Tanzania isitishe uhusiano na Rwanda juu ya DRC?

Tanzania isitishe uhusiano na Rwanda juu ya DRC?

Nchi ya Rwanda imekuwa ikidaiwa kuhusika sana na machafuko ya DRC na kuwa vyanzo mbalimbali (hasa vya Umoja wa Mataifa na nchi za Magharibi) vinaonesha kuwa Rwanda ndio inaunga mkono na kusapoti kundi la waasi la M23. Je, Tanzania ina msimamo gani kuhusu Rwanda na kuhusija kwake na mgogoro wa Congo? Je wakati umefika kwa Tanzania kuchukua msimamo mkali ikiwemo kuzuia Rwanda kutumia bandari zetu kupitisha silaha ambazo nyingine zinaishia mikononi mwa waasi?

Mimi sioni mantiki ya Kusitisha uhusiano..Ni Suala la kutafuta usuluhishi kupitia EAC..hii habari ya kutoa tamko(kwa nchi kama Tanzania haisaidii.

Aidha mgogoro wa Wa Kongo ni zaidi ya tunavyouangalia.Ikumbukwe kuwa Baada ya kuanguka kwa Habyarimana na kagame kuchukua hatamu ya Uongozi kundi lililokuwa likimuunga mkono Habyarimana(ambalo hadi leo linaipinga serikali ya Kagame),yaani FDL linahusika..Lakini pia Kagame amekuwa anahusishwa na kuliunga mkono kundi la M23(ambalo asili yake ni wakongo ambao wana asili ya Rwanda(ambao serikali ya kongo haitaki kuwatambua kama wakongo halali).Kwa hiyo inasemekana Kagame anatumia M23 kujikinga na FDL..kundi linalosemekana kuwa lingeshamuondoa bila msaada wa M23..Kwa hiyo pamoja na interest za Kiuchumi(Ikumbukwe Goma ni mji wa Madini na processing industries za madini allover the country zipo goma..kwa asilimia kubwa)Kagame anatafuta political security kuhakikisha FDL hawakanyagi katika nchi yake,bali wanakuwa mbali kabisa kwa msaada wa M23..Kwa hiyo si suala la kukurupuka bali Tanzania ijihusishe kwa tahadhari kubwa kabisa
 
Tanzania ichukue msimamo kwa kuangalia maslahi ya watanzania kwanza.Imepitwa kipindi kile kwamba tupo tayari kulala na njaa lakini tuseme au tumtetee fulani. Tuweke mbele kwanza harakati za kupambana na umaskini wa wananchi wetu kwanza.Congo nao washughulike kwanza na mambo yao. Ndio tunaogelea kuvuka mto sasa hatuwezi kumbeba mtu mwingine mgongoni tutazama wote. Wasubiri tuvuke tutarudi kuwavusha na wao. Watanzania kwanza wengine baadaye.Dunia ya sifa za kijinga ilishapitwa na tulipoteza sana muda. Tushughulikie matatizo ya wtz
 
Ni wakati muafaka kwa Tanzania kukemea Kagame na Museveni kuwaonea Congo. Ubabe wao haufai.
 
Ile ripoti ya siri ya UN iliyozungumzia involvement ya baadhi ya watanzania kwenye vita huko DRC
 
Suala la migogoro ya DRC na vikundi mbalimbali vya waasi haliihusu TZ, kuna masuala mengi yanayosababisha migogoro hiyo yakiwemo ya utawala bora, uchumi, masuala ya kijamii n.k mogogoro hii ni masuala ya ndani ya nchi hiyo. Hata huko kuhusishwa kwa Rwanda na Uganda ni tuhuma tu ukweli wanaujua wenyewe. Si busara kwa TZ kukurupuka na kuanza kusema kuweka vikwazo kwa ama Rwanda au Uganda ama DRC hawa wote ni jirani zetu na tuna uhusiano mzuri nao. Kama DRC anamchokoza Rwanda au Uganda kwa kisingizio cha waasi sisi tukae mbali ili kuepusha shari. Kwamba silaha zinawafikiaje waasi wa DRC, vongozi wa DRC wanalijua hili na kuna wanaonufaika na migogoro hii. DRC imetengana vipande vipande na viongozi wake wametengana kila mmoja la lake. kwa hali hii migogoro haitoisha na utatuzi wake si kwa kupeleka majeshi bali ni mazungumzo ya kuwaunganisha wananchi wake wawe kitu kimoja, halikadhalika viongozi wawe wanazungumza kitu kimoja, hatua ambayo itachukua muda, vinginevyo suluhisho kama la kuigawa Sudan kuwa na Sudani mbili linaweza kuwa la manufaa.
Wakatabahu.
 
Wakongo waache kuendekeza starehe tu. Mimi ningekua mtawala wa Tz muda huu majeshi yetu yapo DRC wakipora madini na maliasili nyingine kama majirani zetu wanavyofanya!
 
Jana kwenye tweet ya Mhe ZZK aliulizwa na mmoja wa followers wake hawa wacongo wanataka nini? akajibu "peace, stability and dignity" Mimi nasema hiviiiiii nchi ambazo hazina madini zinaweza kupata hivyo vitu lakini nchi kama drc na nyonginezo zenye neema ya vito hawatapata "peace, stability and dignity"

Huu ndiwo ukweli, kwani kinachoisumbua Congo ni rasilimali zake ikiwemo cobalt ambayo ni bidhaa muhimu kwa Marekani. Hebu tuzidi kujiuliza, ikiwa risasi moja tu huwezi kuvuka nayo mpaka, je silaha kali za wanaoitwa waasi zinapitia wapi? Je zinatengenezwa Congo?
 
Huu ndiwo ukweli, kwani kinachoisumbua Congo ni rasilimali zake ikiwemo cobalt ambayo ni bidhaa muhimu kwa Marekani. Hebu tuzidi kujiuliza, ikiwa risasi moja tu huwezi kuvuka nayo mpaka, je silaha kali za wanaoitwa waasi zinapitia wapi? Je zinatengenezwa Congo?

kaka umenikumbusha concept moja hivi ya "the paradox of plenty"...tatizo hapa ni kuwa tuna visible na invisible of actors,thus in solving this issue we must consider the needs and interests of both parties.
 
Mwanakijiji,
Kwa muda mrefu sasa Kagame amekuwa na sera ya kutaka kuitawala kanda yote ya maziwa makuu. Na nadhani mwanzoni ndio iliyokuwa vision yake yeye na Museveni (Sidhani kama amebadilisha vision hii). Ni dhahiri kuwa kagame alitofautiana sana na Mkapa juu ya hili (personality clash)hasa kwa kuwa kila mmoja alikuwa hapendi tabia za mwenzie.

Pili, Kagame na Museveni wamekuwa na sera ya kuukuza utusi - kwa kisingizio cha kuwalinda watusi wasiuwawe.Hii imewapa moral right ya kutumia silaha,kukuza/kujenga majeshi ya uasi Kongo,Uganda,Burundi.

Tatu,Kagame anajua kuwa ni smart na anapenda ajulikane kuwa yeye ni smart hasa katika masuala ya kijeshi, kivita na kimikakati jambo ambalo limewafanya marais/ viongozi wengi wamwogope, hasa kwa sababu za kuto-kujiamini kwao.

Nne, ni katika sifa hizi chache (na nyingine kubwa zaidi) ambazo kagame amekuwa ni kijogoo wa ukanda huu wa maziwa makuu na hakuna kiongozi aliye madarakani kwa sasa anaeweza kumnyoshea kidole.

Tano, Kagame ana sera ya kuwa haongei na vijana wadogo (Kikwete,Kibaki,Museveni nk) bali yeye yuko kwenye club ya juu zaidi ya kina Bush/Blair

NB:Aliwahi kumwambia Mkapa "The whole of East Africa inahitaji Rais mmoja tu MWENYE AKILI. Mkapa alikasirika sanaaaaaaa! This guy is arrogant(or too confident/ with very high opinion over himself) He is a bully,murderer,war criminal etc. Ukimuuliza Kikwete atakuambia ngoja tuongee na Blair. Kaazi kwelikweli
* T dont believe Tanzania ina kiongozi mwenye kuweza kuona sababu ya Kuuangalia Upya uhusiano wetu na Rwanda.

Usimkuze sana Kagame wakati FLDR bado wanampa shida! Vita ya kwanza ya Congo waliweza kwenda mpaka Kinshasa na kuchukua nchi lakini FLDR (wakati huo ALiR) walibaki Kivu. Vita ya pili ya Congo, the same mpaka ikabidi Kabila senior kuwaomba FLDR (wakati huo ALiR) kumsaidia.
 
Matatizo ya ndani yanailemea Tz , Tuombe wapinzani wa watawala wasipate msaada wa Rwanda

Wakipata msaada warwanda watafanya nini? ndiyo wataitoa serikali ya Tanzania? hee basi wananguvu nyingi so wao ni super power wa east africa? Hatuhitaji watu wa nje watuingile mambo yetu na wakijaribu utakuwa ndiyo mwisho wao!
 
Huu ndiwo ukweli, kwani kinachoisumbua Congo ni rasilimali zake ikiwemo cobalt ambayo ni bidhaa muhimu kwa Marekani. Hebu tuzidi kujiuliza, ikiwa risasi moja tu huwezi kuvuka nayo mpaka, je silaha kali za wanaoitwa waasi zinapitia wapi? Je zinatengenezwa Congo?
Mimi bado nalia na UN.Imekuwa kama ni matusi kuwataja UN kwa uovu lakini hawa ni wahusika wa mwanzo wa migogoro.Hivyo tukiwanyamazia watatumaliza.
Tangu lini baba ndani ya nyumba kumtaja mwanawe mmoja kuwa ni mbaya.Si ni kama kumchongea kwa nduguze.Ikiwa imeona Rwanda inahusika mbona hawajaitisha kikao UN kuilaani na kuiwekea vikwazo.Badala yake hao waasi inaosema wamefadhiliwa na Rwanda walipoingia Goma mbona wamewapisha njia huku wanajidai kulalama.
Tayari kuna kauli eti "nchi za Afrika Mashariki zatoa onyo kwa waasi wa DRC".Hatutaki kupiganishwa kwa faida zenu.Vita vyenu viishie huko huko West Africa,Middle East na Asia.
Kama waasi wamepata nguvu ya kuipiga Kongo na watu wa Goma wameshangilia kuingia kwao basi sisi haituhusu.Ikibidi tunaweza kusuluhisha tu lakini sio kupigana kuunga mkono upande wowote.
 
Tanzania iwasaidie Wanyarwanda, kurudisha eneo lao kwani wanaolalamika hawajui kwamba wakazi wa Goma ni wanyamrenge ambao ni wanyarwanda.
 
Pasi na shaka Tanzania inanufaika na vigogo wananufaika moja kwa moja, kwanza vigogo wanamiliki kampuni za uchukuzi na ndio wanaoneemeka moja kwa moja na biashara ya kupeleka mizigo Congo na abiria. Vigogo wanamikono yao katika container terminals , clearing and forwarding companies, wanaagiza bidhaaa kutoka nje, Kwa mfano hata watoto wao wanatajwa wamo HSC na hawalipi kodi, Vigogo wanamiliki makampuni ya mafuta na majina yao yanatajwa kila kukicha na ndio wasambazaji na wauzaji wa mafuta huko.

Binafsi nilienda KIVU na kitendo cha kutokea Tanzania tu wananchi walifunguka na kusema vita yao waTz tuna mikono yetu huko na hata wanajeshi wanakwenda. Nkunda alikuwa ana recruit vijana kutoka bongo kwa mshahara wa USD 600 kwa mwezi na vijana wenu wako huko wanapiga kazi.

Vigogo wanahusika pia kutokana na mahusiano yao na Joseph Kabila wangependa kumuona akiendelea kuwepo, Congo ni OILCOM, Lake Oil na Signon kwa uchache tu makampuni ambayo wakubwa wa TZ wametia mikono yao humo. Baada ya kupiga kelele kuhusu ufisadi bongo, Mafisadi wamepeleka biashara zao Congo, Rwanda na Burundi.

Je inawezekana Tanzania (vigogo wa Tanzania) wananufaika na mapigano yanayoendelea huko DRC?
 
Ukisikia Lorry la Maige linaingiza 20,000 USD per month ujue mpango mzima Lubumbashi sio kubeba viazi vya makambako kuleta Tandale. Hawalipi kodi bongo na Congo ndio kabisa wababe wa serikali na jeshi ndio wenyemamlaka.
 
Wakongo waache kuendekeza starehe tu. Mimi ningekua mtawala wa Tz muda huu majeshi yetu yapo DRC wakipora madini na maliasili nyingine kama majirani zetu wanavyofanya!

daaaah aisee mkuu we n kichwa sana!big up
 
"the paradox of plenty"...
Yeah, you are right,.....caused by (with other things) predatory actors who controlling country's resources. The same concept also affects Tanzania's development way.

Na hii dhana iko sahihi sana, ukichunguza nchi nyingi zilizopata maendeleo ya haraka (catch up development) kama zile za East Asia. Kwa vile hazikuwa eyed na hawa predators kutokana na kutokuwa na rasilimali, na badala yake predators walijikita zaidi Afrika, imepelekea hawa jamaa kuambaa kivyao, hata wazungu walipokuja kushtuka wameona jamaa hawapo tena.
Je ni vipi tunaweza kupambana na hali hii? Kimsingi kama least developed nations hatuwezi kuzuia hawa predators kumiliki rasilimali zetu, badala yake lets trade resource for education. Kwa kuwa hizi rasilimali ni non-renewable, hivyo siku moja zitakwisha tu. Lakini iwapo serikali za ki-afrika zitaingia mikataba ya kusomeshewa wananchi wake katika reputable universities kwa idadi kubwa, mwisho wa siku hatutakuwa na rasilimali lakini tutakuwa na elimu nzuri so itakuwa rahisi kubadilisha na ku-utilize mazingira tuliyonayo kuweza ku-survive. Lakini kinyume chake, in few years to come hatutakuwa na rasilimali wala elimu na hii ndo itakuwa zaidi ya Qiyama chetu hapa duniyani. Hivi nyie watu mlioko serikalini ndo hamuoni haya au mnajifanya mabadiliko ya kiduniya nyie hayawahusu.
Hivi ikitokea Nchi kubwa zinazo-compete na rasilimali zetu like US, Canada, Australia, UK, French, Russia, China, Japan, German, Korea, South Africa nk tukimbana kila mmoja tumpe watoto wetu 1000, kwa madini na gesi wanazokwiba, in 20 years tunaweza kuwa na specialist wangapi? We can live without resources but we cant survive without education.
 
Back
Top Bottom