TANTRADE yapokea vizimba vya mabanda ya kisasa kwa ajili ya maonesho ya 47 ya biashara ya kimataifa ya Dar es salaam (Sabasaba)

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
TANTRADE yapokea vizimba vya mabanda ya kisasa kwa ajili ya maonesho ya 47 ya biashara ya kimataifa ya Dar es salaam (sabasaba)

Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya maendeleo ya biashara Tanzania (TANTRADE) Bi. Latifa Khamis leo tarehe 22 Juni, 2023 amepokea udhamini wa viti, meza na vizimba 170 vya mabanda ya maonesho vyenye thamani ya shilingi milioni 300 kutoka kwa kampuni ya manunuzi ya nchini chini ya East Africa Commercial and Logistic Center ambao pia ni wadhamini wakuu wa maonesho ya 47 ya biashara ya kimataifa ya Dar es salaam (Sabasaba).

Akizungumza katika makabidhiano ya vifaa hivyo mkurugenzi mkuu wa TANTRADE Bi. Latifa Khamis amesema TANTRADE imewaza kuokoa fedha zaidi ya shilingi milioni 100 zilizokuwa zinatumika kukodisha vifaa hivyo ili kukidhi mahitaji ya washiriki katika maonesho hayo.

IMG-20230623-WA0043.jpg
IMG-20230623-WA0042.jpg

 
Seems like Bongo has started building the long due Kilimanjaro towers in Upperhill…. We thank you for your kind investment…. You surely know to put your money where rate of return in very high…😄😄
C7866456-9DA8-404F-A40E-7AF100C27FC8.jpeg
 
Back
Top Bottom