Kwa vyanzo hivi vya umeme Serikali na TANESCO mnakwama wapi?

LUS0MYA

JF-Expert Member
Aug 4, 2011
862
1,097
Jaribu kupitia vyanzo vya umeme wa tanesco kama ilivyoambatanishwa na andiko hili ili kujua panapovuja ni wapi.
Vyanzo vikuu ni kutokana na maji na gesi lakini gesi ndiyo inayoongoza.
Vituo vya gesi
1.Kinyerezi 398MW
2.Ubungo power plant 231MW
3.Songas 189 MW
4.Tegeta Thermal 45MW
5.Somanga Fungu 8 MW
6.Ubungo 2 power plant undisclosed
7.Mtwara 22 MW

Vituo vya umeme wa maji
1.Kidatu 204MW
2.Kihansi 180 MW
3.Mtera 80 MW
4.Pangani 68 MW
5.Hale 21Mw
6.Nyumba ya Mungu 8M

Maswali?
1.Kati ya hivi vyanzo kipi hakifanyi kazi.
2.Je kuna tatizo lolote kubwa kwa upande wa vyanzo vya gesi? Au Tanesco wameshindwa kununua gesi?
3.kwanini tunafikiri utatuzi wa tatieo hili ni kuwshwa kwa mitambo ya bwawa la mwl Nyerere wakati hivi vyanzo vinatosheleza na kubaki kama vinafanya kazi.
4.nini nafasi ya mitambo ya zamani baada ya kuanza kutumia bwawa la Nyerere.
5.Mitambo ya kinyerezi 2,3 na 4 itajengwa au kukamilishwa lini?
Kwa mujibu wa takwimu uwezo wa mitambo kwa sasa ukitoa bwawa la Nyerere ni 1,602 MW na mahitaji ya juu kabisa kwa mwaka 2023 ilikuwa 1,482 . Naibu waziri pia amenukuliwa akisema upungufu wa umeme umeshuka hadi kufikia 144 M sasa kwa nini mgao unazidi kila siku?
.
Screenshot_20240216-123800_Chrome.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom