Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,996
Nchi ya Rwanda imekuwa ikidaiwa kuhusika sana na machafuko ya DRC na kuwa vyanzo mbalimbali (hasa vya Umoja wa Mataifa na nchi za Magharibi) vinaonesha kuwa Rwanda ndio inaunga mkono na kusapoti kundi la waasi la M23. Je, Tanzania ina msimamo gani kuhusu Rwanda na kuhusija kwake na mgogoro wa Congo? Je wakati umefika kwa Tanzania kuchukua msimamo mkali ikiwemo kuzuia Rwanda kutumia bandari zetu kupitisha silaha ambazo nyingine zinaishia mikononi mwa waasi?