Kupitia Bomba la Mafuta Uganda naamini Wazungu hawana Urafiki na Mwafrika Tuamke

themagnificient

JF-Expert Member
Dec 13, 2016
988
3,318
Kama nimekosea mnieleweshe Tafadhali

Niliskia Bomba la mafuta linalotokea Hoima Uganda , yale mafuta yakichimbwa uganda yanasafirishwa hadi Bandari ya Tanga kisha yanapakiwa kwenye meli then yanasafiriswa ulaya kwenda kusafishwa hapo ndio huwa naskia inapatikana petroli,diezel na mafuta mengine

Swala nalojiuliza ni kwa nini Mfaransa hakujenga mitambo ya kuyasafisha yale mafuta pale pale Uganda yaani kama ni Petroli na Diezel zipatikane hapo hapo ili haya mafuta yapatikane hapa hapa kwa bei nafuu?, maana yake mafuta yakichimbwa Uganda yakipelekwa Ufaransa yakirudi Tanzania au Uganda bei ni ile ile

Ndio maana nasema Waafrica tusipoamka kuwa na wataalam wanaoweza kuunda mitambo na kujitegemea wenyewe mzungu ataendelea kufanya hili bara kuwa maskini

Hata Gesi iliyovumbuliwa mtwara hadi leo hii haijawahi saidia lolote kwenye kupungua kwa garama za maisha sana sana mzungu ndio anafaidika

Madini niliskia mzungu anavuna mchanga anasafirisha hadi ulaya kuchuja madini ndio maana Magufuli alikuwa mtata
 
Wamenunua kwaajili ya soko lao la Ulaya sisi ndio wajinga tunauza mafuta ilihali ndio kitu namba moja tunaimport, ila sitaki kuamini kwamba hatamwachia Museveni hata koki moja yakujazia V8 za ikulu, fungu la kila mwezi mpaka kwa wajukuu wake lazima lipo.
 
Ndo ilivyo,we kwanini hujiulizi why watu wanalipia daraja wakati wa kwenda makwao,
 
Kuna watu bado wanaamini mzungu ni rafiki, kwa vile wanaona wazungu ma Padre, au wadada wa kizungu wakitoa misaada ya kulea watoto, wakitoa huduma kwa waathirika wa ukimwi!
Nyuma ya pazia mzungu acheki na kima, ukisikia umoja wa ulaya, ametoa msaada wa kujenga mradi na miundombinu, ujue umeishapigwa Mara 100!
Chukulia kwa mfsno, kinachotokea Niger, viongozi wa kijeshi wamempa saa 48 balozi wa ufaransa,
Aondoke, amegoma,
Wamekata huduma ya maji na umeme, kwenda ubalozini,lakini mfaransa amedinda hataki kutoka,
Jiulize kwa nini, hizi nchi, ufaransa amezifanya kama shamba LA Bibi, amechimba rasilimali kwa muda mrefu, faida yote inaenda Ufaransa, hizi nchi zinazidi kuwa maskini!
 
Niliwahi kuskia mahali kuwa miaka ya nyuma huko wazungu waliwekeana mikataba ya kutoweka MANUFACTURING INDUSTRY YOYOTE HAPA AFRIKA , sasa na hyo mitambo ni sehemu ya manufaturing industry.hata sauz yale magari naskia yanakuwa assembled tu lakin hayawi produced pale completely.anyway ni maneno ya mlevi mwenzangu hapa simwamini sana,acha tuendelee kula chang'aa
 
Tulikuwa na Tipper awamu ya kwanza, tulikuwa tunapokea mafuta ghafi Ila zilipokuja Sera za ubinafsishaji wakaiua.
Ni ujinga wetu wenyewe na sio wazungu kwani Tipper ilikuwa inatoa product mbalimbali.
 
Back
Top Bottom