TensorFlow
JF-Expert Member
- Feb 11, 2020
- 812
- 969
Huyo jamaa wanasema ndiye Rais ajaye!Makamba yeye kila kitu huwa anawaza nje tu , mifumo kama gepg, plann rep , GotTHoMis imetengenezwa na wataalam wetu
Huyo jamaa wanasema ndiye Rais ajaye!Makamba yeye kila kitu huwa anawaza nje tu , mifumo kama gepg, plann rep , GotTHoMis imetengenezwa na wataalam wetu
Whatever the case, ni kwamba Tz nzima hakuna mtu wa kutengeneza huo mfumo?GePG ni erps (enterprise resources planning system) ?????
Sijui ni nani katuloga hii nchiMtu mwenye akili ya ku code GePG ukimpa functions za Tanesco anashindwa vipi ku code hio ERP? Au hujui systems zinavyoandaliwa wewe?
Mpaka uwape wakorea ni kwamba Tz nzima hatuna watu wenye uwezo wa kutengeneza huo mfumo?Wahindi Tena Bora wangepewa hiyo tenda Korea kusini nahisi ndio nchi pekee duniani yenye kuaminika
Mbona huulizi wakati serikali inanunua software za Microsoft Windows? Kwa nini eGA hawaandiki OS itumike serikalini?Unaijua eGA mkuu? Kwanini utumie wahindi wakati eGA ipo?
Akili iliyotumika kutengeneza Corolla na IST, ndio hiyo hiyo iliyotumika kutengeneza Landcruiser V8.GePG ni erps (enterprise resources planning system) ?????
🤣 Haya pigeni marufuku software zote za nje ili zote ziandikwe na eGA. Microsoft, Android, Apple pigeni marufuku fanyeni kila kitu wenyewe. Software za kuongoza ndege airport tengenezeni wenyewe. Za mashine za hospitali tengenezeni wenyewe. Software ni software tuu ukitengeneza moja utaweza kutengeneza zote. 🤣Akili iliyotumika kutengeneza Corolla na IST, ndio hiyo hiyo iliyotumika kutengeneza Landcruiser V8.
Waliotengeneza GePG hawawezi shindwa erps
We ungenyamaza tu mkuu. La sivyo unaweza ukahoji kwanini maisha yana ngazi tofauti. Unachotakiwa kuelewa ni kwamba kila kitu ni msukumo tu. Serikali ikiwa na dira ya kwamba Tanzania itengeneze OS yake na computer zake inawezekana kabisa.Mbona huulizi wakati serikali inanunua software za Microsoft Windows? Kwa nini eGA hawaandiki OS itumike serikalini?
Inawezekana kabisa. Ila itachukua muda kukamilisha miradi yote hiyo. Watu wenye akili kama zako wangeenda nje ya nchi kutafuta GePG.🤣 Haya pigeni marufuku software zote za nje ili zote ziandikwe na eGA. Microsoft, Android, Apple pigeni marufuku fanyeni kila kitu wenyewe. Software za kuongoza ndege airport tengenezeni wenyewe. Za mashine za hospitali tengenezeni wenyewe. Software ni software tuu ukitengeneza moja utaweza kutengeneza zote. 🤣
Najua taasisi zetu,TRA,NIDA,Zina mifumo kama hii,lakini Haina ubora kabisa,lakini kuchukua hayo mapesa ukawapa watu wa nje,badara ya kuzipa Taasisi zetu za ICT zitengeneze hiyo software,ni matumizi mabaya sana ya pesa ya umma,hapo haitaishia kununua software tu,itabidi tukodishe na hardware ambazo ni compatible na hiyo software,na hata kama kulikuwa na haja ya kukodisha software,kwanini hatukwenda South Afrika?au Misri?kwanini twende nje ya Afrika.Watanzania naona tulisahau kabisa ajenda ya ufisadi wakati wa Magufuli, mpaka sasa kuna ufisadi umefanyika fasta fasta bila ya watu hata kushtuka.
Mkataba uliosainiwa baina ya Serikali ya Tanzania (kupitia TANESCO) na kampuni ya Tech Mahindra ya India wenye thamani ya dola milioni 30 ni wa kukodisha software ya Enterprise Resources Planning (ERP) - ambayo wahindi hawa wenyewe wanaiita Corporate Management System (CMS), kama inavyosomeka kwenye bango pichani chini.
Software ya aina hii huwa inaunganisha vitengo vyote vya taasisi katika software moja kwa ajili ya urahisi wa kuendesha taasisi. Hivyo basi kwa lugha nyingine ni kwamba Wahindi hawa watafunguliwa milango ya kuingia kila mahali ndani ya TANESCO, na hivyo kuwa na siri zote za mfumo wetu wa umeme.
Jambo kama hili ni hatari sana kwa usalama wa taifa. Hakuna njia rahisi ya kuiangusha nchi bila ya kufyatua hata kombora moja kama kuangusha mfumo wa nchi wa umeme.
Software kama hizi serikali inatakiwa iwawezeshe wataalam wa ndani kupitia Mamlaka ya Serikali Mtandao kutengeneza, kama vile mfumo wa malipo serikalini ulivyotengenezwa na wataalam wetu wa ndani kwa kuwezeshwa na serikali.
Zabuni ya kukodisha software hii ilianzaga kwenye dakika za lala salama za utawala wa Kikwete. Hivyo basi kitendo cha zabuni hii kukaa benchi kwa miaka mitano ya Magufuli kinaonesha kuwa hakuwa amekubaliana nayo. Baada ya Magufuli kufa naona wadau wa zabuni hii wameiendeleza na kuimwagia wino fasta, kama wanavyotaka kufanya kuhusu bandari ya Bagamoyo.
Kukodisha software?, yaani tutapigwa hadi tusema Shikamooo Bhabha!!!!dola milioni 30 ni wa kukodisha software
hujaona dollar hapo,TAtizo la mtoa Uzi ni mshamba, mill 30 kwa software ni ya kawaida kwa kampuni kubwa kama TANESCO
Mmezoea kutumia software za uwizi unafikiri kampuni kubwa kama TANESCO nao watatumia hapana
tupeni source mkuu, tujihakiki.Jaribu kuangalia source zako za habari sidhani kama ni mill 30
Kama wanayo si wangerekebisha halafu wangewapa Tanesco wanasubiri nini? Tena ERP software yetu tuanze kufanya export nayo kama biashara tuuze au tukodishe nchi zingine ituingizie hela. Tuendelee na kutengeneza hizo zingine tushindane na Microsoft, Android, Apple na makampunzi mengine tunazonunua software zao unaonaje bosi?Inawezekana kabisa. Ila itachukua muda kukamilisha miradi yote hiyo. Watu wenye akili kama zako wangeenda nje ya nchi kutafuta GePG.
eGa tayari software ya ERP wanayo, kama kuna mahitaji mahsusi ya Tanesco ingefanyiwa marekebisho, ili pesa zibaki hapahapa nchini mikononi mwa waTanzania.