BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,011
Ukiamua kutumia akili yako na kuandika kutoka moyoni mwako unaandika yaliyojaa busara na hekima tele, lakini ukiamua kuunga tela la wale Buku 7 basi ni utata mtupu!!!
Huyu FaizaFoxy nitamkaribisha siku yoyote ile nyumbani kwangu aje tule mahanjumati tuongee na kucheka kuhusu mambo mbali mbali ya kuhusu nchi yetu na dunia nzima. Akinialika kwake huyu basi nitafanya kila niwezalo nikanywe hata chai na vitumbua kama siyo pilau la nguvu la binti wa Kariakoo.
Hongera zako na ujue kwamba FaizaFoxy huyu ni kipenzi cha wengi hapa jamvini.
Nakutakia weekend njema
Huyu FaizaFoxy nitamkaribisha siku yoyote ile nyumbani kwangu aje tule mahanjumati tuongee na kucheka kuhusu mambo mbali mbali ya kuhusu nchi yetu na dunia nzima. Akinialika kwake huyu basi nitafanya kila niwezalo nikanywe hata chai na vitumbua kama siyo pilau la nguvu la binti wa Kariakoo.
Hongera zako na ujue kwamba FaizaFoxy huyu ni kipenzi cha wengi hapa jamvini.
Nakutakia weekend njema
Ikiwa waliisaini na mpaka ifikapo October 2014 itakuwa bado ni mikataba hai, hapo tutajiingiza katika gogoro lingine kama lile tililojiingiza na Dowans ya Al Adawi. Mpaka leo tunalipa kwa gharama kubwa sana, kwa kujidai kwetu kutaka kuvunja mkataba wa Kimataifa. Tutawalipa tu.
Lakini ikiwa mpaka ifikapo hapo October 2014 tutakuwa tumemaliza nao mkataba basi itakuwa ni sawa na hatuna lawama.
Ikumbukwe kuwa mikataba ya Aggreko na Symbion ni mikataba ya dharura mpaka pale tutakapoweza kujikimu na umeme wa uhakika. Kuna miradi mingi ya muda mrefu ambayo inatekelezwa kwa sasa. hakuna sababu kwanini tuendelee na mikataba ya dharura pale tutapokuwa tunajiweza wenyewe.
Isitoshe, ni rahisi sana kwa Symbion na Aggrekko kutuuzia mitambo yao kwa bei nafuu pale tutapokuwa tunajiweza kwa umeme wa uhakika na hiyo mi jenereta yao ikabaki kwetu kwa dharura tu, kwani mpaka wakati huo watakuwa wamesharudisha fedha zao na mifaida kibao.
Waafrika tuone hivi hivi tunajuwa sana kuongea, kupanga na kupangua lakini hatujuwi kutekeleza. Leo mchukuwe Mtanzania yeyote umuulize kuhusu ligi ya mpira wa Uingereza, basi utamkuta anaijuwa hiyo ligi na namna timu inatakiwa iwe kuliko Mourinho. Hiyo si kwenye mpira tu, ni kila pahali, tunajuwa kila kitu kwa midomo yetu lakini kutenda? Ng'oo.
Nchi hii muumba dunia na ardhi alitujaaalia kila kitu chema, maji mengi, madini mengi, ardhi nzuri inayo-limika miezi 12 kwa mwaka, misitu mizuri, mbuga nzuri, milima mizuri, mabonde mazuri, watu wazuri, wanyama wazuri. Kwa ufupi katupa pepo ya duniani, lakini kitu kimoja hatukupewa, nacho ni akili. Akili hatuna.
Binaadam hakosi kasoro na kasoro yetu ni akili.
Wakati sisi tutaanza kuwa na umeme wa uhakika (miaka 50-100 ijayo), kumbuka kuwa mpaka sasa ni 14% tu ya Watanzania wenye umeme tena sio wa uhakika, wenzetu watakuwa hawana haja ya maviwanda ya umeme, majumba na maviwanda yanayohitaji umeme yatakuwa yanajizalishia yenyewe umeme (haya yameshaanza kwa wenzetu, kuna majumba mapya huko yanajizalishia yenyewe umeme na ule wa ziada wanawauzia gridi zao) Hapo sasa.
Self-sufficient Urban Buildings | BETTER WORLD // ENGINEERING
Sosoljip is a Self-Sufficient Net Zero Energy House in South Korea | Inhabitat - Sustainable Design Innovation, Eco Architecture, Green Building
MenoMenoPiu Unveils Plans for Wind-Powered Alvar Aalto Campus Otaniemi | Inhabitat - Sustainable Design Innovation, Eco Architecture, Green Building