Tanzania kujipatia faida ya asilimia 60 nayo Uganda ikipata asilimia 40 kutokana na uwekezaji wa mafuta

Nirahisi sana kujua hii, sijui watu wanajitoa akili makusudi ama vipi.

Ni sawa na doctor mwenye preconceived diagnosis; anakuambia mgonjwa fulani ni HIV positive hata kabla hajamuona mgonjwa mwenyewe na kumfanyia vipimo! ...And those are the self-proclaimed great thinkers of this platform. Afadhali idealistic operations zao ziendelee kuwa nyuma ya keyboard, kwa sababu they aren’t positioned to solve any real problem!
 
Hio 60% ya Toll Charges...60% ya gharama ya ushafirishaji wa mafuta mafuta sio kununua au kuuza mafuta...hio ya kuuza mafuta ni biashara ingine kati ya Uganda na Total....
Ni km Leo ijegwe Express road kutoka Dar mpaka Moro ambayo kupitisha roli la mafuta unalipia then mapato ya ile toll fees igawane mikoa hio road inapopitia...habari ya mafuta Muuzaji alikuuzia bei gani au unaenda kuyauza bei gani mikoa haihusiki hapo...uhusika wetu ni km wa hio mikoa
Ulistahili uwepo shuleni ukifundisha,tena hizi ghali za st!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
umeamua kuwazushia wakubwa hawa, una makusudi yako naona, hawawezi kusema uwongo wa namna hiyo. yaani uganda mafuta ni yake halafu ampe tanzania faida kubwa inawezekana hukuelewa labda unaoengelea gharama na mapato ya usafirishaji, kwenye urefu bora hata usingeandika yapo yana km zaidi ya elf4 we unatuletea km1145 ndio liwe refu zaidi duniani!!!! kama ni kampeini umeharibu
 
Tatizo letu ni tabia ya kufikia conclusion bila ya kuwa na all relevant facts mezani. Unazijua responsibilities (obligations) za kila upande, kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa? Unajua jukumu la protection, upkeep ya miundo mbinu ni la nani? Unajua hiyo inayoitwa “faida” inakokotolewaje?

Yapo majukumu ambayo akibebeshwa anayelipwa 60% anaishia kuambulia pesa ya mboga na sana sana indirect benefit inayotokana na watu wake (host) kunufaika kwa namna moja au nyingine!
yes mleta uzi angefafanua na hayo tungemwelewa lakini kwa jinsi alivyotupia lazima aulizwe maswali mengi au akejeliwe
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom