Tanzania isitishe uhusiano na Rwanda juu ya DRC?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Nchi ya Rwanda imekuwa ikidaiwa kuhusika sana na machafuko ya DRC na kuwa vyanzo mbalimbali (hasa vya Umoja wa Mataifa na nchi za Magharibi) vinaonesha kuwa Rwanda ndio inaunga mkono na kusapoti kundi la waasi la M23. Je, Tanzania ina msimamo gani kuhusu Rwanda na kuhusija kwake na mgogoro wa Congo? Je wakati umefika kwa Tanzania kuchukua msimamo mkali ikiwemo kuzuia Rwanda kutumia bandari zetu kupitisha silaha ambazo nyingine zinaishia mikononi mwa waasi?
 
tanzania ni shamba la bibi, kila mtu ana uhuru wa kujisevia! waacheni warwandese wapumulie kwetu!!
 
Nadhani historia inatufundisha jambo hapa.
Kagame ndiye alikuwa anamlea Laura Nkunda. Baada ya Mkapa, Anan na Obasanjo kumlazimisha amkamate hali ilikuwa tulivu kwa muda. Sina shaka kuwa anatumia kundi hilo kama mbadala wa Nkunda.
Nadhani ni wakti EAC ifanye jambo ikiwa ni pamoja na kuzuia usafirishaji wa silaha.
 
Mhnnn...,
Mzee hata anga za kimataifa humo. Find out kama Tanzania haipo kinshansa kumlinda Kabila, find out kama Tanzania haisapoti kijeshi the DRC. all in all before Tanzania gets there, rebels might have genuine reasons. Wasikurupuke kama Membe alivyofanya -Libya case.
 
Matatizo ya ndani yanailemea Tz , Tuombe wapinzani wa watawala wasipate msaada wa Rwanda
 
Jambo moja lipo wazi,Tanzania,Kenya,Msumbiji,South Africa,Namibiana Angola wakikataa kupitisha silaha zinazoenda kwa nchi zinazosemekana zinasaidia rebels waasi wote wanaosumbua Drc wangedhoofika ma wangedhibitiwa. Sioni inashindikana nini!
 
Hivi mtu amewahi kujiuliza silaha zinawafikiaje "waasi"... who are the gun runners of East Africa?

JF intelligency would properly answer your question. What about gongo la mboto scandal? Link the former rebel fighters in BDI with current friendship with Tzn gvt ...and all of that...
 
Mzee Mwanakijiji,

..YES, tunapaswa kuchukua msimamo mkali kuhusu mgogoro wa DRC.

..tunafanya makosa makubwa kuvumilia unyama wa Rwanda na Uganda dhidi ya wananchi wa DRC.
 
Last edited by a moderator:
Nchi ya Rwanda imekuwa ikidaiwa kuhusika sana na machafuko ya DRC na kuwa vyanzo mbalimbali (hasa vya Umoja wa Mataifa na nchi za Magharibi) vinaonesha kuwa Rwanda ndio inaunga mkono na kusapoti kundi la waasi la M23. Je, Tanzania ina msimamo gani kuhusu Rwanda na kuhusija kwake na mgogoro wa Congo? Je wakati umefika kwa Tanzania kuchukua msimamo mkali ikiwemo kuzuia Rwanda kutumia bandari zetu kupitisha silaha ambazo nyingine zinaishia mikononi mwa waasi?

Unataka kuivunja jumuiya ya Afrika Mashariki? Mbona huisemi Uganda ambayo nayo imeshutumiwa na ikatishia kujitoa Somalia?
 
Jambo moja lipo wazi,Tanzania,Kenya,Msumbiji,South Africa,Namibiana Angola wakikataa kupitisha silaha zinazoenda kwa nchi zinazosemekana zinasaidia rebels waasi wote wanaosumbua Drc wangedhoofika ma wangedhibitiwa. Sioni inashindikana nini!

Mkuu unadhani nani ananufaika na vita ya Kongo?
 
Kimbunga,

..EAC ni Kenya na Tanzania, hao wengine ni wadandiaji tu.

..pia SADC ina potential kubwa kuliko EAC.
 
Last edited by a moderator:
Unataka kuivunja jumuiya ya Afrika Mashariki? Mbona huisemi Uganda ambayo nayo imeshutumiwa na ikatishia kujitoa Somalia?

hayo ni maswali na wewe unaweza kuongezea tu... siwezi kufikiria kila scenario ya kumridhisha kila mtu, kila wakati...na kwa kila kitu. Ndio maana ya kuwa na mijadala.
 
Mimi naona kama vile itakuwa ni unafiki tu....na tutasutwa! Hivi Tz ilihusikaje katika kumtoa Mobutu madarakani? - Nazungumzia support tuliyowapa hawa kina Kabila na wengineo waliokuwa wakipinga utawala wa Mobutu. Mpaka leo jumba la kina Kabila lipo pale Mbezi. Vipi kuhusu kina Museveni? Au hayo yalikuwa na matatizo tofauti sana na hili la sasa la Congo?
 
Mhnnn...,
Mzee hata anga za kimataifa humo. Find out kama Tanzania haipo kinshansa kumlinda Kabila, find out kama Tanzania haisapoti kijeshi the DRC. all in all before Tanzania gets there, rebels might have genuine reasons. Wasikurupuke kama Membe alivyofanya -Libya case.
Kwani Laura Nkunda alikuwa na''genuine reasons'' zipi?
 
Kingine nachoshangaa watu wengi wa Congo na hasa hawa public figure na wasanii wakubwa huwa mawaona kama wapo less concerned na mambo ya nchi yao,watu wa nje ya nchi yao na wanasiasa ndio naona wapo concerned zaidi. Chukulia mfano wa Koffi,Papa wemba,werason,jb moiana,nyoshi,samba mapangala,solomon mukubwa nk,mbona hatuoni wakiungana katika jitihada za kutafuta amani ya kudumu Drc? Wengi wao naona kama ni wapenda starehe na matanuzi tu...
 
Unataka kufanya mjadala uwe mlefu. Jambo moja nakumbuka Nkunda na wenzake walitaka utambulisho kama Mkongo-there might be other reasons. How genuine that is-further political negotiations are needed with/without Tnz interventions.
 
hayo ni maswali na wewe unaweza kuongezea tu... siwezi kufikiria kila scenario ya kumridhisha kila mtu, kila wakati...na kwa kila kitu. Ndio maana ya kuwa na mijadala.

Rwanda ni mwanachama wa Jumuiya ya Afrika mashariki; |jumuiya ya afrika mashariki inataka iwe shirikisho la kisiasa. Nadhani ni muda muafaka sasa waonyanye na kuambiana ukweli. Kuna wakati nilisikia walikaa Uganda kama mara mbili hivi lakini out come sikuiona zaidi ya General Bosco Ntaganda na mwenzake general Sultani Makenga kukaribia kuiteka Goma. Mkuu hili si suala la Tanzania kuvunja uhusiano bali suala la jumuiya ya Afrika mashariki kulisemea.
 
Back
Top Bottom