TANESCO yautaja umeme wa gesi kama 'umeme wa gharama'

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,413
7,678
TANESCO katika mpango mkakati wake wa miaka mitano imesema pamoja na kupungua utegemezi wa matumizi ya mafuta mazito kuzalishia umeme, gesi nayo majanga. Gharama ya kufikisha gesi kwenye vituo vya kuzalishia umeme kutoka inapochimbwa inabakisha gharama ya uzalishaji wa umeme kuendelea kuwa juu.

Kati ya mwaka 2015 mpaka 2019 megawats 320 ziliondolewa kwenye gridi ya Taifa kutoka kwenye makampuni binafsi ya Aggreko(100MW), Symbion (120MW), IPTL(100MW) na umeme kutoka nje ya nchi mojawapo ya sababu ikiwa kupunguza gharama ya uendeshaji TANESCO.

Mpango kazi wa TANESCO ukaitaka TANESCO kuendelea kuwekeza kwenye vyanzo nafuu kama mbadala wa vyanzo vya gharama.

Hii ni sababu ya awamu ya tano kuamua kwenda Rufiji badala ya kujikita Kinyerezi?

TANESCO 1.JPG
 
Elimu hapa, gesi ni mafuta yaliyo kwenye hali ya kimiminika.

Kama umeme wa mafuta ni gharama na gesi nao ni gharama vile vile kwakua vyanzo vinafanana, tofauti ni wingi wa nishati kwa ujazo unaofanana (volume in cubic metres)
 
Niliwambia watu humu Zitto naye ni kilaza..wwtu wote wameingia wamekuta gasi iliuzwa na kikwete hivyonkama nchi hatuna gasi ya kujichotea.

Sasa na samia aliingia na mbwembe na akina january nao wamekwamana wanawaza kwenda kwenye solar na windi ..mbona hawaendi kwenye gas waliokuwa wanamtukania magufuri kuwa kaitelekeza?
 
Tunaweza kupata hiyo document..tukarefer au you tube wakito hotuba husika.
 
Makamba anakuambia twende kwenye umeme wa upepo na solar, hizo ndio gharama zaidi. Yaani mtu anakurupuka tu anawaza kupiga 10% zake.
Hta SGR ni gharama kuliko reli ya kawaida mbona hamuongelei gharama? Hta Airport mpya maintenance cost yake ni kubwa kuliko kabla ya upanuzi.

Cha msingi supply ya umeme iwepo ila tukiangalia gharama tu hakuna kitu tungeshafanya.
 
TANESCO katika mpango mkakati wake wa miaka mitano imesema pamoja na kupungua utegemezi wa matumizi ya mafuta mazito kuzalishia umeme, gesi nayo majanga. Gharama ya kufikisha gesi kwenye vituo vya kuzalishia umeme inabakisha gharama ya uzalishaji wa umeme kuendelea kuwa juu....
Huu ndiyo mzizi wa kutangaziwa mabwawa yamekauka.

Haya makampuni yanataka yarudi kuiuzia Tanesco
 
Niliwambia watu humu Zitto naye ni kilaza..wwtu wote wameingia wamekuta gasi iliuzwa na kikwete hivyonkama nchi hatuna gasi ya kujichotea..sasa na samia aliingia na mbwembe na akina january nao wamekwamana wanawaza kwenda kwenye solar na windi ..mbona hawaendi kwenye gas waliokuwa wanamtukania magufuri kuwa kaitelekeza?
Mradi wa gesi ni trillion of Tshs pengine tusingeweza wenyewe walau mwanzoni coz gharama zinakua juu. So mnafanya tu concession agreement ila kusema imeuzwa ni overstatement.

Otherwise mliotaka tuchimbe wenyewe 100% mtuambie hyo pesa tungetoa wapi?
 
TANESCO katika mpango mkakati wake wa miaka mitano imesema pamoja na kupungua utegemezi wa matumizi ya mafuta mazito kuzalishia umeme, gesi nayo majanga. Gharama ya kufikisha gesi kwenye vituo vya kuzalishia umeme inabakisha gharama ya uzalishaji wa umeme kuendelea kuwa juu...
Sasa si bora wa gharama uwake kuliko wa cheap hauwaki, watu wanakwenda na Technologia duniani wewe unakwenda na historia wapi na wapi ndugu.
 
Hta SGR ni gharama kuliko reli ya kawaida mbona hamuongelei gharama? Hta Airport mpya maintenance cost yake ni kubwa kuliko kabla ya upanuzi.

Cha msingi supply ya umeme iwepo ila tukiangalia gharama tu hakuna kitu tungeshafanya.
Bidhaa zetu haziwezi kushindana na soko la nje kama tutaendelea kujikita kwenye uzalishaji kwa gharama kubwa ya umeme.
 
TANESCO katika mpango mkakati wake wa miaka mitano imesema pamoja na kupungua utegemezi wa matumizi ya mafuta mazito kuzalishia umeme, gesi nayo majanga. Gharama ya kufikisha gesi kwenye vituo vya kuzalishia umeme inabakisha gharama ya uzalishaji wa umeme kuendelea kuwa juu...
Policy changes awamu ya 4 gas awamu ya 5 hydro awamu ya 6 wind solar geothermal.

Gas ya uhakika lakini ghali hatuna trillions za exploration rigs special pipes refineries.

Lakini wataalam wetu wanashindwa kushauri focus iwe wapi kwanza ambayo iko efficient ktk time resources and financial resources tukapriotize.

Hizo options za wind, solar na geothermal zinahitaji muda nazo na kwa mabadiliko tabia nchi uhakika wa mvua ni mdogo sana.

Jopo la wataalam wakae na kishauri option hipi ni ya haraka na nafuu
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom