TANESCO wanalazimika kubeba hasara kubwa tunazopata wananchi, kutokana na mgao wao wa umeme, usio na ratiba maalum

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,484
30,162
Hivi sasa siyo tena habari, kuona maeneo kadhaa ya nchi, yakiwa yako gizani, kutokana na mgao wa umeme, ambao ni "endless" bila ya TANESCO kutoa taarifa za mapema, kuwa kutakuwa na mgao wa umeme katika maeneo hayo husika!

Nyinyi watu wa TANESCO hebu jaribuni kufikiria, hizo hasara kubwa mnazotusababishia sisi wananchi, kutokana na kukata kwenu umeme kusiko na ratiba maalum.

Hebu nyinyi watu wa TANESCO, jaribuni kuvaa viatu vyetu sisi wananchi na kufikiria mitaji mingapi ya mabilioni ya pesa, inayoangamia Kila siku, kutokana na kukata kata kwenu umeme, kusiko na ratiba maalum?

Shirika lenu ni la kutoa huduma, hivyo pale ambapo wananchi, haturidhishwi na huduma zenu, sisi wananchi, inatubidi tulalamike.

Kwani mnashindwa nini kutoa ratiba ya ukataji wa umeme katika maeneo husika?

Nyinyi TANESCO mshukuruni sana Mungu, shirika lenu lipo Tanzania, lenye wananchi wasiojua haki zao za msingi na wapole wa kupitiliza.

Mimi naamini kuwa kama shirika lenu, lingekuwa lipo kwenye nchi nyingine, ambako wananchi wake wanajitambua na kuzijua haki zao za msingi wateja, shirika lenu, lingefilisika, kutokana na madai ya wateja wenu, kufidiwa kutokana na uzembe wenu wa kuwakatia umeme, bila ratiba maalum!

Hivi siyo nyinyi TANESCO, mwaka Jana tu, mlikuwa mkituambia sisi wananchi, kuwa mgao wa umeme uliokuwa ukiendelea hapa nchini, unatokana na mabwawa hayo yanayozalisha umeme kukauka?

Sasa Mungu naye kawaheleleza, amemwaga mvua ya El-Nino ya kufa mtu, hadi mabwawa yetu yote yamejaa hadi kutapika!

Msivyo na haya machoni kwenu, mmebadilisha "story" sasa hivi mmekuja na kutueleza kuwa, mgao huu wa umeme, unatokana na miundombinu ya TANESCO kuwa ni chakavu!

Nyinyi TANESCO mmeungana na chama tawala cha CCM, kututesa sisi wananchi, Kwa kutoa ahadi zosizotekelezeka Kila leo za alifu lela ulela, ya kuwa, suala la kukatika umeme, litakuwa historia ndani ya nchi yetu!

Hizo "sound" mmekuwa mkitoa, tokea mimi nasoma shule ya msingi, miaka mingi sana ya nyuma!

Nadhani sisi wananchi tunapaswa sasa kusema, enough is enough, tuwapige chini nyinyi TANESCO na "wabia" wenu wa CCM, katika chaguzi zijazo, kutokana na kuwa nyinyi ni waongo sugu, mnaopenda kutoa matumaini Kwa wananchi, ambayo hayapo!

Nimewasikia mara kadhaa, nyinyi TANESCO mkijigamba kuwa, mradi wa umeme wa Bwawa la Nyerere, ukikamilika, basi hili suala la kukatika katika, umeme katika nchi hii, litakuwa ni suala la historia!

Hiyo siyo ahadi ya kwanza, kutolewa na kiongozi wa CCM, kutokana na kero ya kukatika umeme, kwa kuwa nakumbuka zaidi ya miaka 10 ya nyuma, aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati wa wakati huo, alinukuliwa na vyombo vya habari akinena, kuwa mradi mkubwa wa Bomba la gesi kutoka Mtwara, ukikamilika, basi tuhesabu kuwa mateso yanayotokana na kero ya kukatika Kwa umeme, itakuwa ni historia katika nchi yetu!

Hivyo "vichekesho" tushaanza kuvizoea sisi wananchi kwenye masikio yetu, kutokana na viongozi wetu, kutuona sisi wananchi wa nchi hii ni wajinga na malofa tunaoweza kudanganywa miaka yote!
 
Umeongea kwa uchungu sana ila bahati mbaya watanzania tuna tabia ya kuendana na shida. Matatizo ni sehemu ya fahari yetu mfano watu wajigambavyo, mimi nimetokea familia maskini au nyumbani tulilala njaa sana na muda mwingine tulikula ugali na chumvi , au tumeishi kwa vibatari

Kwa mindset hizi, sijui ni nini kitatokea ila wacha ni waache wafu mzike wafu wengine
 
Inasikitisha sana
 
Tutafanyaje, ukichoka vuka boda, hamia zambia 😁
Yale maneno yaliowahi kutamkwa na Waziri wa Fedha, naweza kusema ni ya mtu aloyelewa madaraka!

Kwa kuwa siamini Kwa kiongozi muadilifu, unaweza kutamka maneno hayo, kisa tu wananchi wametoa malalamiko yao kuhusu uendeshaji wa nchi yetu
 
Taasisi za serikali zatakiwa zijilipe kutokana na faida wanayopata, Iwe kama Kampuni binafsi mapato yakipungua tu wapunguze wafanyakazi
 
Sasa jiulize, inawezekanaje Kwa TANESCO, kuwepo na upungufu wa pesa, kutokana na kupungua Kwa mapato yao kutokana na huo mgao, lakini idadi ya wafanyakazi wao Iko pale pale??
 
Yale maneno yaliowahi kutamkwa na Waziri wa Fedha, naweza kusema ni ya mtu aloyelewa madaraka!

Kwa kuwa siamini Kwa kiongozi muadilifu, unaweza kutamka maneno hayo, kisa tu wananchi wametoa malalamiko yao kuhusu uendeshaji wa nchi yetu
Viongozi waliopo ni reflection ya wananchi tulivyo mkuu 🙏🏽
 
Unataka kusema kuwa sisi wananchi, hatuko "serious" ya mambo yanavyokwenda, ndani ya nchi yetu?😙
 
TANESCO ni uthibitisho wa laana kwa taifa

Back
Top Bottom