Dotto Biteko aambiwe ukweli. Kuzuia likizo za wafanyakazi wa TANESCO ni ukiukwaji wa sheria, na hakuleti umeme

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
21,563
50,415
Tatizo la umeme hapa nchini ni la kimfumo, siyo la mtu (waziri). Ndiyo maana mawaziri wengi wanateuliwa na kutenguliwa lkn tatizo liko pale pale.

Waziri Biteko naye kama wenzake waliopita hana jipya. Namuona amejaa maneno mengi ya vitisho na manyangaso kwa wafanyakazi wa TANESCO lkn tatizo la umeme liko palepale.

Waziri Biteko amesikika mara kadhaa akiwakataza watumishi wa wizara yake hasa TANESCO kwenda likizo. Ikumbukwe kuwa hizi likizo zipo kisheria na ni haki ya mfanyakazi kwenda likizo.

Biteko baada ya kukosa mbinu na ubunifu wa kutatua tatizo la umeme sasa ameona ajifiche kwenye kichaka cha kukanyaga haki za wafanyakazi wa TANESCO.

Pia soma
- Biteko afuta likizo zote za Watumishi wa TANESCO
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom