M23 yaua wanajeshi 3 wa Tanzania huko Goma DRC

kibarango

Senior Member
Sep 6, 2014
146
308
Majina hayajatajwa.

Ikumbukwe jana Rais wa Rwanda Bw Kagame amekiri kuwa anawaunga mkono waasi wa M23 kwa kusema haoni sababu ya kuwapinga waasi hao.

Hivyo kwa tafasiri ni kuwa Wanajeshi wa Rwanda wamewauwa wanajeshi wa Tanzania huko DRC.

=====

Wanajeshi watatu wa Tanzania wameuawa kwenye shambulio la kombora lililotokea katika Mji wa Kivu ulio Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Jumuiya ya Ushirikiano ya SADC imethibitisha habari hizo kupitia tovuti yake.

Taarifa ya SADC iliyowekwa kwenye akaunti yake ya mtandao wa X (zamani Twitter) ,ilisema katika shambulio hilo la kombora, wanajeshi wengine watatu wa Tanzania walijeruhiwa.

Askari wa Tanzania ni sehemu ya Kikosi cha SADC kilichopelekwa Mashariki mwa DRC kwaajili ya kulinda amani ikijumuisha pia nchi za Malawi na Afrika Kusini.

548030615.jpg
 
"Hivyo kwa tafasiri ni kuwa Wanajeshi wa Rwanda wamewauwa wanajeshi wa Tanzania huko DRC"

Watanzania sio mbumbumbu kama inavyofikiriwa

Tafsiri yake, haina maana kuna Ukweli wowote ule na Tafasiri.

Badala ya kuchochea uhasama, kwanini tusichochee Urafiki?

Yaani hizi nyuzi za Uchonganishi mwisho wake utakuwa ni Vita-sasa utakuwa umefanya nini-Kuongeza Watanzania wengine wafe tu, to what end?
 
Halafu huwezi tumia lugha eti M23 wawaua wanajeshi 3 wa Tanzania,huko kuna jeshi la Tanzania +la South Afrika na wamekwenda kwa mwambuli wa SADC ingekuwa vyema kutumia neno kuwa Wanajeshi 3 wa kikosi cha Tanzania kinachowakilisha SADC kilichopo DRC wauwaawa
 
"Hivyo kwa tafasiri ni kuwa Wanajeshi wa Rwanda wamewauwa wanajeshi wa Tanzania huko DRC"

Watanzania sio mbumbumbu kama inavyofikiriwa

Tafsiri yake, haina maana kuna Ukweli wowote ule na Tafasiri.

Badala ya kuchochea uhasama, kwanini tusichochee Urafiki?

Yaani hizi nyuzi za Uchonganishi mwisho wake utakuwa ni Vita-sasa utakuwa umefanya nini-Kuongeza Watanzania wengine wafe tu, to what end?
kwa maoni yako sema tu kikosi cha tanzania kiondoke huko, Congo ijipambanie yenyewe na bila shaka itashindwa na waasi hao watayatwaa maeneo ya mashariki mwa congo na kuunda himaya yao
 
Hutaki hiyo tafasiri. Jana PK kaulizwa kama anaunga mkono M23 akajibu haoni sababu ya kutowaunga mkono. Thats means anawaunga mkono.

Hivyo tafasiri ni kutokana na maneno ya PK.

Kama M23 ni nduguzo waambie waache kuuwa raia wa DRC. Africa tumechoka vita za Watutsi.

Tangu na tangu kila vita lazima mshiriki mnauwa maras na marais. Zama na zama

Sent from my A002SH using JamiiForums mobile app
 
kwa maoni yako sema tu kikosi cha tanzania kiondoke huko, Congo ijipambanie yenyewe na bila shaka itashindwa na waasi hao watayatwaa maeneo ya mashariki mwa congo na kuunda himaya yao
Na baada ya hapo wataungana na kuoata nguvu zaidi. Watataka Kigoma, Geita, Kagera na Tabora.

Mwezi mmoja uliopita Waziri Biruta wa Rwanda alisema hata Waha wa Tz ni Wanywarwanda

Sent from my A002SH using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom