Tangazo: Wanaohitaji mtu wa kusimamia ujenzi wa nyumba, mtu wa uhakika muaminifu anapatikana

Ruble

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
620
1,038
Wakuu heshima kwenu.

Kuna watu wako busy kwenye kazi, wengine hawajui kusimamia nyumba kwa maana ndio ujenzi wa kwanza labda.

Sasa ondoa shaka mtaalamu kijana wa kiha muaminifu anapatikana. Ni rafiki yangu wa karibu kaomba nimtangazie humu. Ana uzoefu wa kusimamia mafundi wakiwa wanajenga ili asiibiwe na pia kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa.

Ni kijana muaminifu. Ana uzoefu wa kusimamia nyumba za mabosi Kigamboni. Anapatikana Dar Kigamboni. Ni muaminifu, anajua kutumia pikipiki japo hana leseni.

Kama kuna mtu anataka mtu muaminifu asiye na konakona wa kumtuma na kusimamia nyumba au ujenzi wa mabanda, boma la mifugo au ujenzi wowote ule unaohitaji usimamizi kuondoa usumbufu na usanii wa mafundi basi yeye yupo.

Namba yake 0716389999. Karibuni kwa huduma ya uaminifu.
 
Back
Top Bottom