Wakuu wote JF, heshima mbele sana:-
- Kifo cha Sheikh Yahaya jana, kimetushitua wananchi wengi sana hasa wale tuliomzoea toka enzi za Utawala wa Awamu Ya Kwanza, I mean you wanted to ignore the guy lakini he was all over the map coming from Kenya, enzi hizo kwenye mabazeti ya Taifa na Baraza, ambayo kuwa nayo Tanzania ilikuwa ni very luxurious.
- Ninakumbuka ukiyaona hayo magazeti, hasa kwa kuomba kwa waliokuwa nayo, the first thing you wanted ilikuwa ni kukimbilia kwenye ukurasa wa Nyota na Utabiri wa Sheikh Yahaya, as opposed na miaka ya karibuni na hadi kuelekea kutangulia kwake kwenye haki.
- Ni muhimu wana-hisstoria wa taifa hili wakampa nafasi Marehemu, of his role either positive au negative katika maisha ya wananchi hasa enzi za Cold War: Je Historia imuhukumu vipi ndugu zangu?
William @ NYC, USA.
Ni kweli Marehemu alikuwa mtu mwenye umaharufu wake, si enzi ya awamu ya kwanza tu, ila awamu zote za Urais wa nchi hii.
Kusema kweli kwa habari ambazo mimi nazijuwa, Mrehemu Yahaya Hussein, si kuwa alikuwa mtabiri tu, aliyekuwa na sifa mbali mbali ndani na nje ya nchi ya Tanzania, pia alikuwa ni mfanyakazi wa serikali, ukipenda unaweza kumuita shushu.
Uko Kenya ambako alikwenda, si kwa ajili ya mambo ya utabiri peke yake, bali ilikuwa ni mbinu mojawapo ya yeye kuweza kufunguliwa ofisi ili haweze kufanyakazi ya ushushu bila ya kushtukiwa, na uku akiwa kwenye undercover ya utabiri. Nadhani Kenya walipopata hizo tetesi ndio ikawa sababu ya yeye kuondolewa uko.
Kuhusu kazi yake ya Utabiri, kuna watu wenye kumuunga mkono kuwa alichokuwa anakifanya ni sawa na kuna wale ambao kina sisi, tunajuwa kuwa alichokuwa akikifanya si katika imani ya Uislam.
Uislam unapinga ilo jambo kwa nguvu zote.
Uislam unatufahamisha kuwa Mtabiri wa nyota, kusoma viganja vya watu vya mikono na kuwaeleza hivyo wanavyosema ameona, huyu mtu ana tofauti na mpiga ramri.
Na hii ni tofauti na zile tabiri za hali ya hewa ambazo watu wengi wenye kushabikia utabiri wa kinyota, ufananisha nazo.
Watu wengi wameshindwa kutofautisha dini yake na kazi yake ya utabiri, na wachache wnafikiria ndio Uislam unafundisha hayo mambo, na wapo wengine wakamuhusisha na mambo ya majini.
Uislam upo wazi kabisa, wla haujaficha kitu...! Kinachobakia ni mtu, mwenyewe kuchagua wapi pa kukamata.
Tunasoma kwenye Qur'an:
Enyi Mlioamini! Bila shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli ni uchafu katika kazi za shetani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa
Al-Maaida: 90
Na vile vile Mtume Muhammad (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza jambo hilo, hivyo inatakiwa tujiweke kando kabisa.
Mambo yote haya ni haramu na yeyote mwenye kuamini kuwa jambo fulani limetokea kwa sababu ya nyota kadhaa na kadhaa amemkanusha Mwenyezi Mungu kama Alivyosema katika Hadiyth ifuatayo:
Yeyote atakayejimai (kufanya kitendo cha ndoa) na mwanamke mwenye hedhi, au kwa kutumia njia ya nyuma, au kumkaribia mtabiri na kuamini aliyoambiwa, basi amekufuru yale aliyoteremshiwa Muhammad.
[Hadiyth Sahiyh imesimuliwa na AsWhabus-Sunnan na wengineo]
Na kufanya hivyo ni humpeleka mtu kuingia katika shirk. Na Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) humghufuria mtu dhambi zote ila shirk kama Alivyosema:
"
Hakika Mwenyezi Mungu Hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa Amtakaye. Na anayemshirikisha Mwenyezi Mungu basi hakika amezua dhambi kubwa"
An-Nisaa: 48
Tunachotakiwa sisi wengine ni kuangalia kile ambacho tunakiona kinafaa na kuyawacha yale ambayo si katika Uislam.
Na hakuna miongoni mwetu, mwenye kujua kama Marehemu aliomba Toba kwa Mola wake kabla ajafariki au lah au aliwacha madhambi yote na kujuta kwa kila dhambi aliyoifanya, pamoja na kuwa na azma ya kutorudia tena kutenda dhambi hiyo. Hapo ni yeye na Mungu wake ndio wenye kujua na si sisi.
"
Al-Ladhīna 'Idhā 'Aşābat' hum Muşībatun Qālū 'Innā Lillāhi Wa 'Innā 'Ilayhi Rāji`ūna".
Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.
Baqarah: 156