Uchambuzi: Mambo ya msingi kabisa ya kuyatambua kuhusu mgogoro wa wapiganaji wa M23 na Congo DRC na mapendekezo ya nini kifanyike

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,400
Mengi bado yasemwa kuhusu mgogoro unoendelea huko Congo DRC na kwamba hawa wapiganaji wa M23 wafyekwe au wapotezwe mazima jambo ambao si rahisi kama wengi wanavyodhani.

Serikali za Afrika hususan eneo la maziwa makuu zimefikia uamuzi wa kutuma majeshi yao Tanzania ikiwemo pamoja na Afrika Kusini. Serikali ya Rwanda imetuhumiwa kuwasaidia wapiganaji hawa wa M23 na Uganda pia kwa asilimia fulani. Hapa ni lazima ieleweke kwamba ushiriki wa majeshi ya Tanzania katika mgogoro huu ni katika kuhakikisha usalama wa eneo lote la Goma ya kusini ambao lipo karibu kabisa na mpaka na Tanzania na pia kuhakikisha usalama wa eneo lote la mashariki ya Congo DRC.

Afrika Kusini nayo imejiingiza katika mgogo huu kutokana na uwezo wake wa kijeshi ambao umewazidi nchi za Tanzania na pia katika kutaka kuonyesha kuwa nchi hiyo nayo sasa ni mwamba katika medani za kivita baranio Afrika.

Lakini mgogoro huu kati ya wapiganaji hawa wa M23 na serikali ya Congo DRC waweza kutatuliwa endapo Serikali ya Congo DRC itaamua kumeza risasi na kuwaachia M23 wawe na Kivu yao ambayo ndo sehemu ya walipozaliwa baba zao na mama zao.

Ntachambua namna mgogoro huu ulivyoanza na jinsi unavyokwenda na kuona kama kuna dalili za kuwepo maridhiano yoyote kati ya pande hizi mbili.

M23 kilianzishwa rasmi miaka 10 ilopita.

Baada ya kuanzishwa tu wakateka mji wa Goma ulioko mashariki ya Congo DRC karibu na Tanzania.

Goma ni mji wenye watu wapatao milioni 2 ambao sasa hivi wapo kwenye dhahama ya kuukimbia mji huo kutokana na madhila ya mapigano kayti ya M23 na Majeshi ya Congo DRC, Tanzania na Afrika Kusini.

Lakini tukirudi nyuma kulikuwepo na usitishaji wa mapigano kati ya mwaka 2017 na 2020, lakini mwaka 2021 mapigano yakazuka upya.

Wapiganaji wa sasa wa M23 ni watoto wa "Original M23" waliliunda hili kundi mwaka 2012. Wale wapiganaji wa awali ndo walipigana sana na majeshi ya Congo DRC wakati huo wapiganaji hawa wakiitwa CNDP kwa kirefu National Congress for the Defence of People.

M23 madai yao ni kwamba wabaguliwa na Wakongo na wao ni kizazi cha watutsi walozaliwa Kivu pamoja na makabila mengine madogo walozaliwa sehemu hiyo. Hawa ni kizazi cha Rwanda na wajulikana wazi kwa jina la Rwandophones yaani wazungumza kinyarwanda.

Mwaka 2012 M23 waliuteka mazima mji wa Goma na baada ya mazungumzo ya hapa na pale bado kundi hili liliendelea kudai haki yake ya kutambuliwa rasmi na baadae kundi hili likaanza kupata msaada kutoka Rwanda. Hata umoja wa SADC nao ulifanikisha kufanya mazungumzo ambapo kundi hili lilisitisha mapigano rasmi mwaka 2013.

Lakini baadae kundi la M23 likasambaratika na wapiganaji wapatao 1700 wakakimbilia Uganda na wengine wapatao 700 hivi wakakimbilia Rwanda. Hapo waweza kuunganisha "Dots" kwamba kundi jipya la M23 limetokea wapi likiwa na silaha kali na za kisasa zikiwemo la SAM.

Mapema mwaka 2017 kukaanza "Movement" ya wapiganaji kutoka Uganda ambao walianza kuingia nchini Congo DRC na kuanza kupigana na majeshi ya Congo DRC. Mwaka 2021 mapigano mapya yakazuka na kuanza kuenea sehemu mbalimbali za Kivu. Mwaka 2022 vita ikakolea huku M23 ikiwa imara na yenye uwezo wa kuyachachafya majeshi ya Congo DRC.

Uwezo huo wa M23 ndo uloanza kutia shaka kwamba Rwanda yahusika kwa kutoa msaada wa mafunzo, vifaa na mbinu za kijeshi kwa kundi hilo. (Pia Uganda kwa kiasi fulani nayo imetuhumiwa kuhusika na kundi hili (rejea vile vikosi 1700 na 700).

Kwanini M23 wapigania sana Kivu?

Kama nilivyoeleza hapo juu wapiganaji wengi wa M23 watokea sehemu ya kaskazini mwa jimbo la Kivu hususan sehemu za Rutshuru na Masisi ambazo zipo karibu kabisa na mipaka na Rwanda hivyo kuwafanya wapiganaji hawa kuwa na uzoefu mkubwa wa miteremko na maporomoko ya milima ambapo wakiwa juu milimani wapiganaji hawa waweza kuiona Goma.

Rutshuru yenyewe yapakana na Rwanda, Congo DRC na pia Uganda ambapo sehemu hii ina biashara kubwa ambayo yahusisha malori ya mizigo yatokayo Mombasa nchini Kenya na yanokwenda Congo DRC sehemu za Goma na Bukavu kupitia Uganda. Pia sehemu hii ina madini na rasilimali zingine hivyo kuwapa uwezo kundi hili la M23 kukusanya ushuru unotokana na kodi kwa magari yanopita sehemu ya mpaka wa Bunagana.

Sehemu nyingi zenye migogoro kati ya vikundi vya waasi au magaidi kitu cha kwanza kabisa ni kushikilia vyanzo vya mapato. Hata makundi ya ISIS, Al Shabab, Hamas na makundi yanopigana huko Colombia na Uturuki na Yemen ni lazima yawe na vyanzo vya uhakika vya mapato ambapo ushuru wa barabara ni namba moja. Ingawa nisingependa kuliita kundi la M23 kundi la magaidi lakini nalo ni kundi ambalo latumia mbinu zilezile.

Nguvu ya M23 kupigana na kuyazidi nguvu majeshi ya Congo DRC yatokana na nini?

Uwezo mkubwa wa kupigana uliionyeshwa na kundi hili umetia shaka kuwa ni lazima wapewa au wapata msaada kutoka Rwanda au Uganda. Kumekuwepo matumizi ya silaha kali kama vile SAM (Surface to Air Missiles) ambapo kumekuwepo na taarifa za kudunguliwa kwa helikopta kadhaa za jeshi la Congo DRC.

Pia M23 wameonekana na uwezo wa kuhimili mapigano kwa masaa mengi jambo linoashiria kuwa kundi hili wana vifaa vya kisasa kabisa kama vile vyenye kusaidia kuona nyakati za usiku (night vision cameras) na vifaa vingine vya kisasa kama makombora, mizinga na silaha za SMG za kisasa. Ni dhahiri kuwa kama vifaa hivi vimefika mikononi mwa M23 basi kuna msaada mkubwa wa ugavi wa silaha hivi na ndo maana jeshi la Rwanda lahusishwa na kundi hili.

Pia licha ya kupigana kwa kutumia silaha za kisasa, kundi hili la M23 laonekana kupigana vita ya kitaalam yaani ya hatua kwa hatua (Conventional warfare) kuharibu mifumo na silaha za adui kwa kudungua silaha na vifaa vya adui jambo linoashiria kwamba kundi hili lina msaada mkubwa wa kilaama.

Kwa kudhihirisha hilo, leo hii M23 wamefika karibu kabisa na mji wa Goma na mida hii wazuia mizigo na chakula kupitishwa katika barabara kuu za kuelekea kwenye mji huo na pia wameingia katika mji wa Sake uliopo kilomita zipatazo 25 kaskazini magharibi mwa Goma.

Kwa vipi mgogoro huu utapa suluhisho?

Kwanza kabisa tuangalie jeshi la Congo DRC na uwezo wake. Jeshi hili ni la hovyo, lilokosa mpangilio wa kijeshi, lenye uhaba wa silaha na vifaa vya kisasa. Mgao au malipo ya wanajeshi mara nyingi huishia kwa majenerali ambapo huneemeka na misaada ya kijeshi kutoka nje na nchi jirani za Tanzania na Burundi. Pia majenerali hao na viongozi wengine wa kijeshi hutumia muda mwingi kwenda migodini kutafuta dhahabu au madini kwa ajili ya kuuza ili kupata fedha za mabilioni.

Ndo maana leo hii Afrika Kusini wameamua kutuma vikosi vipatavyo 2900 kwenda kusaidia kampeni ya kudhibiti kundi hili la M23.

Mgogoro huu waweza kuisha kwa kurudia makubaliano yalofikiwa miaka 10 ilopita ambapo ilikubaliwa kuwa wapiganaji wa M23 waingizwe kwenye jeshi la Congo DRC jambo ambalo halikutekelezwa. Pia mfumo wa kisiasa wa M23 ulipaswa kutambuliwa na kinyume chake jambo hilo likapuuzwa hadi leo. Endapo M23 wangekuwa wakishiriki harakati za kisiasa huenda leo hii nao wangekuwa na uwakilishi bungeni.

Jambo jingine ambalo wanasiasa wa Congo DRC wataka kulisahau ni ushiriki wa Rwanda katika vita ya kumwondoa aliekuwa raisi wa wakati ule ikiitwa Zaire Mabutu Sese Seko mwaka 1996 ambapo Laurent Kabila alikuja kuwa raisi wa Congo DRC. Hivyo Congo DRC kutokea raisi Joseph Kabila na sasa Felix Tsishekedi wamekuwa wakikwepa kuwa karibu na Rwanda ambayo nayo kwa sababu za kiusalama na kisiasa imewalazimu kuwa macho na Congo DRC.

Rwanda imebakia haina jinsi bali kuachana na kutoa msaada kwa kundi la M23 jambo ambalo ni gumu kwa kuzingatia kuwa Congo DRC wana ushirikiano wa kijeshi na Uganda na pia majeshi yake yamekuwa yakiingia Burundi ambako pia kuna makundi ya waasi ambao pia yahisiwa kuwa yana msaada mkubwa kutoka vikosi vya kijasusi vya Rwanda. Pia Kwa Rwanda kuwaondoa M23 katika maeneo wanoyashikilia ya Kivu na Goma jambo ambalo ni gumu kutokea kutokana na rasilimali kubwa zilizopo katika eneo hilo.

Huko nyuma mwaka 2009 iliwahi kutokea ambapo Rwanda na CNDP walikubaliana na serikali ya Congo DRC kuachana na Goma na Kivu jambo ambalo M23 walilikubali kwa shingo upande kwani liliwaathiri wao zaidi kiuchumi kuliko Congo DRC. Rwanda yataka kuwepo na guarantee kutoka jumuiya ya Afrika Mashariki kwamba vikosi vya kuleta amani vya nchi za maziwa makuu havitaleta athari yoyote ya kiusalama katika eneo la kaskazini mwa mji wa Kivu jambo litopelekea Rwanda kuhisi haiko salama.

Jambo la mwisho ni kwa serikali za Tanzania, Congo DRC, Kenya, Uganda, Burundi na Sudan ya kusini ambazo zaunda Umoja wa Afrika Mashariki kuitisha mkutano na Rwanda ambao utafikia azimio la kuitaka Rwanda kuacha kutoa msaada kwa M23 na pia kuuwa tayati kutuma majeshi yake kwenda Kivu na Goma kusaidia kudhibiti kikundi cha M23 ambacho chaundwa na Wakongo wenye asili ya Rwanda.

Bila hivyo, mgogoro huu utaendelea kuitafuna Congo DRC na kueneza makundi mengi zaidi ya waasi ambayo yatatokana na migogoro mingine iliyopo barani Afrika kama Sudan. Jambo lillo wazi ni kwa serikali ya Congo Kuketi kikao na waasi wa M23 na kuangalia upya makubaliano ya mwaka 2010.

Uchambuzi huu pia umetumia vyanzo mbalimbali kama AP, na Reuters.
 
Mengi bado yasemwa kuhusu mgogoro unoendelea huko Congo DRC na kwamba hawa wapiganaji wa M23 wafyekwe au wapotezwe mazima jambo ambao si rahisi kama wengi wanavyodhani.

Serikali za Afrika hususan eneo la maziwa makuu zimefikia uamuzi wa kutuma majeshi yao Tanzania ikiwemo pamoja na Afrika Kusini. Serikali ya Rwanda imetuhumiwa kuwasaidia wapiganaji hawa wa M23 na Uganda pia kwa asilimia fulani. Hapa ni lazima ieleweke kwamba ushiriki wa majeshi ya Tanzania katika mgogoro huu ni katika kuhakikisha usalama wa eneo lote la Goma ya kusini ambao lipo karibu kabisa na mpaka na Tanzania na pia kuhakikisha usalama wa eneo lote la mashariki ya Congo DRC.

Afrika Kusini nayo imejiingiza katika mgogo huu kutokana na uwezo wake wa kijeshi ambao umewazidi nchi za Tanzania na pia katika kutaka kuonyesha kuwa nchi hiyo nayo sasa ni mwamba katika medani za kivita baranio Afrika.

Lakini mgogoro huu kati ya wapiganaji hawa wa M23 na serikali ya Congo DRC waweza kutatuliwa endapo Serikali ya Congo DRC itaamua kumeza risasi na kuwaachia M23 wawe na Kivu yao ambayo ndo sehemu ya walipozaliwa baba zao na mama zao.

Ntachambua namna mgogoro huu ulivyoanza na jinsi unavyokwenda na kuona kama kuna dalili za kuwepo maridhiano yoyote kati ya pande hizi mbili.

M23 kilianzishwa rasmi miaka 10 ilopita.

Baada ya kuanzishwa tu wakateka mji wa Goma ulioko mashariki ya Congo DRC karibu na Tanzania.

Goma ni mji wenye watu wapatao milioni 2 ambao sasa hivi wapo kwenye dhahama ya kuukimbia mji huo kutokana na madhila ya mapigano kayti ya M23 na Majeshi ya Congo DRC, Tanzania na Afrika Kusini.

Lakini tukirudi nyuma kulikuwepo na usitishaji wa mapigano kati ya mwaka 2017 na 2020, lakini mwaka 2021 mapigano yakazuka upya.

Wapiganaji wa sasa wa M23 ni watoto wa "Original M23" waliliunda hili kundi mwaka 2012. Wale wapiganaji wa awali ndo walipigana sana na majeshi ya Congo DRC wakati huo wapiganaji hawa wakiitwa CNDP kwa kirefu National Congress for the Defence of People.

M23 madai yao ni kwamba wabaguliwa na Wakongo na wao ni kizazi cha watutsi walozaliwa Kivu pamoja na makabila mengine madogo walozaliwa sehemu hiyo. Hawa ni kizazi cha Rwanda na wajulikana wazi kwa jina la Rwandophones yaani wazungumza kinyarwanda.

Mwaka 2012 M23 waliuteka mazima mji wa Goma na baada ya mazungumzo ya hapa na pale bado kundi hili liliendelea kudai haki yake ya kutambuliwa rasmi na baadae kundi hili likaanza kupata msaada kutoka Rwanda. Hata umoja wa SADC nao ulifanikisha kufanya mazungumzo ambapo kundi hili lilisitisha mapigano rasmi mwaka 2013.

Lakini baadae kundi la M23 likasambaratika na wapiganaji wapatao 1700 wakakimbilia Uganda na wengine wapatao 700 hivi wakakimbilia Rwanda. Hapo waweza kuunganisha "Dots" kwamba kundi jipya la M23 limetokea wapi likiwa na silaha kali na za kisasa zikiwemo la SAM.

Mapema mwaka 2017 kukaanza "Movement" ya wapiganaji kutoka Uganda ambao walianza kuingia nchini Congo DRC na kuanza kupigana na majeshi ya Congo DRC. Mwaka 2021 mapigano mapya yakazuka na kuanza kuenea sehemu mbalimbali za Kivu. Mwaka 2022 vita ikakolea huku M23 ikiwa imara na yenye uwezo wa kuyachachafya majeshi ya Congo DRC.

Uwezo huo wa M23 ndo uloanza kutia shaka kwamba Rwanda yahusika kwa kutoa msaada wa mafunzo, vifaa na mbinu za kijeshi kwa kundi hilo. (Pia Uganda kwa kiasi fulani nayo imetuhumiwa kuhusika na kundi hili (rejea vile vikosi 1700 na 700).

Kwanini M23 wapigania sana Kivu?

Kama nilivyoeleza hapo juu wapiganaji wengi wa M23 watokea sehemu ya kaskazini mwa jimbo la Kivu hususan sehemu za Rutshuru na Masisi ambazo zipo karibu kabisa na mipaka na Rwanda hivyo kuwafanya wapiganaji hawa kuwa na uzoefu mkubwa wa miteremko na maporomoko ya milima ambapo wakiwa juu milimani wapiganaji hawa waweza kuiona Goma.

Rutshuru yenyewe yapakana na Rwanda, Congo DRC na pia Uganda ambapo sehemu hii ina biashara kubwa ambayo yahusisha malori ya mizigo yatokayo Mombasa nchini Kenya na yanokwenda Congo DRC sehemu za Goma na Bukavu kupitia Uganda. Pia sehemu hii ina madini na rasilimali zingine hivyo kuwapa uwezo kundio hili la M23 kukusanya ushuru unotokana na kodi kwa magari yanopita sehemu ya mpaka wa Bunagana.

Sehemu nyingi zenye mogogoro kati ya vikundi vya waasi au magaidi kitu cha kwanza kabisa ni kushikilia vyanzo vya mapato. Hata makundi ya ISIS, Al Shabab, Hamas na makundi linopigana huko Colombia na Uturuki na Yemen ni lazima yawe na vyanzo vya uhakika vya mapato ambapo ushuru wa barabara ni namba moja. Ingawa nisingependa kuliita kindi la M23 kundi la magaidi lakini nalo ni kundi ambalo latumia mbinu zilezile.

Nguvu ya M23 kupigana na kuyazidi nguvu majeshi ya Congo DRC yatokana na nini?

Uwezo mkubwa wa kupigana uliionyeshwa na kundi hili umetia shaka kuwa ni lazima wapewa au wapata msaada kutoka Rwanda au Uganda. Kumekuwepo matumizi ya silaha kali kama vile SAM (Surface to Air Missiles) ambapo kumekuwepo na taarifa za kudunguliwa kwa helikopta kadhaa za jeshi la Congo DRC.

Pia M23 wameonekana na uwezo wa kuhimili mapigano kwa masaa mengi jambo linoashiria kuwa kundi hili wana vifaa vya kisasa kabisa kama vile vyenye kusaidia kuona nyakati za usiku (night vision cameras) na vifaa vingine vya kisasa kama makombora, mizinga na silaha za SMG za kisasa. Ni dhahiri kuwa kama vifaa hivi vimefika mikononi mwa M23 basi kuna msaada mkubwa wa ugavi wa silaha hivi na ndo maana jeshi la Rwanda lahusishwa na kundi hili.

Pia licha ya kupigana kwa kutumia silaha za kisasa, kundi hili la M23 laonekana kupigana vita ya kitaalam yaani ya hatua kwa hatua (Conventional warfare) kuharibu mifumo na silaha za adui kwa kudungua silaha na vifaa vya adui jambo linoashiria kwamba kundi hili lina msaada mkubwa wa kilaama.

Kwa kudhihirisha hilo, leo hii M23 wamefika karibu kabisa na mji wa Goma na mida hii wazuia mizigo na chakula kupitishwa katika barabara kuu za kuelekea kwenye mji huo na pia wameingia katika mji wa Sake uliopo kilomita zipatazo 25 kaskazini magharibi mwa Goma.

Kwa vipi mgogoro huu utapa suluhisho?

Kwanza kabisa tuangalie jeshi la Congo DRC na uwezo wake. Jeshi hili ni la hovyo, lilokosa mpangilio wa kijeshi, lenye uhaba wa silaha na vifaa vya kisasa. Mgao au malipo ya wanajeshi mara nyingi huishia kwa majenerali ambapo huneemeka na misaada ya kijeshi kutoka nje na nchi jirani za Tanzania na Burundi. Pia majenerali hao na viongozi wengine wa kijeshi hutumia muda mwingi kwenda migodini kutafuta dhahabu au madini kwa ajili ya kuuza ili kupata fedha za mabilioni.

Ndo maana leo hii Afrika Kusini wameamua kutuma vikosi vipatavyo 9000 kwenda kusaidia kampeni ya kudhibiti kundi hili la M23.

Mgogoro huu waweza kuisha kwa kurudia makubaliano yalofikiwa miaka 10 ilopita ambapo ilikubaliwa kuwa wapiganaji wa M23 waingizwe kwenye jeshi la Congo DRC jambo ambalo halikutekelezwa. Pia mfumo wa kisiasa wa M23 ulipaswa kutambuliwa na kinyume chake jambo hilo likapuuzwa hadi leo. Endapo M23 wangekuwa wakishiriki harakati za kisiasa huenda leo hii nao wangekuwa na uwakilishi bungeni.

Jambo jingine ambalo wanasiasa wa Congo DRC wataka kulisahau ni ushiriki wa Rwanda katika vita ya kumwondoa aliekuwa raisi wa wakati ule ikiitwa Zaire Mabutu Sese Seko mwaka 1996 ambapo Laurent Kabila alikuja kuwa raisi wa Congo DRC. Hivyo Congo DRC kutokea raisi Joseph Kabila na sasa Felix Tsishekedi wamekuwa wakikwepa kuwa karibu na Rwanda ambayo nayo kwa sababu za kiusalama na kisiasa imewalazimu kuwa macho na Congo DRC.

Rwanda imebakia haina jinsi bali kuachana na kutoa msaada kwa kundi la M23 jambo ambalo ni gumu kwa kuzingatia kuwa Congo DRC wana ushirikiano wa kijeshi na Uganda na pia majeshi yake yamekuwa yakiingia Burundi ambako pia kuna makundi ya waasi ambao pia yahisiwa kuwa yana msaada mkubwa kutoka vikosi vya kijasusi vya Rwanda. Pia Kwa Rwanda kuwaondoa M23 katika maeneo wanoyashikilia ya Kivu na Goma jambo ambalo ni gumu kutokea kutokana na rasilimali kubwa zilizopo katika eneo hilo.

Huko nyuma mwaka 2009 iliwahi kutokea ambapo Rwanda na CNDP walikubaliana na serikali ya Congo DRC kuachana na Goma na Kivu jambo ambalo M23 walilikubali kwa shingo upande kwani liliwaathiri wao zaidi kiuchumi kuliko Congo DRC. Rwanda yataka kuwepo na guarantee kutoka jumuiya ya Afrika Mashariki kwamba vikosi vya kuleta amani vya nchi za maziwa makuu havitaleta athari yoyote ya kiusalama katika eneo la kaskazini mwa mji wa Kivu jambo litopelekea Rwanda kuhisi haiko salama.

Jambo la mwisho ni kwa serikali za Tanzania, Congo DRC, Kenya, Uganda, Burundi na Sudan ya kusini ambazo zaunda Umoja wa Afrika Mashariki kuitisha mkutano na Rwanda ambao utafikia azimio la kuitaka Rwanda kuacha kutoa msaada kwa M23 na pia kuuwa tayati kutuma majeshi yake kwenda Kivu na Goma kusaidia kudhibiti kikundi cha M23 ambacho chaundwa na Wakongo wenye asili ya Rwanda.

Bila hivyo, mgogoro huu utaendelea kuitafuna Congo DRC na kueneza makundi mengi zaidi ya waasi ambayo yatatokana na migogoro mingine iliyopo barani Afrika kama Sudan. Jambo lillo wazi ni kwa serikali ya Congo Kuketi kikao na waasi wa M23 na kuangalia upya makubaliano ya mwaka 2010.

Uchambuzi huu pia umetumia vyanzo mbalimbali kama AP, na Reuters.
Story ngiingi. Pk akipinduliwa Congo aman imerud Chief. Tatizo ni Kagame. Kwanini hawa watutsi Rwanda ndio inaona wasikilizwe kwani hapo hakuna watutsi wa Burundi
 
M23 wapo kwenye rasilimali nyingi,halafu wanalalamika wanatengwa na DRC wanachukua maamuzi wajitenge.

Kuna kitu hakiko sawa.
Jibu lake ni kwamba Goma ni mji wenye ofisi nyingi za kibalozi na za kimataifa kutoka nchi mbalimbali duniani kutokana na umuhimu wake kiuchumi kwa kusaidia uchimbaji wa madini.

Pia mataifa mengi ya nje pamoja na vikosi vya kulinda amani nchini Congo DRC macho yao yamekuwa ni Goma.

Hivyo Goma haiwezi kuachiwa M23 iwe yao kivyao ni jambo ambalo litapingwa ziku zote na Congo DRC, mataifa hayo pamoja na mataifa yote ya Afrika sehemu ya maziwa makuu.

Goma ni "centre of gravity" ya mataifa makubwa duniani.
 
Back
Top Bottom