Sitakaa nimsifu mchawi. Yahya hatokumbukwa kwa mazuri si Tz Si ulimwenguni. Wale wote wanaoutafuta nyadhifa au urais ama kwa kuua ngamia au wale wa kulindwa na mashetani ya Yahya sitegemei kuwakuta mbinguni! Unajimu na utabiri na uchawi ni vitu vitatu tofauti kabisa. Uchawi wa nyota na matukio ya kufa watu kama mchawi marehemu Yahya Hussein alivokuwa ni ushetani. Sikatai kuwa kuna watu watampenda na kumkosa mchawi uyu kwa kuwa muda wake umeisha hapa duniani,ila siwaungi mkono kwa kuwa kila mtu ana mtazamo wake. Nakumbuka mwaka 2004 Yahya alitabiri taifa kumpata rais mwanamke,hapa alicheza pata potea akitegemea mama wa umoja wa mataifa kurudi Tz kuchukua fomu iliposhindikana wakati wa kampeni2005 akadai watampata waziri mkuu mwanamke,pia mama akuweza kurudi kupata ubunge,wala uwaziri,mama uyo hatimaye karud2010 na kuambulia uwaziri tu. Uyu mchawi mkuu Yahya alipoulizwa akasema eti yeye alimaanisha kuwa atatokea rais mzuri mwenye sura na mvuto wa kike! Hapa niliona kama tusi kwa mh.rais jakaya,isiwe tabu,yahya si mfano wa kuigwa. Watu wanasema eti yahya alikuwa amesomea,kwani uchawi hausomewi huko afrika ya kati na ya magharibi? Hapana,simwombei mtu kufa ila ntasema kama alivosema rais jk kwa kifo cha osama,yahya kafa,mioyo ya watu itatulia. Nijuavyo mimi hata ktk agano la kale Mungu aliwakataza watu kuwapindua ktk uongozi wateule wake,lakini ilipotokea Mungu aliwanyima upeo wa kutawala au hata kuwaamuru watubu kwa kumpindua mteule wake! Lakini mchawi Yahya akasema,atakayechukua fomu kumpinga Jk atakufa! Akasema kati ya wagombea urais atakufa,wote ni wacha Mungu,hamna aliyekufa! Kwa kuwa hakutoa timeframe ya tukio ilo,tumesubiri weee mpaka sasa ile sala aliyowaombea wenzie wafe imejibiwa ila sasa anwani haikuwa ya mgombea,majibu yametumwa moja kwa moja kwenye address ya mwombaji. Unajimu wa kisayansi ambao wengi tumeupitia ni ule wa kubashiri matukio yaliyokwisha kujitokeza na kujirudia/seasonal forecasting,japo pia kuna seasonal variations. Ila si uchawi wa nani atakufa nani ataishi milele. Yahya alikuwa mwakilishi wa watu wasio na Mungu,pia siwezi kumuita sheikh kwa kuwa najua fika maana ya kuitwa Sheikh! Japo ninajua anuani ya nilipo,ila sitasema maana ni aina ya ulimbukeni,sori kwa yeyote atakaedhania namsema maana huo ndo ukweli. Mwisho namshukuru mleta mada mr.William wa New York.USA kwa kuleta mada tuijadili. Siku njema.