TensorFlow
JF-Expert Member
- Feb 11, 2020
- 812
- 969
Nimecheka sana.Kuna Halmashauri niliwahi kufanya kazi Idara ya Ardhi waliibia Halmashauri huku madiwani wakimwaga sifa nyingi kwa ubunifu wa ile Idara. Walidownload Google Map wakadai wamenunua software kwa gharama ya Sh 20 milioni ili kusaidia mipango mji.
Lile dude tulilibeba mpaka Maonesho ya Nane Nane kuwaonesha wananchi jinsi Halmashauri yetu ilivyopiga hatua katika Idara ya Mipango Miji. Sidhani mpaka leo kama ile Halmashauri ilishagundua iliibiwa. Tuligundua vijana wawili tu kitoka Idara nyingine ambao tulikuwa ndo tumepata ajira.
Just imagine kama Halmashauri inaibiwa kienyeji namna hiyo hali ikoje katika mambo makubwa ambayo Watanzania wengi hawana utaalam nayo?