Ngongo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2008
- 18,921
- 31,161
Heshima kwako W J Malecela.
Unaweza kumwelezea Sheikh Yahaya Hussen ndani ya jamii yetu kama ifuatavyo.
[1] Mtabiri.
Kazi yake ya utabiri ilifahamika afrika mashariki na maeneo mbali mbali duniani.Alifanya kazi ya utabiri hadi mauti ilipomkuta.Unaweza kumhukumu Sheikh Yahaya kwa kazi ya utabiri lakini wapo wengi waliofaidika na utabiri wake.
[2] Kiongozi wa kiroho [Sheikh]
Sheikh Yahaya Hussein kwa nyakati tofauti aliwahi kushika madaraka makubwa ndani ya BAKWATA taifa.Mara wa mara nimemshuhudia akisoma Quran ndani ya misikiti mbali mbali.Sheikh yahaya Hussein ni mmoja wa mwanzilishi wa mashindano ya usomaji wa Quran Tanzania.Najua wapo wapinzani wake kibao wanaohoji ushiriki wake wa utabiri unaopingana na dini ya kIslamu mara nyingi amekuwa akitoa ufafanuzi fasaha dhidi ya wapinzani wake.
[3] Kachero / Shushu.
Lazima nikiri nilikuwa sijawahi kusikia habari za Sheikh Yahaya Hussein na ushushu lakini baada ya kusoma kitabu cha Mwl Ludovick Mwijage 'The dark side of Nyerere' ndio nikajua kumbe Sheikh alikuwa na kazi nyingine nyuma ya pazia.Enzi za vita baridi ushushu ulikuwa juu sana huwezi kutarajia mtu wa aina ya Sheikh Yahaya aweza kuwa shushu !.
[4] Mbabaishaji.
Nadhani kuelekea mwisho wa maisha yake Sheikh Yahaya Hussein alikuwa amepigikika kimaisha.Kuna baadhi ya mambo yaliashiria Sheikh alikuwa ameishiwa au hakuwa na fedha za kutosha kumudu maisha yake sawa sawa.Utakumbuka kuna kipindi aliugua ikabidi apelekwe India kwa matibabu ya moyo,fedha za matibabu na usafiri alilipiwa na Mheshimiwa B Mkapa.Baada ya safari ya India Sheikh Yahaya Hussein hakuwa yule tuliyemzoea bali alikuwa mganga njaa zaidi.Mfano aliwatisha wanaCCM watakao mpinga Kikwete atakufa,ukiangalia kwa makini utagundua Sheikh alikuwa akijikomba kwa Rais Kikwete.Mfano mwingine ni kujitolea kutoa ulinzi usionekana kwa Rais Kikwete.Kifupi njaa ilimfanya Sheikh Yahaya Hussein abwabwaje chochote mbele ya wenye fedha na madaraka.