ya ushafirishaji wa mafuta mafuta sio kununua au kuuza mafuta...hio ya kuuza mafuta ni biashara ingine kati ya Uganda na Total....
Ni km Leo ijegwe Express road kutoka Dar mpaka Moro ambayo kupitisha roli la mafuta unalipia then mapato ya ile toll fees igawane mikoa hio road inapopitia...habari ya mafuta Muuzaji alikuuzia bei gani au unaenda kuyauza bei gani mikoa haihusiki hapo...uhusika wetu ni km wa hio mikoa
Waeleze hao wajinga na wapumbavu wanokimbilia kujifanya wajuaji hata hawajui kinachoongelewa!
 
Waeleze hao wajinga na wapumbavu wanokimbilia kujifanya wajuaji hata hawajui kinachoongelewa!
wasamee mkuu....hawajui walitendalo.
Tatzo la watanzania wengi ktk mitandao hawataki kujielimisha au kutafta taarifa sahihi...wao wakishaona taarifa wanatirirka nayo iwe sahihi ama isiwe sahihi...na wajanja washazijua tabia zetu mbovu wanatuletea taarifa za kutuchokonoa ilimradi waone how good are we ktk kutoka mapovu...we so negative kiasi kwamba hatuna muda wa ku think positively na kutafuta taarifa sahihi...
 
Gharama za Ushafirishaji wa Mafuta kutoka Uganda mpaka Tanga zinakadiriwa kua $12.25 kwa pipa...ktk hii sisi yetu ni 60% Uganda yao ni 40%....hii ni nje ya Pesa ambayo Total itawalipa Uganda km Mrahaba, Kodi huko Uganda na gharama nyingine km zipo...na ni nje na pesa Ambayo Total itaenda kuyauza huko nje...sisi chetu ni 60% ya gharama za usafirishaji kutoka Uganda kuja Tanga...hayo mengine hayatuhusu
 
Mwenye akili atafakari
IMG_20200913_234811.jpg
View attachment 1569158
 
Makubaliano ya bomba la mafuta: Tanzania kujipatia faida ya asilimia 60 nayo Uganda ikipata asilimia 40

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli na mwenzake wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika picha ya awali

CHANZO CHA PICHA,IKULU YA RAIS TANZANIA
Maelezo ya picha,
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli na mwenzake wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika picha ya awali.​
Viongozi wa Tanzania na Uganda hatimaye wamekubaliana kuhusu ujenzi wa bomba la mafuta linalotarajiwa kujengwa kutoka mji wa Hoima nchini Uganda hadi changalieni mjini TangaTanzania.
Katika makubaliano hayo yaliotiwa saini na mawaziri wa nishati kutoka pande hizo mbili na marais wa mataifa hayo mawili John Pombe Magufuli wa Tanzania na Yoweri Museveni wa Uganda katika eneo la Chato , asilimia 60 ya faida ya mafuta hayo itaenda kwa Tanzania huku asilimia 40 ikienda kwa Uganda.​
Akizungumza katika hafla hiyo , rais wa Uganda Yoweri Museveni alisema kwamba cha muhimu ilikuwa kuanza mradi huo aliodai kucheleweshwa kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.​
''Niliamua kwamba kucheleweshwa kwa mradi huu kwasababu ya zile dola milioni 800 sio jambo la akili kwasababu tunazugumnzia kuzalisha mapipa bilioni 6.5 ikiwa ni asilimia 40 pekee ya mafuta yaliogunduliwa katika eneo la Albert, lakini huenda tukapata mafuta hata zaidi katika eneo hilo'', alisema.​
Rais Museveni akihutubia uma baada ya kutia saini mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanzania
CHANZO CHA PICHA,MAELEZOPHOTO​
Maelezo ya picha,
Rais Museveni akihutubia uma baada ya kutia saini mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanzania​
Kiongozi huyo amesema kwamba uwekezaji wa bomba hilo la mafuta utagharimu dola bilioni 4 za Marekani.​
''Niliamua kwamba wacha tuwache kuchelewesha tuanze mradi. Tuliongea kwa simu mimi na mdogo wangu, nikamwambia achukue hata asilimia 70 au 80 lakini mdogo wangu akaona aibu akasema hapana , ni asilimia 60 itakwenda Tanzania, 40 nayo ikisalia na Uganda.​
Awali akizungumza , rais Magufuli amesema kwamba mradi huo utaimarisha uchumi wa mataifa haya mawili na eneo lote la Afrika mashariki na kati.​
Alisema kwamba mataifa yaliopo katika ushoroba wa kaskazini yatafaidika pakubwa na bomba hilo.​
Uganda kupitishia mafuta yake Tanzania
Maelezo ya picha,
Uganda kupitishia mafuta yake Tanzania​
Rais Magufuli akimpongeza rais Museveni baada ya kutia saini uanzishaji wa ujenzi wa bomba la mafuta Kutoka Uganda hadi Tanzania
Maelezo ya picha,​
Rais Magufuli akimpongeza rais Museveni baada ya kutia saini uanzishaji wa ujenzi wa bomba la mafuta Kutoka Uganda hadi Tanzania​
Amesema kwamba takriban Watanzania kati ya 10,000 na hadi 15,000 watafaidika na ajira za kazi mradi huo utakapokamilika.​
Ameongezea kwamba bomba hilo litakuwa refu zaidi duniani linalotumia teknolojia ya kupasha moto mafuta likiwa na urefu wa kilomita 1445.​
''Litakuwa bomba refu zaidi duniani lenye teknolojia ya sasa ya kusafirisha mafuta yakiwa katika joto'', alisema raia Magufuli​
Kilomita 1115 za bomba hilo zitakuwa upande wa Tanzania huku kilomita 330 zilizosalia zikiwa upande wa Tanzania.​
Rais Magufuli amesema kwamba mradi huo utapitia mikoa minane ikiwemo wilaya 24. Mikoa hiyo ni Kagera, Geita , Shinyanga , Tabora, Singida, Dodoma, Manyara, na Tanga.​
Bomba hilo la mafuta litakwenda kilomita 1,400km kuanzia Hoima, hadi kwenye bandari ya Tanga

Maelezo ya picha,
Bomba hilo la mafuta litakwenda kilomita 1,400km kuanzia Hoima, hadi kwenye bandari ya Tanga​
Magufuli amesema kwamba Watanzania 90,000 watakaoathiriwa mashamba yao watalipwa fidia ya bilioni 21 fedha za Tanzania.​
Ameongezea kwamba Ujenzi wa vituo 14 vya bomba hilo vitawafidia watakaoathiriwa bilioni 9.9 za Tanzania.​
Kalaga baoooooooo mgeni kamwaga mbogaView attachment 1569164
IMG_20200913_234804.jpg
 
Back
Top Bottom