Tanzania isitishe uhusiano na Rwanda juu ya DRC?

Hivi kwanini huwa tunaamini kila kinachosemwa na nchi za magharibi kuwa ni cha kweli? Kwanini tusiamini kile watuhumiwa wanachokisema? Hebu refer hotuba ya Kagame kuhusu hizi allegations...

Exclusive: Kagame
Wazungu wana interest zao ktk nchi za Africa na wakiona kiongozi yeyote mwenye nia yakuwafanya waafrica waamke nakuwa na confidence na maamuzi yao then anakuwa threat kwa wazungu na lazima watafute namna yakumchafua kama siyo kumwondolea uhai! We unadhani viongozi wote wa Africa wanaokufa vifo vya ghafla wanakufa kawaida?

Anyway, inategemea mtu umesimama wapi na unataka kuona nini!

Nchi ya Rwanda imekuwa ikidaiwa kuhusika sana na machafuko ya DRC na kuwa vyanzo mbalimbali (hasa vya Umoja wa Mataifa na nchi za Magharibi) vinaonesha kuwa Rwanda ndio inaunga mkono na kusapoti kundi la waasi la M23. Je, Tanzania ina msimamo gani kuhusu Rwanda na kuhusija kwake na mgogoro wa Congo? Je wakati umefika kwa Tanzania kuchukua msimamo mkali ikiwemo kuzuia Rwanda kutumia bandari zetu kupitisha silaha ambazo nyingine zinaishia mikononi mwa waasi?
 
Tanzania haiko katika nafasi nzuri kusuluhisha au kutoa tamko, kama silaha zinapitishwa kutumia bandari yetu then we are guilty kama Rwanda kwa ku aid waasi wa M23

Kwani Tanzania imeikatalia serikali ya Kongo kupitisha silaha zao Tanzania? hivi Tanzania kama nchi yenye bandari itazikataliaje nchi jirani kama Rwanda kupitisha silaha zake?

Matatizo ya Kongo ni ya Wakongo wenyewe na serikali yao na ni wao wenyewe wanaoweza kuyatatua,kama Rais Kabila ni dhaifu atolewe tu la akachutame kwa vijana wa M23 warudi kwenye jeshi la serikali..
 
Mzee Mwanakijiji,ungejuwa watu wanaonufaika na vita vya Congo,wala usingejisumbuwa kusema Tanzania wafanye lolote.Hizi ni zama mpya mkuu.

Congo is extremely wealthy,lakini pia vita vyake vimekuwa regarded as vita vya tatu vya dunia.Kwa miaka tisa tu(1994-2003),watu zaidi ya milioni 5 wameuwawa kwenye vita hivyo!

Hiyo ni number kubwa sana!Lakini kama nilivyosema,fuatilia uone nani ananufaika na hivyo vita(ikiwemo utajiri wa Congo).

Ujuwe achilia mbali diamond,gold,copper,cobalt na zinc,Congo pia wanasupply coltan ambazo zinatumika kwenye mobile phones.

Mbali ya corporations na warlords ambao wametumika kuwagawa wananchi in ethnic groups,bado kuna nchi kama Namibia,Zimbabwe na Angola ambao nao walijichumia utajiri wa Congo kama wanavyotaka.

Tatizo la Rwanda na Congo halikuanzishwa na Kagame vs Kabila kama wengi wanavyodhani,tatizo lilianzia kwenye vita vya Rwanda kati ya watusi na wahutu,watusi walipochukuwa madaraka Rwanda,wahutu(waliokadiriwa kuwa milioni mbili na zaidi),walikimbilia Congo ikiwa chini ya Mobutu.

Hao wahutu walijiunga na Mobutu,lakini wakawa wanawauwa wa Tutsi walioko Congo ambao ni minorities na wameishi Congo kwa vizazi vingi.Watu nadhani hawajui kuwa kuna watutsi wa kutosha tu huko Congo ambao wana asili ya hapo Congo na si wanyarwanda.

Baada ya wahutu waliohamia Congo kuanza kuwauwa watutsi ambao ni wakongo,Rwanda ndipo walipoanza kuwasapoti watutsi wa pale ili kuwalinda na mauwaji ya wahutu waliokuwa wakishirikiana na serikali ya Mobutu.

Na ni watutsi baada ya kusaidiwa na Uganda pia,ndiyo walimwondoa madarakani Mobutu na kumweka Kabila,na Kabila mwenyewe aliishi Tanzania na tulimsapoti,so hadi hadi hapo nadhani wengi hawajui kuwa Kabila nyuma yake alikuwa ni Rwanda na watutsi,na kama ni kupingana na Rwanda,tungefanya hivyo toka kipindi wakimweka Kabila.

Na kitendo cha Kabila kushindwa kuwashughulikia wahutu ndicho kilimsababisha akauwawa tena na watutsi ambao waliondoa imani kwake.

Na kabila baada ya kuona watutsi wamemgeuka ndiyo akaomba msaada kutoka kwa Zimbabwe,Namibia na Angola,jambo ambalo lilisababisha even more instability kwasababu nchi hizo zina maslahi yake binafsi.

General Nkunda aliwekwa under house arrest baada ya makubaliano kati ya serikali za Rwanda na DRC kuwa watashirikiana kupigana na kundi la waasi la FDLR ambalo ni la masalia ya wahutu waliokuwa kwenye maeneo ya kaskazini na kusini mwa Kivu huko Congo.

Tatizo lililopo ni kwamba licha ya serikali ya Congo kusaidiwa na majeshi ya UN(peace keepers),bado wameshindwa kulifutilia mbali kundi la wahutu la FDLR.

Na baada ya wanyarwanda(Tutsi) kuona kwamba serikali ya Congo imeshindwa kazi kama walivyokubaliana(ikiwa ni pamoja na kuwaondoa wahasi wa FDLR ambao ni wahutu),ndipo kundi la M23 lilipoanzishwa na kujijenga ili kuendeleza pale kina Kabila waliposhindwa(kuwaprotect watutsi wa Congo).

Na kwasababu UN peace keepers wameshindwa kuzuia mauwaji na hata crimes zinazoendelea,rais Kabila hivi majuzi amewataka waondoke nchini Congo.Na ni UN panel ambayo ilisema kuwa Uganda nao wanawasapoti M23.

Lakini pia UN nao pamoja na kuwa na majeshi yao,bado mauwaji ya raia yanaendelea kama kawaida chini ya uangalizi wao.

Na pia baadhi ya rebels wamekuwa wakishirikiana na makundi ya kihalifu kuanzia Africa,Western Europe hadi North America,sasa ndipo utashangazwa na kazi ya UN,yani mataifa makubwa huwa hayawashughulikii wahalifu wao kama wanaiba nje ya nchi.Hii ina maana wananufaika na kile ambacho makundi ya kihalifu toka nchini mwao yanafanya huko Congo!

Kwa hiyo usishangazwe na kutokupatikana kwa amani huko Congo.Utajiri walionao unakuwa exploited kutokana na tofauti zao.Kama tunategemea sijui eti UN ama hayo mataifa ya Western Europe na North America,ndipo tutakuwa tumeliwa kubwa!Kwa mfano taarifa zinasema kuwa ni makundi ya wahalifu wa mataifa hayo,sasa nani anajuwa kuwa kumepenyezwa wanajeshi na majasusi kwa kutumia mwavuli wa wahalifu?Je wahalifu hao wanauza wapi hizo RM na wanatoa wapi hizo silaha za kuwauzia?

Tunavyozungumza hapa,Kabila amepanda ndege kwenda Kampala kusuluhishwa,ila kiukweli ni kwamba wananchi w Congo nao wameshachoshwa na Kabila.
 
Unachukulia masuala ya silaha kirahisi lakini sioni kama Tanzania inaweza ku broker mapatano yoyote kama na yenyewe haiwezi simama kati, ikiwa tunapitisha silaha zinazoenda kuua wamama na watoto wasio hatia vipi tunaweza kukemea au kuleta mapatano....
 
kwa sasa Rwanda rebels wameshaiteka Goma,soon ramani ya rwanda itabadilishwa,Kagame na Kabila wako Kampala for peace negotiation
 
Hivi mtu amewahi kujiuliza silaha zinawafikiaje "waasi"... who are the gun runners of East Africa?

Kongo vigumu sana kuzuia uingizwaji wa silaha kwani siyo landlocked na misitu kedekede ambako chopper inaweza kuwatelemshia huko. Chezea bongo za watu nini. Na sasa wameshateka airport access ni kubwa tu. Kuna mambo yao wakongo, wakongo wengi huenda hawapendezwi na mfumo wa kifalme ndio yale yale tunayoyalalamikia hapa vigogo kuwarithisha watoto wao. Kabila baada ya kifo mwanae karidhi, na huenda naye anamwandaa mwanaye kuchukua dola. Haya tuwaachie Wakongo wenyewe. Wakati mwingine kukaa kimya ni busara.
 
Ni kweli hii ni ishu ya wacongo kudeal nayo ,tz tuna matatizo yetu chungu nzima ambayo tumeshindwa kuyapatia ufumbuzi,sioni kama ni busara kuingilia ishu za nchi zingine let the congelese and rwandese solve their own problems!
Kongo vigumu sana kuzuia uingizwaji wa silaha kwani siyo landlocked na misitu kedekede ambako chopper inaweza kuwatelemshia huko. Chezea bongo za watu nini. Na sasa wameshateka airport access ni kubwa tu. Kuna mambo yao wakongo, wakongo wengi huenda hawapendezwi na mfumo wa kifalme ndio yale yale tunayoyalalamikia hapa vigogo kuwarithisha watoto wao. Kabila baada ya kifo mwanae karidhi, na huenda naye anamwandaa mwanaye kuchukua dola. Haya tuwaachie Wakongo wenyewe. Wakati mwingine kukaa kimya ni busara.
 
Hivi msasani iko wilaya ya Temeke?,naona zile chai za pale kwa wahindi wa K.T Shop zimekulevya ndugu!!
 
Hivi na yule anayefikia pale kariakoo Nyavyamo Guest H'se na Madhahabu yake naye pia ni mgeni wa Rwanda?
 
Unachukulia masuala ya silaha kirahisi lakini sioni kama Tanzania inaweza ku broker mapatano yoyote kama na yenyewe haiwezi simama kati, ikiwa tunapitisha silaha zinazoenda kuua wamama na watoto wasio hatia vipi tunaweza kukemea au kuleta mapatano....

The thing is Rwanda ni nchi huru na inaruhusiwa kununua silaha kwa matumizi yake binafsi na sisi kama majirani hatuwezi kuwazuia japokua ni kweli kabisa tunafahamu kuwa end user ni wale waasi.

Hapo ndio inapokuja ile dhana ya keep your enemies closer ndio tunayoitumia hapa kwa nia njema( Japokua pia kutokana na rushwa kuna watu wanatake advantage na kujinufaisha)

Tanzania tuko kwenye nafasi nzuri zaidi kuliko mataifa yote kuweza kuikemea Rwanda sasa. Tuna vijana kule tayari kama advisers( Congo) na pia juzi juzi tumepewa jukumu la kuongoza Task force ya kuwachapa hao M23 chini ya Brig James Mwakibolwa(JVM) kwahiyo si kweli kuwa haiwezekani. Ni vitu ambavyo vinafanyika tayari Kagame na Museveni wanapumulia mashine sasa hivi.
 
Hivi vitu vyote ni matatizo yanayotengenezwa na mayahudi kupitia UN halafu mnapeleka lawama kwa watu wasiohusika ili kuendeleza uhasama baina ya majirani.
Hii ndiyo hali ya Syria na ilivyokuwa Libya.Nani anayefaidika zaidi ya Marekani na majambazi wenzake.Hali ndiyo hiyo hiyo ya Uamsho wa Zanzibar na uchochezi unaoendelea Tanzania baina ya waislamu na wakristo.
Katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuna watu wao makini wa kuunga mkono hujuma zao.
 
The thing is Rwanda ni nchi huru na inaruhusiwa kununua silaha kwa matumizi yake binafsi na sisi kama majirani hatuwezi kuwazuia japokua ni kweli kabisa tunafahamu kuwa end user ni wale waasi.

