Tanga: Idadi ya Wanawake waliopata huduma ya uzazi wa mpango kwa njia ya kisasa imepanda kutoka 40% hadi 59% Muheza

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
1.JPG

Elimu inayotolewa kwa makundi ya vijana Wilaya ya Muheza Mkoa wa Tanga imechangia kupunguza idadi ya mimba za chini ya umri wa miaka 19 (mimba za utotoni).

Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni zilizotolewa na Mratibu wa Afya ya Mzazi na Mtoto Wilaya ya Muheza, Angelina Sengwaji anaeleza kuwa Mwaka 2021 idadi ya mimba ilikuwa ni 808, Mwaka 2022 ni 717.

Angelina anasema “Takwimu hizo zinahusisha pia walioolewa, maana wapo kuna wengine wameishia darasa la saba wakaolewa lakini yupo under 18. Januari hadi Machi 2023 idadi ya mimba ni 159 kwa Watoto wenye umri chini ya miaka 18.”

Awali, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maendeleo ya uzazi wa mpango ofisini kwake Muheza hivi karibuni, Angelina alisema: “Mimi kama mratibu kutokana na ushirikiano wa Wadau, Serikali na Halmashauri katika utoaji wa huduma ya uzazi wa mpango na huduma ya Afya ya Uzazi kwa ujumla, tumeona mabadiliko mengi ambayo tumeyapata kutokana na ushirikiano huo.

“Kwanza uwezekano wa kuweza kufanya Huduma Mkoba sisi kama Halmashauri, wakati mwingine tunashindwa lakini Wadau wanatuisaidia kufanya Huduma Mkoba (Outreach) ambapo tunaweza kuwafikia wateja wengine wanaohitaji huduma kutoka maeneo ya mbali.

“Nasema hivyo kwa kuwa kuna maeneo mengine hakuna Zahanati na kuna makazi ya watu, nao wanahitaji huduma.

“Kwa mfano katika Halmashauri yetu ya Wilaya ya Muheza kuna maeneo yapo pembezoni mwa mji, ukiwa Zirai kuna vijiji vipo huko vinaitwa Antakaye na Kwinzitu, huko hakuna Zahanati lakini kutokana na ushirikiano wa Wadau wa Huduma Mkoba wateja na wananchi wa kule wanaweza kufaidika na huduma mbalimbali zinazotolewa na wadau kwa kushirikiana na Halmashauri ikiwemo huduma rafiki kwa vijana.

Vijana wamepata elimu ya masuala ya afya ya uzazi na wananchi kwa ujumla, jamii imeweza kupata elimu imeweza kutumia huduma hizo na sasa hivi kwa kweli wanafurahia kwa sababu malengo yao yametimia.
2.JPG

Angelina anasema Mwaka 2022 idadi ya kina mama waliopata huduma ya uzazi wa mpango kwa njia za muda mrefu na muda mfupi lakini kwa ujumla njia za kisasa tofauti na njia za asili imepanda kutoka 40% (2021) hadi 59% (2022).

Hiyo idadi ya wateja wanaotumia njia za uzazi wa mpango ni moja ya viashiria ambavyo vinapimwa katika utoaji wa huduma kutokana ma idadi ya wateja wanaotumia njia za uzazi wa mpango, huduma ya afya ya uzazi kwa ujumla.

Angelina anaeleza kuwa vijana wanapata taarifa sahihi juu ya afya ya uzazi, anasema: “Katika Halmashauri ya Wilaya ya Muheza tunazo klabu ambazo zinaelimisha vijana walioko katika kundi la balehe walioko Shule za Msingi, Sekondari na wengine walioko vyuoni.

“Hizo klabu tunazo katika vituo vyetu vitatu, Muheza DDH, Ubwari Health Centre (kituo cha afya) pia na Mkuzi, bado tunaendelea tunataka hiyo huduma iweze kusambaa katika vituo vyote lakini kwa jamii kwa jumla tunazo pia Huduma Mkoba ambazo tunazitoa katika shule zetu, tunakwenda kutoa elimu shuleni.

“Pia kuwapatia mabinti chanjo ya kuzuia mlango wa Saratani baada ya kuwapa elimu na kuelewa na wazazi wao wakakubaliana.
3.JPG

“Kwa hiyo vijana wanapata huduma ya afya ya uzazi kupitia Huduma Mkoba lakini pia wanapokuja vituoni watoa huduma wanawapa ushirikiano hakuna mtoa huduma ambaye atamshangaa kijana kwa kuja kupatiwa huduma hizo, anapewa ushirikiano lakini pia tunazo kliniki zinafanyika wikiendi (mapumziko ya wiki-Jumamosi) wanafunzi wanakuwa mapumziko.

“Tuna klabu za vijana wanapata huduma ya afya ya uzazi, elimu lakini pia wanapata huduma matunzo wale ambao wanaishi na maambukizi ya VVU, kwa hiyo tuna special clinic (kliniki maalum), ambazo zinafanyika siku ya Jumamosi.

“Kliniki hizo katika Wilaya ya Muheza tunazo 15 ambapo wanapokuja kliniki wanapata pia elimu ya afya ya uzazi,” anasema Angelina.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Zahanati ya Nkumba, Muheza Josiah Nyange ambaye ni mtoa huduma Taasisi ya Marie Stopes Muheza anasema wameweza kutoa Huduma ya Mkoba kwa jamii na makundi yote katika maeneo ambayo hayafikiki kwa urahisi.
4.JPG

“Makadirio kwa siku tunawaona na kutoa huduma kwa Wanawake 100 mpaka 150, kwa upande wa vijana tunatoa. Tunapata ushirikiano mzuri kutoka kwa Mganga Mkuu wa Mkoa na pia katibu tawala, kila mwaka tunashiriki vikao vya wadau.

“Mapokeo ya huduma kwa jumla ni mazuri kuna baadhi ya maeneo jamii ilikuwa haikubali lakini baada ya kutoa elimu, imeelewa na inapokea huduma,” anasema Nyange.

Akizungumza na waandishi wa habari akiwa Zahanati ya Zirai, Amani Muheza, Mtalaam wa Uzazi wa Mpango Yunus Mnnduma (Marie Stopes) alisema faida ya kutumia uzazi wa mpango ni pamoja na mama kuimarika kiafya, mtoto kukua vizuri pamoja na kupatiwa huduma stahiki ya malezi na elimu.


Chanzo: Mary Victor
 
Wangejua wanajitafutia kansa wasingekubali kuwekewa njiti na bla bla za uzazi wa mpango
 
Back
Top Bottom