TANZANIA: Historia ya Taifa Letu na Sheikh Yahya (RIP!) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TANZANIA: Historia ya Taifa Letu na Sheikh Yahya (RIP!)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by W. J. Malecela, May 21, 2011.

 1. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #1
  May 21, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  Wakuu wote JF, heshima mbele sana:-

  - Kifo cha Sheikh Yahaya jana, kimetushitua wananchi wengi sana hasa wale tuliomzoea toka enzi za Utawala wa Awamu Ya Kwanza, I mean you wanted to ignore the guy lakini he was all over the map coming from Kenya, enzi hizo kwenye mabazeti ya Taifa na Baraza, ambayo kuwa nayo Tanzania ilikuwa ni very luxurious.

  - Ninakumbuka ukiyaona hayo magazeti, hasa kwa kuomba kwa waliokuwa nayo, the first thing you wanted ilikuwa ni kukimbilia kwenye ukurasa wa Nyota na Utabiri wa Sheikh Yahaya, as opposed na miaka ya karibuni na hadi kuelekea kutangulia kwake kwenye haki.

  - Ni muhimu wana-hisstoria wa taifa hili wakampa nafasi Marehemu, of his role either positive au negative katika maisha ya wananchi hasa enzi za Cold War: Je Historia imuhukumu vipi ndugu zangu?


  William @ NYC, USA.
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  May 21, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  W. J. William,
  Mkuu wangu navyofahamu mimi Sheikh Yahya alikuwa Mnajimu, ni elimu ya nyota ambayo inatolewa na sisi kwa Udanganyika wetu huita Uchawi. Lakini hata hivyo dini zetu zote kama sikosei zinapingana na Unajimu isipokuwa ule uliotabiriwa na mitume..Hivyo kupiga bao na ramli ni haramu na tunapotumia dini zetu kumhukumu inatuweka hata sii mahala pabaya hasa tunapowasikiliza wanajimu wakituambia hali za hewa na kadhalika maana hii ni sayansi na inaaminika matukio mengi duniani huwa yamekwisha andikwa kutokea hivyo alama zake zipo..

  Hivyo basi tunapomtazama Sheikh Yahya kwa jicho la imani ya dini huyu ni mkosa na hatuwezi kumhukumu sisi isipokuwa Mola aliyemuumba. Sindivyo dini zinatuamrisha?.. lakini maajabu ya Mungu hapa JF kuna watu wanajifanya wana dini ile mbaya lakini ndio wa kwanza kuhukumu..

  Kila binadamu ana mapungufu yake na hakika ukimchambua Sheikh Yahya alikuwa anatisha na aliweza kuitumia elimu yake kujinufaisha kimaisha pamoja na kwamba watu wengi walimwona akivuka mipaka ya unajimu na kuingia ktk kundi la wachawi haswa..Yote haya ni ktk kujifunza kwetu kwani wasingekuwepo watu kama Sheikh Yahya wacha Mungu lakini wana mapungufu hata ktk imani zao, sisi maamuma tungekuwa kundi gani!..Sii ndio tungeamini wapo Miungu watu?
  Sii wacha Mungu wote hutenda mema , bali watenda mema ndio wacha Mungu!
   
 3. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #3
  May 21, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Mkuu Bob, sawa sawa sana mimi sasa hivi namuona Sheikh Yahaya RIP Mnajimu representing a hope kwa wananchi wengi wanyonge nje ya the life system tuliyokuwa nayo under siasa za Utawala wa Awamu wa kwanza, infact kune recorded facts kwamba watwala wa wa Awamu ya kwanza hawakumtaka kabisa hapa nchini ndio maana alikuwa akiishi kama mkimbizi Kenya, na alirudi pale tulipobadili siasa zetu, ndio maana ninasema kwamba Nationally he was very influencial in his own way, infact ingekua nchi za wenzetu angeweza hata kuwa a National hero, even though matokeo ya utabiri wake siku zote ulikuwa debatable, lakini huwezi kukataa au ku-igonre his infulencial socially kwa taifa.

  William @ NYC, USA.
   
 4. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #4
  May 21, 2011
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Peleka kwenye thread mama, hii thread haina chochote cha ziada zaidi ya huyu bwana @NYC,USA kujikweza tu!
   
 5. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #5
  May 21, 2011
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Una maana anajikweza kwa kumnunulia pombe na kujikomba komba kwa Professor, ili ambebe kwenye kamati ya kulazimishwa na balozi? ha! ha! ha! ha! ha! aghrrrrrrrrr! kweli akili ni mali sana kwa wenye nazo!

  - Na kutuma e-mails mpaka saa tisa usiku ha! ha! ha! ha!

