Tanzania kujipatia faida ya asilimia 60 nayo Uganda ikipata asilimia 40 kutokana na uwekezaji wa mafuta

snowden E

JF-Expert Member
Apr 27, 2018
360
500
Makubaliano ya bomba la mafuta: Tanzania kujipatia faida ya asilimia 60 nayo Uganda ikipata asilimia 40

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli na mwenzake wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika picha ya awali

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli na mwenzake wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika picha ya awali​

Viongozi wa Tanzania na Uganda hatimaye wamekubaliana kuhusu ujenzi wa bomba la mafuta linalotarajiwa kujengwa kutoka mji wa Hoima nchini Uganda hadi changalieni mjini TangaTanzania.

Katika makubaliano hayo yaliotiwa saini na mawaziri wa nishati kutoka pande hizo mbili na marais wa mataifa hayo mawili John Pombe Magufuli wa Tanzania na Yoweri Museveni wa Uganda katika eneo la Chato , asilimia 60 ya faida ya mafuta hayo itaenda kwa Tanzania huku asilimia 40 ikienda kwa Uganda.​
Akizungumza katika hafla hiyo , rais wa Uganda Yoweri Museveni alisema kwamba cha muhimu ilikuwa kuanza mradi huo aliodai kucheleweshwa kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.​
''Niliamua kwamba kucheleweshwa kwa mradi huu kwasababu ya zile dola milioni 800 sio jambo la akili kwasababu tunazugumnzia kuzalisha mapipa bilioni 6.5 ikiwa ni asilimia 40 pekee ya mafuta yaliogunduliwa katika eneo la Albert, lakini huenda tukapata mafuta hata zaidi katika eneo hilo'', alisema.​
Rais Museveni akihutubia uma baada ya kutia saini mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanzania

Rais Museveni akihutubia umma baada ya kutia saini mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanzania.​

Kiongozi huyo amesema kwamba uwekezaji wa bomba hilo la mafuta utagharimu dola bilioni 4 za Marekani.​
''Niliamua kwamba wacha tuwache kuchelewesha tuanze mradi. Tuliongea kwa simu mimi na mdogo wangu, nikamwambia achukue hata asilimia 70 au 80 lakini mdogo wangu akaona aibu akasema hapana , ni asilimia 60 itakwenda Tanzania, 40 nayo ikisalia na Uganda.​

Awali akizungumza, Rais Magufuli amesema kwamba mradi huo utaimarisha uchumi wa mataifa haya mawili na eneo lote la Afrika mashariki na kati. Alisema kwamba mataifa yaliopo katika ushoroba wa kaskazini yatafaidika pakubwa na bomba hilo.​

Uganda kupitishia mafuta yake Tanzania

Uganda kupitishia mafuta yake Tanzania

Rais Magufuli akimpongeza rais Museveni baada ya kutia saini uanzishaji wa ujenzi wa bomba la mafuta Kutoka Uganda hadi Tanzania

Rais Magufuli akimpongeza rais Museveni baada ya kutia saini uanzishaji wa ujenzi wa bomba la mafuta Kutoka Uganda hadi Tanzania
Amesema kwamba takriban Watanzania kati ya 10,000 na hadi 15,000 watafaidika na ajira za kazi mradi huo utakapokamilika.​
Ameongezea kwamba bomba hilo litakuwa refu zaidi duniani linalotumia teknolojia ya kupasha moto mafuta likiwa na urefu wa kilomita 1445.​
''Litakuwa bomba refu zaidi duniani lenye teknolojia ya sasa ya kusafirisha mafuta yakiwa katika joto'', alisema raia Magufuli​
Kilomita 1115 za bomba hilo zitakuwa upande wa Tanzania huku kilomita 330 zilizosalia zikiwa upande wa Tanzania.​
Rais Magufuli amesema kwamba mradi huo utapitia mikoa minane ikiwemo wilaya 24. Mikoa hiyo ni Kagera, Geita , Shinyanga , Tabora, Singida, Dodoma, Manyara, na Tanga.​
Bomba hilo la mafuta litakwenda kilomita 1,400km kuanzia Hoima, hadi kwenye bandari ya Tanga


Maelezo ya picha,
Bomba hilo la mafuta litakwenda kilomita 1,400km kuanzia Hoima, hadi kwenye bandari ya Tanga​
Magufuli amesema kwamba Watanzania 90,000 watakaoathiriwa mashamba yao watalipwa fidia ya bilioni 21 fedha za Tanzania.​
Ameongezea kwamba Ujenzi wa vituo 14 vya bomba hilo vitawafidia watakaoathiriwa bilioni 9.9 za Tanzania.​
 

Mokaze

JF-Expert Member
Aug 3, 2018
6,728
2,000
mafuta ya kwao, kupitisha kwako tu wakupe (60) faida kubwa kuliko wao (40)?


Kama hawataki wayasafirishe wao wenyewe tuone kama hata hiyo 40% wataipata, kumbuka Museveni alitaka tuchukue 70% na Magu akaona ni too much ndipo akashuka hadi 60%.


Juu ya yote nguo ya kuazima haisitiri maun; tutafute mafuta yetu wenyewe ili tutumie bomba hilo kabla ya Waganda hawajagoma (kuvunja mkataba) kwani hiyo ya 60% sio waganda wengi wameipokea na kumbuka Museveni days in the office are numbered due to agewise etc.
 

Pulchra Animo

JF-Expert Member
Jun 16, 2016
1,004
2,000
mafuta ya kwao, kupitisha kwako tu wakupe (60) faida kubwa kuliko wao (40)?

Tatizo letu ni tabia ya kufikia conclusion bila ya kuwa na all relevant facts mezani. Unazijua responsibilities (obligations) za kila upande, kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa? Unajua jukumu la protection, upkeep ya miundo mbinu ni la nani? Unajua hiyo inayoitwa “faida” inakokotolewaje?

Yapo majukumu ambayo akibebeshwa anayelipwa 60% anaishia kuambulia pesa ya mboga na sana sana indirect benefit inayotokana na watu wake (host) kunufaika kwa namna moja au nyingine!
 

road master

JF-Expert Member
Jun 11, 2020
563
1,000
wanachadema kila kitu ni kupinga tu poleni sana
Vitu vingine ukiwa na akili huwezi kukubali labda uwe mpumbavu tuu!!! Hivi unakuba tutapata 60% wakati mafuta niya Uganda??? Hivi huwa mnafikiri kwa kutumia kiungo gani??? Hivi kwann watz wajinga hivi??? Yani mafuta ni ya Uganda ila kupitia tuu Tz tupate60%??? Je hiyo 60% ni yann??? Ya nn!??
 

Ti Go

JF-Expert Member
Jun 28, 2012
505
500
wanachadema kila kitu ni kupinga tu poleni sana
Hili jukwa ni la great thinkers na siyo la CCM na CDM. Ukileta hoja isiyo sawa, lazima tusikubaliane na wewe. Nadhani kuna kitu mmlitaka kusema ila mmeshindwa kukielezea. Kama ni faida ya usafirishaji wa mafuta tu, hilo ni swala jingine
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom