JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,308
- 5,460
Watu sita wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya gari aina ya Fuso lenye namba za usajili T 239 AFB walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kutumbukia kwenye korongo katika eneo la barabara ya Soni/Mombo wilayani Lushoto mkoani Tanga.
RPC wa Tanga, Safia Jongo amesema ajali hiyo imetokea asubuhi ya leo Jumanne Machi 29, 2022.
Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Lushoto na majeruhi wapo Hospitalini hapo wakiendelea kupata matibabu.
RPC Jongo ametoa wito kwa watumiaji wa vyombo vya moto mkoani humo kuendelea kufuata sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani.
Chanzo: MillardAyo