  Es!
   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  May 21, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu sii vizuri kuwa negative kwa kila jambo maadam kaandika William. Kule kwenye mada mama wanazungumzia kifo chake na nadhani nia ya Wiliam ni kumjadili zaidi kwa mapana nje ya salaam, rambirambi, matusi na hata kukejeri dini na waumini wake...Na kama ujuavyo ukijumuika na vichaa kubishana, wangine hawataelewa nani kichaa ila watapenda kumjua nani kichaa zaidi kuwashinda wenzake..
   
 7. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #7
  May 21, 2011
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Change ID within a fraction! unajiona ndiyo ujanja. Nilishasema kuwa IQ yako iliacha kukua tangu 2000. Umekuwa ukikuwa mwili tu, wanaokujua watakuwa wananigonge thanks kibao.

  Mimi nimesema kuwa Thread yako ni kuweka tu mishikaki ya issue moja humu, wewe unakuja na ID nyingine macho yamekutoka. MIMi sijikombi kwa mtu yoyote yule!
   
 8. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #8
  May 21, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Wacha uwongo, Kama kawaida yako unajaribu kuhusisha kuishi kwa Sheikh Yahya mjini Nairobi na awamu ya kwanza, pole sana kwani hujui kitu kuhusu historia ya huyo mchawi na tapeli. Sheikh Yahya alifungwa Kenya kwa vitendo vya uchawi, utapeli na kuhusika katika wizi akiwa Nairobi na alipoachiwa alipigwa marufuku asikanyage tena Kenya. Nchini Tanzania kuna watu kweli walitegema kuutumia unajimu wake na udanganyika wa Watanzania kupata madaraka lakini hawakufanikiwa, pole yao.
   
 9. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #9
  May 21, 2011
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Bob usipoteze muda wako na huyo mtu mana tunaomuelewa huwa tunampuuza na kumuuzia taarabu zake mwenye maana yeye mwenyewe huwa siku zote yuko kwenye glasi, lakini anapenda sana kujikweza kweza kwa kurusha mawe kwenye vioo, dawa ni kumjibu lugha anayoipenda na kuijua zaidi yaani ya ngonjera na utapeli tapeli!

  Es!
   
 10. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #10
  May 21, 2011
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Lahaula lakwata! ha! ha! ha! ha! ha! hujikombi kwa mtu yoyote? ha! ha! ha! ha! mshikaki kama ile uliyoipora Canada na zile hela za gari? ha! ha! ha! ha! eti kumbe unajua hata maana ya IQ? Nayo ni kujikomba komba kwa watu suifanana nao ili ujikweze na kutuma e-mails mpaka saa tisa asubuhi1 ha! ha! ha! IQ yako kubwa sana mkuu!


  Es!
   
 11. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #11
  May 21, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Pole sana Mwalimu, kama kawaida yako ikishaguswa Awamu ya kwanza ni lazima uje na mapovu, nenda kule kwenye facebook yangu uone Balozi wetu mmoja aliyeko nje alivyo-comment kuhusu Sheikh Yahya na Awamu ya kwanza, kwamba walimfukuza kwa sababu angekwua kikwazo kwa siasa za the times! sio mimi mkuu wanajua zaidi ndio wamesema, ameishi maisha yake yote Kenya, mimi nimeshinda sana kwenye banda lake Uwanja wa Maonyesho ya Saba Saba enzi hizo, anatuonyesha Video za Super Mazembe na Mfuweni Lipua Lipua, alikuwa akitokea Kenya, infact he had a Porshe!

  - Sasa magazeti ya Kenya yaliyokuwa yakiheshimiwa sana wakati ule yaliwezaje kuweka articles za mwizi na mtapeli, I mean mkuu zile mambo ya Awamu ya kwanza ya zidumu fikra za other imperfect human beings ziliisha sasa tuko huru kufikiri na kuchambua facts!


  William @ NYC, USA
   
 12. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #12
  May 21, 2011
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu nimekuelewa, ila inabidi kupambana huko huko kama tunavyofanya sisi wote, hao MOD wakiona tu thread inayofanana wanabanaisha na ndiyo utaratibu . Ona sasa alivyokuja baada ya hilo ombi au kosa langu kumwita @NYC/ si yeye ndiyo anavyotaka? Alikpokuwa anakaa majumba sita au Kigoma mbona alikuwa haweki @Majumba sita sasa kulikoni?
   
 13. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #13
  May 21, 2011
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Umeandika nini sasa, nikisema IQ yako imeacha kukua kuna mtu wa kukutetea?
   
 14. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #14
  May 21, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Nadhani Marehemu alikuwa ana namna ya pekee ya kutoa "motivation" kwa watu. Binafsi sitasahau siku mojja niliangalia kipindi chake kwenye TV akitoa maelezo na "kumotivate" nini taifa starr ilitakiwa kufanya ili wawashinde Senegal teh teh the. baada ya kusikia akitaja taifa star ilibidi ningalie kipindi chote

  Nadhani mchango wake japo kuanzia sasa ni histoiria upo kama mchango wa babu samunje wa Loliondo. Japo kuna tofauti but kuna positive and negative  BTN

  jamani hii sio thread ya kisiasa tafuta jukwaa linalofaa.
   
 15. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #15
  May 21, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Nimeishi sehemu nyingi sana, Sitakishari alikua anaishi mama yangu na mimi sasa hizi nimejenga nyumba yangu huko Kinyerezi, Kigoma nilikuwa training melini MV Tanganyika na Mwongozo, pia nimeishi Mahenge, Mbeya, Arusha, Dodoma, Tanga, Belgium, Hong Kong, Shangai, na sasa New York City.

  - Isipokuwa all this times hakukuwa na mtandao ungekuwepo ningesema nilpo bila uoga, maana kujficha ficha sio tabia yangu!


  William @ NYC, USA.
   
 16. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #16
  May 21, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kwa mwenye imani ya mizuka ni dhahiri atamwimbia nyimbo nyingi, lakini kwa mwenye kumwona kama mtishaji na mdhalilishaji wa saikolojia tutamwona kama ni mtu aliyependa kutumia njia za gizani ili kujenga jina na maisha yamwendee vema badala ya njia ya mwana ambayo wenye imani ya mola wanaiendea.
   
 17. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #17
  May 21, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Unaonekana huna stability katika maisha yako, na huoni sehemu ukatulia, na usipoamua kutulia mahali utabaki kuhangaika maisha yote kwenda nchi baada ya nchi na hutaikuta nchi ambayo ni zaidi ya ulizopita ila tu kuamua kutulia.
   
 18. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #18
  May 21, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Wanaume tumeumbwa kutafuta maisha, huko kote nilikuwa natafuta maisha, nikaishia kuyapata hapa New york City, ambako nimeishi since 1987 na toka 1988 ninafanya kazi kwenye kampuni moja mpaka leo, nikitoka hapa ninarudi bongo home Kinyerezi kwenye kibanda changu nilichojenga kwa jasho langu, so angalia tena maneno yako kama yako sawa, samahani kwa kutoka nje ya mada ila ni vyem kurekebishana mtu anapokuwa hajui anachosema!

  William @ NYC, USA.
   
 19. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #19
  May 21, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Well, huu ni mtizamo wako na ndio maana ya Demokrasia kila mwananchi kuona apendavyo bila kuvunja sheria!

  william @ NYC, USA
   
 20. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #20
  May 21, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Wasifu Mfupi wa marehemu Sheikh Yahaya Hussein

  Mdogo wa marehemu Sheikh Yahya Hussein bwana Abdallah Juma amesema kuwa kaka yake:

  • Alizaliwa miaka 89 iliyopita katika mtaa wa Mkunguni Kipande, Kariakoo, Dar es Salaam.
  • Kabila lake likiwa ni Mmanyema, mwenyeji wa Kigoma.
  • Alisoma shule ya kati ya Uhuru, Dar es Salaam kabla ya kuhamishiwa Zanzibar kwa Sheikh Abdallah Saleh Farqy, alikojifunza Kurani na baadae kwenda nchini Misri na kujiunga na Chuo cha Al Adhar cha Cairo.
  • Alikuwa mwalimu wa Kurani, kwa kuisoma na kuifundisha.
  • Alianza kuupata umaarufu tangu alipokuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Waislamu wa Afrika Mashariki katika miaka ya 1950.
  • Alianza masuala ya unajimu na utabiri wa nyota mwanzoni mwa miaka ya 1960.

  Kuhusu kifo chake, mtoto wa marehemu aitwaye, Hussein Yahya, alisema baba yake:

  • Alifariki dunia jana saa tano asubuhi, baada ya kusumbuliwa na maradhi ya moyo kwa muda wa miaka miwili.
  • Alifariki dunia akiwa katika Hospitali ya Mount Ukombozi, Kinondoni ambapo alipelekwa jana asubuhi kwa matibabu baada ya hali yake kuwa mbaya.
  • Mwili wa marehemu ulihifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo.
  • Awali, dua ya kumwombea marehemu ilipangwa kufanyika katika Msikiti wa Tambaza majira saa 4 adhuhuri lakini taarifa iliyosomwa na TBC saa 7 mchana imesema dua hiyo itafanyika katika msikiti wa Manyema uliopo Kariakoo.
  • Maziko yake yatafanyika leo saa saba mchana katika makaburi ya Tambaza.
  • Ameacha mjane, watoto 15 na wajukuu kadhaa.
  • Hadi alipofariki jana alikuwa na ofisi mjini London, Uingereza, Nairobi, Kenya, Botswana, Swaziland na Tanzania, za kazi zake alizokuwa akifanya enzi za uhai wake.

  source: Wavuti - Habari

  Rest in Peace
   
Loading...