Hapo ndio inapokuja ile dhana ya keep your enemies closer ndio tunayoitumia hapa kwa nia njema( Japokua pia kutokana na rushwa kuna watu wanatake advantage na kujinufaisha)

Tanzania tuko kwenye nafasi nzuri zaidi kuliko mataifa yote kuweza kuikemea Rwanda sasa. Tuna vijana kule tayari kama advisers( Congo) na pia juzi juzi tumepewa jukumu la kuongoza Task force ya kuwachapa hao M23 chini ya Brig James Mwakibolwa(JVM) kwahiyo si kweli kuwa haiwezekani. Ni vitu ambavyo vinafanyika tayari Kagame na Museveni wanapumulia mashine sasa hivi.
Wajinga tu nyie!.Ya kwenu yanawashinda halafu mnapangiwa kazi nyengine.Na nani huyo anayewapa kazi hiyo?.
 
Mzee Mwanakijiji,ungejuwa watu wanaonufaika na vita vya Congo,wala usingejisumbuwa kusema Tanzania wafanye lolote.Hizi ni zama mpya mkuu.

Congo is extremely wealthy,lakini pia vita vyake vimekuwa regarded as vita vya tatu vya dunia.Kwa miaka tisa tu(1994-2003),watu zaidi ya milioni 5 wameuwawa kwenye vita hivyo!

Hiyo ni number kubwa sana!Lakini kama nilivyosema,fuatilia uone nani ananufaika na hivyo vita(ikiwemo utajiri wa Congo).

Ujuwe achilia mbali diamond,gold,copper,cobalt na zinc,Congo pia wanasupply coltan ambazo zinatumika kwenye mobile phones.

Mbali ya corporations na warlords ambao wametumika kuwagawa wananchi in ethnic groups,bado kuna nchi kama Namibia,Zimbabwe na Angola ambao nao walijichumia utajiri wa Congo kama wanavyotaka.

Tatizo la Rwanda na Congo halikuanzishwa na Kagame vs Kabila kama wengi wanavyodhani,tatizo lilianzia kwenye vita vya Rwanda kati ya watusi na wahutu,watusi walipochukuwa madaraka Rwanda,wahutu(waliokadiriwa kuwa milioni mbili na zaidi),walikimbilia Congo ikiwa chini ya Mobutu.

Hao wahutu walijiunga na Mobutu,lakini wakawa wanawauwa wa Tutsi walioko Congo ambao ni minorities na wameishi Congo kwa vizazi vingi.Watu nadhani hawajui kuwa kuna watutsi wa kutosha tu huko Congo ambao wana asili ya hapo Congo na si wanyarwanda.

Baada ya wahutu waliohamia Congo kuanza kuwauwa watutsi ambao ni wakongo,Rwanda ndipo walipoanza kuwasapoti watutsi wa pale ili kuwalinda na mauwaji ya wahutu waliokuwa wakishirikiana na serikali ya Mobutu.

Na ni watutsi baada ya kusaidiwa na Uganda pia,ndiyo walimwondoa madarakani Mobutu na kumweka Kabila,na Kabila mwenyewe aliishi Tanzania na tulimsapoti,so hadi hadi hapo nadhani wengi hawajui kuwa Kabila nyuma yake alikuwa ni Rwanda na watutsi,na kama ni kupingana na Rwanda,tungefanya hivyo toka kipindi wakimweka Kabila.

Na kitendo cha Kabila kushindwa kuwashughulikia wahutu ndicho kilimsababisha akauwawa tena na watutsi ambao waliondoa imani kwake.

Na kabila baada ya kuona watutsi wamemgeuka ndiyo akaomba msaada kutoka kwa Zimbabwe,Namibia na Angola,jambo ambalo lilisababisha even more instability kwasababu nchi hizo zina maslahi yake binafsi.

General Nkunda aliwekwa under house arrest baada ya makubaliano kati ya serikali za Rwanda na DRC kuwa watashirikiana kupigana na kundi la waasi la FDLR ambalo ni la masalia ya wahutu waliokuwa kwenye maeneo ya kaskazini na kusini mwa Kivu huko Congo.

Tatizo lililopo ni kwamba licha ya serikali ya Congo kusaidiwa na majeshi ya UN(peace keepers),bado wameshindwa kulifutilia mbali kundi la wahutu la FDLR.

