TANESCO yautaja umeme wa gesi kama 'umeme wa gharama'

Bidhaa zetu haziwezi kushindana na siko la nje kama tutaendwlea kuj8kita kwenye uzalishaji kwa ghalama kubwa ya umeme.
Hapana kuna mbinu zingine mfano kuondoa kodi kadhaa kwa kampuni ambazo zinaongeza thamani ya bidhaa kwa ajili ya kuuza nje. Na ndio uwepo wa EPZA upo kwa ajili hiyo, so issue sio umeme tu kma kuna kodi zingine zitaondolewa bado tunabaki competitive.

Kuna nchi kibao tu zinatoa export subsidies kwa kigezo cha Green Box!! So tunaweza kutumia hiyo kushusha bei za bidhaa zetu, maana siamini umeme ndio kila kitu.
 
Duuuu lazima tuchanganyikiwe mwaka huu yani hii wizara kila mtu msemaji na ni kambale...
Hii wizara ameingia mjuaji na amekutana na wajuaji. Ngoja tuone itaishia wapi. Ila kuna mtu atasalimu amri muda sio mrefu.
Ni ukweli usiofichika kwamba thermal power plants are more expensive than hydro ones. The best option is to mix the two in a certain prudent propotional.

Nishati lazima mtu mzalendo na muelewa akae pale. Dr. Tito Mwinuka sijui kwanini wamemuondoa maana alikuwa anafaa sana kwenye kiti kile kwa jinsi alivyo
 
Elimu hapa, gesi ni mafuta yaliyo kwenye hali ya kimiminika.

Kama umeme wa mafuta ni gharama na gesi nao ni gharama vile vile kwakua vyanzo vinafanana, tofauti ni wingi wa nishati kwa ujazo unaofanana (volume in cubic metres)
Dangote kwa sasa Malori yake yanashifti from mafuta kwenda gas na hapo unasema?
 
Elimu hapa, gesi ni mafuta yaliyo kwenye hali ya kimiminika.

Kama umeme wa mafuta ni gharama na gesi nao ni gharama vile vile kwakua vyanzo vinafanana, tofauti ni wingi wa nishati kwa ujazo unaofanana (volume in cubic metres)

..Na mkopo tuliochukua kujenga Stiegler una masharti magumu ya kibiashara, hivyo umeme wa maji nao utakuwa wa bei ghali kufidia gharama za kulipa mkopo.
 
TANESCO katika mpango mkakati wake wa miaka mitano imesema pamoja na kupungua utegemezi wa matumizi ya mafuta mazito kuzalishia umeme, gesi nayo majanga. Gharama ya kufikisha gesi kwenye vituo vya kuzalishia umeme kutoka inapochimbwa inabakisha gharama ya uzalishaji wa umeme kuendelea kuwa juu...
Basi TANESCO wajaribu umeme wa upepo kama umeme wa gesi ni ghali.
 
Sitaki kuamini kama gharama za uchimbaji gesi iliyo chini ya maji baharini zinalingana na gharama za solar au wind.

Ni kitu gani kinachowasukuma wanasiasa kukomaa na umeme wa gas licha ya gharama kubwa iliyopo huko?

Hata kama ni kwa mkopo, wanachotaka wao ni kuhakikisha hayo mapesa watayopata huko wanayachota $30 mil. then wanaenda zao, wakijua fika mzigo wa kulipia hizo gharama hautawahusu wao personally licha ya kutuibia % kadhaa, utakuwa mzigo wa watanzania wote.

Hapa haihitajiki akili yoyote ya ziada kujua wote wanaotaka mradi wa gas uanze wana malengo gani kwa hili taifa, simply wanachojali wao ni kupata hizo pesa nyingine wakwapue wafanyie mambo yao, kama walivyochota 10% kwenye mikataba ya madini
 
Elimu hapa, gesi ni mafuta yaliyo kwenye hali ya kimiminika.

Kama umeme wa mafuta ni gharama na gesi nao ni gharama vile vile kwakua vyanzo vinafanana, tofauti ni wingi wa nishati kwa ujazo unaofanana (volume in cubic metres)
Mafuta unanunua kutoka UARABUNI, Na gesi unaipata kutoka KUSINI kwa NCHI YAKO. Kupanga ni KUCHAGUA.
 
Sitaki kuamini kama gharama za uchimbaji gesi iliyo chini ya maji baharini zinalingana na gharama za solar au wind.

Ni kitu gani kinachowasukuma wanasiasa kukomaa na umeme wa gas licha ya gharama kubwa iliyopo huko?...
UMEWAHI KUFIKA MTWARA AU LINDI??? KAMA GAS NI GHARAMA KWANINI BEI NI SAWA KWA WATU WA KUSINI NA MIKOA MINGINE AMBAYO HAWATUMII UMEME WA GAS?

Tatizo mliaminishwa ujinga sana. We unadhani Prof Muhongo aliokotwa UDSM? Watz tuna ujuaji mwingi sana. Gesi ni chanzo cha uhakika kwa umeme.

Gharama lazima ziwe kubwa kwa mwanzoni lkn wakifika at EP taratibu utaona bei inakuwa ya kawaida sana. Gesi ni rasilimali yetu. Na kama ingekuwa ya kwao kwann wasijenge viwanda wakauza nje wao wenyewe?
 
UMEWAHI KUFIKA MTWARA AU LINDI??? KAMA GAS NI GHARAMA KWANINI BEI NI SAWA KWA WATU WA KUSINI NA MIKOA MINGINE AMBAYA HAWATUMII UMEME WA GAS??
Japo sijakuelewa ulichoandika, kama uchimbaji wa gas usingekuwa wa gharama tusingekuwa tunauziwa kwa bei ya juu, gharama za uchimbaji ndizo zinasababisha bei kuwa juu kwa mtumiaji, ndio maana nataka vyanzo vingine visivyo na gharama kama upepo na jua vitumike.
 
Not necessarily, ukikopa ukajenga nyumba sio lazima atakae kaa kwenye nyumba yako alipe kodi kubwa ili umalize mkopo.

..ukichukua mkopo wenye masharti mabaya lazima utaingia gharama kubwa kuulipa.

..kwenye mfano wako wa nyumba iliyojengwa kwa mkopo, gharama za mkopo itabidi abebe mpangaji, au abebe mwenye nyumba, au wote. It's a choice.
 
UMEWAHI KUFIKA MTWARA AU LINDI??? KAMA GAS NI GHARAMA KWANINI BEI NI SAWA KWA WATU WA KUSINI NA MIKOA MINGINE AMBAYO HAWATUMII UMEME WA GAS??
Tatizo mliaminishwa ujinga sana. We unadhani Prof Muhongo aliokotwa UDSM? Watz tuna ujuaji mwingi sana. Gesi ni chanzo cha uhakika kwa umeme. Gharama lazima ziwe kubwa kwa mwanzoni lkn wakifika at EP taratibu utaona bei inakuwa ya kawaida sana. Gesi ni rasilimali yetu. Na kama ingekuwa ya kwao kwann wasijenge viwanda wakauza nje wao wenyewe?
Hapo kwenye YETU una uhakika ya kwenu? Husiwaone Tanesco na Mwendazake ni wajinga kukimbilia umeme wa maji.
 
Back
Top Bottom