TANESCO yaingia mkataba wa kukodi software kutoka India kwa USD 30M

Siku hizi software nyingi zinakodishwa badala ya kuuzwa moja kwa moja. Faida ya kukodi ni kwamba kila wakati unapate updates na latest version ya hiyo software. Ukinunua, inakubidi kila mara ununue mpya. Hii ni gharama kubwa sana. Shida ya kukodi ni kuwa inategemea na vifaa vingapi unataka kufunga/kuunganisha hiyo software. Nyingine ni kuwa ukiacha kulipa kodi basi access yako nayo inakwenda na maji. Kwa mantik hii ni kuwa hii pesa iliyotajwa ni ya kila mwaka au kila baada ya kipindi walichokubaliana.

Amandla...
Siyo lazima ukodi

Kukodi ni mbinu mpya ya software developers ili uwe mteja wao wa milele

Kuna software nyingi tu unanunua mara 1 tu na unapata free lifetime upgrades and updates
 
Very correct SIR!

Everything begins with a thought, and thoughts are turned into plans, and plans into reality​

 
Kama wanayo si wangerekebisha halafu wangewapa Tanesco wanasubiri nini? Tena ERP software yetu tuanze kufanya export nayo kama biashara tuuze au tukodishe nchi zingine ituingizie hela. Tuendelee na kutengeneza hizo zingine tushindane na Microsoft, Android, Apple na makampunzi mengine tunazonunua software zao unaonaje bosi?
Ndugu unachoandika hakipo au hujuwi ni nini unaongea

Ni bora unyamaze tu nimekuona muda mrefu unaongea pumba tu kwenye huu uzi
 
Siyo lazima ukodi

Kukodi ni mbinu mpya ya software developers ili uwe mteja wao wa milele

Kuna software nyingi tu unanunua mara 1 tu na unapata free lifetime upgrades and updates

Nimesema nyingi. Sio zote. Ziko mpaka za bure.

Amandla...
 
Hii inagharimu dola 155 kwa mwezi kwa mwaka ni usd 1860


Ni ya WordPress

Unachohitaji ni WordPress site (WordPress ni bure) na hiyo plugin

Kutoka hapo sasa unaweza kufanya reverse engineering ya source code ya hiyo plugin ukarekebisha hiyo software yako kwa mjibu wa mahitaji yako na ikawa yako milele bila kuhitaji kumlipa mtu kila mwaka au mwezi
 
Hata hizo chache kukodi au kununua ni UJINGA wako mwenyewe

Mimi sijawahi kunununua windows wala Microsoft Word miaka yote tangu niijue computer
Inaonyesha ulivyo mshamba huo ni uwizi kaka
Mfano
Juzi jamaa alienda marekani na alikua anatumia spss iliyokua crack, kitendo Cha kuingia New York city na kuacess wifi Ile spss ili disappear immediately

We ndo mjinga sababa unachofanya ni ujinga ndo maana watanzania wakija na software biashara kwasababu Kuna wajinga kama wewe unataka kutumia bure usionge mbele ya watu huu upupu tena
 
Ndugu unachoandika hakipo au hujuwi ni nini unaongea

Ni bora unyamaze tu nimekuona muda mrefu unaongea pumba tu kwenye huu uzi
Kama nimeandika kipo na wewe umekisoma. Labda wewe uwezo wako wa kuelewa kilichoandikwa ni mdogo.
 
Watanzania naona tulisahau kabisa ajenda ya ufisadi wakati wa Magufuli, mpaka sasa kuna ufisadi umefanyika fasta fasta bila ya watu hata kushtuka.

Mkataba uliosainiwa baina ya Serikali ya Tanzania (kupitia TANESCO) na kampuni ya Tech Mahindra ya India wenye thamani ya dola milioni 30 ni wa kukodisha software ya Enterprise Resources Planning (ERP) - ambayo wahindi hawa wenyewe wanaiita Corporate Management System (CMS), kama inavyosomeka kwenye bango pichani chini.

Software ya aina hii huwa inaunganisha vitengo vyote vya taasisi katika software moja kwa ajili ya urahisi wa kuendesha taasisi. Hivyo basi kwa lugha nyingine ni kwamba Wahindi hawa watafunguliwa milango ya kuingia kila mahali ndani ya TANESCO, na hivyo kuwa na siri zote za mfumo wetu wa umeme.

Jambo kama hili ni hatari sana kwa usalama wa taifa. Hakuna njia rahisi ya kuiangusha nchi bila ya kufyatua hata kombora moja kama kuangusha mfumo wa nchi wa umeme.

Software kama hizi serikali inatakiwa iwawezeshe wataalam wa ndani kupitia Mamlaka ya Serikali Mtandao kutengeneza, kama vile mfumo wa malipo serikalini ulivyotengenezwa na wataalam wetu wa ndani kwa kuwezeshwa na serikali.

Zabuni ya kukodisha software hii ilianzaga kwenye dakika za lala salama za utawala wa Kikwete. Hivyo basi kitendo cha zabuni hii kukaa benchi kwa miaka mitano ya Magufuli kinaonesha kuwa hakuwa amekubaliana nayo. Baada ya Magufuli kufa naona wadau wa zabuni hii wameiendeleza na kuimwagia wino fasta, kama wanavyotaka kufanya kuhusu bandari ya Bagamoyo.

img-618a884f193e3.jpg
Yaani Enterprise Resources Planning (ERP) ni 30M usd tena ya kukodi? Wakati wangeweza kutengeneza watu wa IT nchini. Hata sisi tuna uwezo wa kutengeneza hizo na CRM ni ufisadi
 
Huyo ni mjinga kama anaona kununua au kukodisha software ni ujinga

Kwa mentality yake anaweza support software ambayo imetengenezwa na mtanzania
Sasa wewe hata hujuwi tofauti ya usd na tsh unafikiri naweza kujibizana na wewe?

Bilioni 69 kwa ajili ya trial software ya erp ni wizi wa mchana kweupe

Tangaza hiyo tenda kwa Watanzania uone kama watashindwa kuunda hicho kisoftware uchwara
 
Inawezekana kabisa. Ila itachukua muda kukamilisha miradi yote hiyo. Watu wenye akili kama zako wangeenda nje ya nchi kutafuta GePG.
eGa tayari software ya ERP wanayo, kama kuna mahitaji mahsusi ya Tanesco ingefanyiwa marekebisho, ili pesa zibaki hapahapa nchini mikononi mwa waTanzania.
Ndio unaacha kumlipa mtanzania kwa tsh unaenda kupeleka dollars nje ya nchi tena kwa program za kawaida tu
 
Mbona huulizi wakati serikali inanunua software za Microsoft Windows? Kwa nini eGA hawaandiki OS itumike serikalini?
we jamaa pumba sana, kwani hujui kuna mifumo mingine ipo kwenye windows? kwa hiyo serikali iandike OS kisha ifuatie na utility softwares n.k issue ni kuwa huu mfumo ungeweza kutengenezwa na watanzania kama ambavyo mingine imetengenezwa na kutika mpaka sasa bila shida, hiyo kununua nje ni ishara ya upigaji,mboba watu hawajalalamika ndege kununuliwa nje??? sababu tunajua sio uwezo wetu, ila kwa hili hapana, wataalamu wa ndani ni muhimu wapewe fursa ili waweke ujuzi wao
 
we jamaa pumba sana, kwani hujui kuna mifumo mingine ipo kwenye windows? kwa hiyo serikali iandike OS kisha ifuatie na utility softwares n.k issue ni kuwa huu mfumo ungeweza kutengenezwa na watanzania kama ambavyo mingine imetengenezwa na kutika mpaka sasa bila shida, hiyo kununua nje ni ishara ya upigaji,mboba watu hawajalalamika ndege kununuliwa nje??? sababu tunajua sio uwezo wetu, ila kwa hili hapana, wataalamu wa ndani ni muhimu wapewe fursa ili waweke ujuzi wao
Kuna swala la usalma pia yaan mfumo ukicrush kidogo wataalaam wanakuja unawalipia kila kitu ikiwepo perdiem kwa rate za dollars
 
34 Reactions
Reply
Back
Top Bottom