Na baada ya wanyarwanda(Tutsi) kuona kwamba serikali ya Congo imeshindwa kazi kama walivyokubaliana(ikiwa ni pamoja na kuwaondoa wahasi wa FDLR ambao ni wahutu),ndipo kundi la M23 lilipoanzishwa na kujijenga ili kuendeleza pale kina Kabila waliposhindwa(kuwaprotect watutsi wa Congo).

Na kwasababu UN peace keepers wameshindwa kuzuia mauwaji na hata crimes zinazoendelea,rais Kabila hivi majuzi amewataka waondoke nchini Congo.Na ni UN panel ambayo ilisema kuwa Uganda nao wanawasapoti M23.

Lakini pia UN nao pamoja na kuwa na majeshi yao,bado mauwaji ya raia yanaendelea kama kawaida chini ya uangalizi wao.

Na pia baadhi ya rebels wamekuwa wakishirikiana na makundi ya kihalifu kuanzia Africa,Western Europe hadi North America,sasa ndipo utashangazwa na kazi ya UN,yani mataifa makubwa huwa hayawashughulikii wahalifu wao kama wanaiba nje ya nchi.Hii ina maana wananufaika na kile ambacho makundi ya kihalifu toka nchini mwao yanafanya huko Congo!

Kwa hiyo usishangazwe na kutokupatikana kwa amani huko Congo.Utajiri walionao unakuwa exploited kutokana na tofauti zao.Kama tunategemea sijui eti UN ama hayo mataifa ya Western Europe na North America,ndipo tutakuwa tumeliwa kubwa!Kwa mfano taarifa zinasema kuwa ni makundi ya wahalifu wa mataifa hayo,sasa nani anajuwa kuwa kumepenyezwa wanajeshi na majasusi kwa kutumia mwavuli wa wahalifu?Je wahalifu hao wanauza wapi hizo RM na wanatoa wapi hizo silaha za kuwauzia?

Tunavyozungumza hapa,Kabila amepanda ndege kwenda Kampala kusuluhishwa,ila kiukweli ni kwamba wananchi w Congo nao wameshachoshwa na Kabila.

...This is by far one of the best analysis that one can find,big up jMush at least umejaribu kuonyesha angle zote za Congo crisis bila kuweka politics
 
Sisi wenyewe hatujiwezi. Unategemea tutasema kitu?
 
Mhnnn...,
Mzee hata anga za kimataifa humo. Find out kama Tanzania haipo kinshansa kumlinda Kabila, find out kama Tanzania haisapoti kijeshi the DRC. all in all before Tanzania gets there, rebels might have genuine reasons. Wasikurupuke kama Membe alivyofanya -Libya case.

Huyo ndio Mwanakijiji anatandawika kila anga .. Namkubali.. Chezea Mwanakijiji wewe
 
jmushi1,

..kuna mambo ambayo umeyaacha ktk posting yako, hali ambayo inaweza kuwachanganya wasomaji wako.

..Mkuu wa majeshi ya Congo wakati wa Kabila Sr alikuwa ni Maj.Gen.James Kabarebe ambaye sasa hivi ndiyo mkuu wa majeshi ya Rwanda.

..kwa msingi Kabila Sr hakupaswa kubeba mzigo wa lawama za kushindwa kuwadhibiti Wahutu. aliyepaswa kulaumiwa hapo ni James Kabarebe ambaye alikuwa anaongoza majeshi ya Congo, pamoja na vikosi vya Rwanda vilivyokuwa ndani ya Congo.

..Rwanda hawakuingia Congo kuwalinda Watutsi wa huko, bali kuzuia wakimbizi wa Kihutu wasiweze kujipanga upya na kurudi Rwanda kuiangusha serikali ya Watutsi ya RPF.

..wakati wakielekea Kinshasa, vikosi vya Rwanda vilivyokuwa vikimsaidia Kabila Sr viliuwa Wahutu wengi mno, na inaaminika kwamba baadhi yao walikuwa unarmed, wanawake, na watoto. UN ilijaribu kupeleka wachunguzi kufuatilia tuhuma hizo lakini Kabila Sr, kutokana na ukaribu wake na Rwanda, aliwazuia.

..Kitendo cha Kabila Sr kuzuia wachunguzi wa UN kilimjengea sifa mbaya ktk jumuiya ya kimataifa. Kabila Sr pia alijijengea maadui wengine baada ya kufuta leseni za uchimbaji madini za makampuni ya nchi za magharibi. Internally, askari wa Kinyarwanda walikuwa wana-miss behave na hivyo kumfanya Kabila Sr aonekane ni kibaraka machoni mwa Wacongomani.

..Ili kujijengea uhalali kwa wananchi wake, na kurudisha heshima ya serikali yake kimataifa, Kabila Sr aliamua kuruhusu uchunguzi wa UN, na kuwarudisha nyumbani wanajeshi wa Rwanda waliokuwa stationed Congo. Within a month, majeshi ya Rwanda yaliamua kumvamia Kabila Sr Kinshasa.

..Zimbabwe iliingia ktk vita vya Congo kwasababu wao ndiyo waliotoa silaha na pesa za kumuondoa Mobutu madarakani. Ilikuwa ni lazima wahakikishe Kabila Sr anabaki madarakani ili waweze kurudisha pesa zao. Angola walilazimika kuingia kijeshi kwa kuogopa Jonas Savimbi asiweke base yake Congo. Pia Rwanda na Uganda walianza kuwa na mahusiano ya kijeshi na Jonas Savimbi. Namibia walikuwa wakiburuzwa tu na marafiki zao wa Zimbabwe na Angola.

..mwisho, Congo ni mwanachama wa SADC, na mkataba wa ulinzi wa jumuiya hiyo ndiyo uliohalalisha Zimbabwe, Angola, na Namibia, kupeleka askari wao Congo. Swali la kujiuliza ni kwanini Tanzania iliondoa askari wake waliokuwepo Kitona wakati Kabila Snr anavamiwa na Rwanda?? Pia kwanini hatukulaani uvamizi huo? Zaidi, kwani Afrika Kusini iliwatambua waasi vibaraka waliokuwa wakisaidiwa na Rwanda, na kuanza kuhoji uhalali wa Zimbabwe kupeleka vikosi vyake kumsaidia Kabila Snr??
 
Sisi wenyewe hatujiwezi. Unategemea tutasema kitu?

Hatujiwezi mbele ya nani? Ni kweli hatujiwezi mbele ya Rwanda,DRC na Uganda? We have a great role to play to stop innocent blood shade in DRC.
 
Mzee Mwanakijiji,ungejuwa watu wanaonufaika na vita vya Congo,wala usingejisumbuwa kusema Tanzania wafanye lolote.Hizi ni zama mpya mkuu.

Congo is extremely wealthy,lakini pia vita vyake vimekuwa regarded as vita vya tatu vya dunia.Kwa miaka tisa tu(1994-2003),watu zaidi ya milioni 5 wameuwawa kwenye vita hivyo!

Hiyo ni number kubwa sana!Lakini kama nilivyosema,fuatilia uone nani ananufaika na hivyo vita(ikiwemo utajiri wa Congo).

Ujuwe achilia mbali diamond,gold,copper,cobalt na zinc,Congo pia wanasupply coltan ambazo zinatumika kwenye mobile phones.

Mbali ya corporations na warlords ambao wametumika kuwagawa wananchi in ethnic groups,bado kuna nchi kama Namibia,Zimbabwe na Angola ambao nao walijichumia utajiri wa Congo kama wanavyotaka.

Tatizo la Rwanda na Congo halikuanzishwa na Kagame vs Kabila kama wengi wanavyodhani,tatizo lilianzia kwenye vita vya Rwanda kati ya watusi na wahutu,watusi walipochukuwa madaraka Rwanda,wahutu(waliokadiriwa kuwa milioni mbili na zaidi),walikimbilia Congo ikiwa chini ya Mobutu.

Hao wahutu walijiunga na Mobutu,lakini wakawa wanawauwa wa Tutsi walioko Congo ambao ni minorities na wameishi Congo kwa vizazi vingi.Watu nadhani hawajui kuwa kuna watutsi wa kutosha tu huko Congo ambao wana asili ya hapo Congo na si wanyarwanda.

Baada ya wahutu waliohamia Congo kuanza kuwauwa watutsi ambao ni wakongo,Rwanda ndipo walipoanza kuwasapoti watutsi wa pale ili kuwalinda na mauwaji ya wahutu waliokuwa wakishirikiana na serikali ya Mobutu.

Na ni watutsi baada ya kusaidiwa na Uganda pia,ndiyo walimwondoa madarakani Mobutu na kumweka Kabila,na Kabila mwenyewe aliishi Tanzania na tulimsapoti,so hadi hadi hapo nadhani wengi hawajui kuwa Kabila nyuma yake alikuwa ni Rwanda na watutsi,na kama ni kupingana na Rwanda,tungefanya hivyo toka kipindi wakimweka Kabila.

Na kitendo cha Kabila kushindwa kuwashughulikia wahutu ndicho kilimsababisha akauwawa tena na watutsi ambao waliondoa imani kwake.

Na kabila baada ya kuona watutsi wamemgeuka ndiyo akaomba msaada kutoka kwa Zimbabwe,Namibia na Angola,jambo ambalo lilisababisha even more instability kwasababu nchi hizo zina maslahi yake binafsi.

General Nkunda aliwekwa under house arrest baada ya makubaliano kati ya serikali za Rwanda na DRC kuwa watashirikiana kupigana na kundi la waasi la FDLR ambalo ni la masalia ya wahutu waliokuwa kwenye maeneo ya kaskazini na kusini mwa Kivu huko Congo.

Tatizo lililopo ni kwamba licha ya serikali ya Congo kusaidiwa na majeshi ya UN(peace keepers),bado wameshindwa kulifutilia mbali kundi la wahutu la FDLR.

Na baada ya wanyarwanda(Tutsi) kuona kwamba serikali ya Congo imeshindwa kazi kama walivyokubaliana(ikiwa ni pamoja na kuwaondoa wahasi wa FDLR ambao ni wahutu),ndipo kundi la M23 lilipoanzishwa na kujijenga ili kuendeleza pale kina Kabila waliposhindwa(kuwaprotect watutsi wa Congo).

Na kwasababu UN peace keepers wameshindwa kuzuia mauwaji na hata crimes zinazoendelea,rais Kabila hivi majuzi amewataka waondoke nchini Congo.Na ni UN panel ambayo ilisema kuwa Uganda nao wanawasapoti M23.

Lakini pia UN nao pamoja na kuwa na majeshi yao,bado mauwaji ya raia yanaendelea kama kawaida chini ya uangalizi wao.

Na pia baadhi ya rebels wamekuwa wakishirikiana na makundi ya kihalifu kuanzia Africa,Western Europe hadi North America,sasa ndipo utashangazwa na kazi ya UN,yani mataifa makubwa huwa hayawashughulikii wahalifu wao kama wanaiba nje ya nchi.Hii ina maana wananufaika na kile ambacho makundi ya kihalifu toka nchini mwao yanafanya huko Congo!

Kwa hiyo usishangazwe na kutokupatikana kwa amani huko Congo.Utajiri walionao unakuwa exploited kutokana na tofauti zao.Kama tunategemea sijui eti UN ama hayo mataifa ya Western Europe na North America,ndipo tutakuwa tumeliwa kubwa!Kwa mfano taarifa zinasema kuwa ni makundi ya wahalifu wa mataifa hayo,sasa nani anajuwa kuwa kumepenyezwa wanajeshi na majasusi kwa kutumia mwavuli wa wahalifu?Je wahalifu hao wanauza wapi hizo RM na wanatoa wapi hizo silaha za kuwauzia?

Tunavyozungumza hapa,Kabila amepanda ndege kwenda Kampala kusuluhishwa,ila kiukweli ni kwamba wananchi w Congo nao wameshachoshwa na Kabila.

Akhsante kwa uchambuzi mkuu JMUSHI,binafsi mengi nilikuwa siyajui nimejifunza kutoka kwako.
 
Kimbunga,

..EAC ni Kenya na Tanzania, hao wengine ni wadandiaji tu.

..pia SADC ina potential kubwa kuliko EAC.
Sio Kweli, Tanzania inanufaika zaidi na EAC kuliko SADC na nadhani kanuni za biashara za kimataifa zinataka nchi isiwe mwanachama wa zaidi ya jumuiya moja ya kiuchumi. Tz inapaswa kujitoa SADC kinachozuia na kwa Kenya na Uganda bado hazijajitoa COMESA.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom