TANTRADE na Ubalozi wa Hispania wakutana kuangalia fursa mbalimbali za biashara

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
TANTRADE NA UBALOZI WA HISPANIA WAKUTANA KUANGALIA FURSA MBALIMBALI ZA BIASHARA
_________
24 Mei, 2023
Dar es Salaam

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Ukuzaji Biashara - Bw. Fortunatus Mhambe, Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Biashara - Bw. Fredy Liundi na Afisa Biashara - Bi. Samira Mohamed wametembelea Balozi wa Hispania nchini Tanzania Balozi Jorge Moragas.

Mhe.Balozi alikuwa na Watumishi wawili wa Ubalozi ambao Ana Mendez-Abascal Fernandez, Mkuu wa Idara ya Uchumi na Biashara na José Ramos Afisa anayehusika na Biashara.

Lengo kuu la mazungumzo hayo lilikuwa ni kuangalia namna ya kuboresha mahusiano na mashirikiano l ya kibiashara baina ya Hispania na Tanzania.

Aidha, TanTrade ilitumia fursa hiyo kuhamasisha ushiriki wa kampuni za Hispania katika sekta mbalimbali kushiriki katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 28 Juni - 13 Julai, 2023 katika Uwanja wa Maonesho wa Mwl. J. K Nyerere, Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam.

Balozi huyo aliihakikishia TanTrade kwamba mwaka huu kampuni za sekta binafsi zitashiriki ili kutangaza bidhaa zinazozalishwa na kampuni hizo zilizopo nchini Tanzania.

Naye Bi. Ana Fernandez, Afisa Mkuu wa Uchumi na Biashara, ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuboresha Sekta ya Uwekezaji na kuvutia kampuni nyingi zaidi kutoka nchi mbalimbali duniani ikiwemo Hispania kuja kuwekeza nchini Tanzania.

IMG-20230524-WA0196(1).jpg
IMG-20230524-WA0194(2).jpg
IMG-20230524-WA0193(2).jpg
 
Back
Top Bottom