Kwanini, Simiyu, Kigoma, Mara, Geita na Pemba hawatumii Uzazi wa Mpango Kama Mbeya na Iringa?

Jul 30, 2013
96
36
Katika ripoti ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2022 ya Wizara ya Afya Dodoma kushirikiana na Wizara ya Afya Zanzibar, Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dodoma, Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar, iliyotoka Januari 2023, INaonesha Kuna Mikoa kabisa haina Uelewa kuhusu Uzazi wa Mpango.

Kiwango cha upatikanaji wa njia za uzazi wa mpango

Asilimia ya wanawake wanaotumia njia yoyote ya uzazi wa mpango.
Sampuli: Wanawake wenye umri wa miaka 15-49 ambao kwa sasa wako kwenye ndoa na wanawake wenye umri wa miaka 15-49 ambao kwa sasa hawako kwenye ndoa lakini wanajamiiana

Njia za Kisasa za Uzazi wa Mpango

Inajumuisha kufunga kizazi kwa mwanamme na mwanamke, sindano, kitanzi (IUDs), vidonge, vipandikizi, kondomu ya kike na kondomu ya kiume, njia ya dharura, njia ya kalenda na njia ya kunyonyesha.

Jedwali Na. 6 linaonesha matumizi ya njia za uzazi wa mpango kati ya wanawake walioolewa hivi sasa na wasioolewa lakini wanashiriki tendo la kujamiiana.

Asilimia 38 ya wanawake walioolewa kwa sasa wanatumia njia yoyote ya uzazi wa mpango, ikijumuisha asilimia 31 ya wanaotumia njia zozote za kisasa na asilimia 7 ya wanawake wanaotumia njia za asili za uzazi wa mpango
Njia ya vipandikizi ndiyo njia inayotumika zaidi miongoni mwa wanawake walioolewa (asilimia 14), ikifuatiwa na njia ya sindano (asilimia 9).

Miongoni mwa wanawake wasioolewa lakini wanashiriki tendo la kujamiiana, asilimia 45 hutumia njia yoyote ya uzazi wa mpango, ikiwa ni pamoja na asilimia 36 kutumia njia yoyote ya kisasa na asilimia 8 kutumia njia yoyote ya asili

Jedwali Na. 6: Matumizi ya sasa ya njia za uzazi wa mpango kulingana na sifa bainifu Mgawanyo kwa asilimia ya wanawake walioolewa kwa sasa na wasioolewa lakini wanashiriki tendo la kujamiiana wenye umri wa miaka 15-49, kwa njia za uzazi wa mpango inayotumika sasa, kulingana na sifa bainifui, Tanzania DHS-MIS 2022
TB1.png
TB2.png
TB3.png
TB4.png
TB5.png
TB6.png

Angalizo: Ikiwa zaidi ya njia moja inatumiwa, ni njia bora zaidi pekee inayozingatiwa katika jedwali hili.
SDM = Njia ya Shanga
LAM = Njia ya Kunyonyeshal
1 wasioolewa lakini walishiriki tendo la kujamiianandani ya siku 30 kabla ya Utafiti​
Mwenendo: Miongoni mwa wanawake walioolewa, matumizi ya njia yoyote ya kisasa ya uzazi wa mpango ni takriban sawa na iliyoripotiwa katika utafiti wa TDHS-MIS wa mwaka 2015–16. Ingawa, miongoni mwa ya wanawake wasioolewa lakini wanashiriki tendo la kujamiiana, matumizi ya njia yoyote ya kisasa yamepungua kutoka asilimia 46 kwa TDHS-MIS ya mwaka 2015-16 hadi asilimia 36 kwa TDHS-MIS ya mwaka 2022.

Ramani 1: Matumizi ya njia za uzazi wa mpango kimkoa

Asilimia ya wanawake wenye umri wa miaka 15-49 ambao kwa sasa wanatumia njia yoyote ya uzazi wa mpango
RMN.png

Mikoa ya Njombe, Mbeya, Iringa, Songwe, Lindi Wanafanya vizuri kutumia Uzazi wa Mpango. Wakati Njombe asilimia 64 ya Wanawake wanatumia aina yoyote ya Uzazi wa mpango, Simiyu ni asilimia 11 tu ndio wanatumia aina yoyote ya Uzazi wa Mpango. Mikoa mingine inaonesha kuwa na idadi ndogo ya wanaotumia Uzazi wa mpango ni ni pamoja na Tabora, Geita, Katavi, Mara, Shinyanga nk.

Serikali inabidi ingilie kati kuangalia tatizo ni nini.
 
Back
Top Bottom