TANESCO kuachana na Symbion na Aggreko?

Shirika la tanesco liuzwe kwa shirika la umeme la Zambia. Watanzania tutaufaidi umeme kwa bei poa
Mkuu,

Nadhani humaanishi.

Zambia? Seriously? Unasikia tu au umefuatilia? Satta ana wakati mgumu sana. Labda kama hufuatilii kwa karibu!

Kwa muda wako, soma hii kitu na kisha urejee mezani unambie kama utarudia kutoa reference ya Zambia - Energy crisis threaten to paralyse Zambia
 
Wakiweza kuvunja hii mikataba tutafungua ukurasa mpya, lakini wasiwasi wangu ni kama tunao mbadala wa makampuni haya ambayo kiukweli yanatia hasara kubwa sana japo yanasaidia.

Kumbuka, ni mwaka jana tu tuliambiwa kuwa TANSECO wanailipa kila siku Symbion Power milioni 152 na katika kila sh.100 zinzoingia TANESCO, sh.86 inaelekwzwa kwenye malipo hayo!
my concern ni kwamba kwenye hiyo mikataba waliyosaini kuna kipengele cha kuivunja?,kama hakuna na wakivunja huoni watakuwa wamekiuka masharti?
 
Mind games; Think again!

Siasa zimeingia kila sehemu. Tutazuiwa na wanasiasa kuongelea hata baadhi ya issues na usishangae kuwa unaweza kuwa branded 'msaliti' au 'unatumiwa' au 'hii hoja yetu' na wale wanufaika wanazidi kunufaika kutokana na kugawanyika kwetu!

Tunatakiwa kurejea kwenye mstari. Tunajenga nyumba moja, tusigombanie fito. Wanawekeza kwenye ujinga wa wachache, wanakatisha tamaa wale wenye kuweza kuyaona madudu na kuyakemea critically

Asante!
 
my concern ni kwamba kwenye hiyo mikataba waliyosaini kuna kipengele cha kuivunja?,kama hakuna na wakivunja huoni watakuwa wamekiuka masharti?

Kwani biashara ya utumwa ilikuwa na mkataba kwamba kuna siku ingekuja kukoma? Ukoloni ulikuwa na mikataba kwamba ungeisha miaka ya 1960s?

Ni uamuzi tu. Gharama za kuvunja mikataba ni nafuu kuliko kuendelea kuteseka hivi!

Fikiria nchi haina umeme, lakini katika kila 100% ya mapato, wamiliki wa mikataba hewa wanalamba 86%.
 
Ikiwa waliisaini na mpaka ifikapo October 2014 itakuwa bado ni mikataba hai, hapo tutajiingiza katika gogoro lingine kama lile tililojiingiza na Dowans ya Al Adawi. Mpaka leo tunalipa kwa gharama kubwa sana, kwa kujidai kwetu kutaka kuvunja mkataba wa Kimataifa. Tutawalipa tu.

Lakini ikiwa mpaka ifikapo hapo October 2014 tutakuwa tumemaliza nao mkataba basi itakuwa ni sawa na hatuna lawama.

Ikumbukwe kuwa mikataba ya Aggreko na Symbion ni mikataba ya dharura mpaka pale tutakapoweza kujikimu na umeme wa uhakika. Kuna miradi mingi ya muda mrefu ambayo inatekelezwa kwa sasa. hakuna sababu kwanini tuendelee na mikataba ya dharura pale tutapokuwa tunajiweza wenyewe.

Isitoshe, ni rahisi sana kwa Symbion na Aggrekko kutuuzia mitambo yao kwa bei nafuu pale tutapokuwa tunajiweza kwa umeme wa uhakika na hiyo mi jenereta yao ikabaki kwetu kwa dharura tu, kwani mpaka wakati huo watakuwa wamesharudisha fedha zao na mifaida kibao.

Waafrika tuone hivi hivi tunajuwa sana kuongea, kupanga na kupangua lakini hatujuwi kutekeleza. Leo mchukuwe Mtanzania yeyote umuulize kuhusu ligi ya mpira wa Uingereza, basi utamkuta anaijuwa hiyo ligi na namna timu inatakiwa iwe kuliko Mourinho. Hiyo si kwenye mpira tu, ni kila pahali, tunajuwa kila kitu kwa midomo yetu lakini kutenda? Ng'oo.

Nchi hii muumba dunia na ardhi alitujaaalia kila kitu chema, maji mengi, madini mengi, ardhi nzuri inayo-limika miezi 12 kwa mwaka, misitu mizuri, mbuga nzuri, milima mizuri, mabonde mazuri, watu wazuri, wanyama wazuri. Kwa ufupi katupa pepo ya duniani, lakini kitu kimoja hatukupewa, nacho ni akili. Akili hatuna.

Binaadam hakosi kasoro na kasoro yetu ni akili.

Wakati sisi tutaanza kuwa na umeme wa uhakika (miaka 50-100 ijayo), kumbuka kuwa mpaka sasa ni 14% tu ya Watanzania wenye umeme tena sio wa uhakika, wenzetu watakuwa hawana haja ya maviwanda ya umeme, majumba na maviwanda yanayohitaji umeme yatakuwa yanajizalishia yenyewe umeme (haya yameshaanza kwa wenzetu, kuna majumba mapya huko yanajizalishia yenyewe umeme na ule wa ziada wanawauzia gridi zao) Hapo sasa.

Self-sufficient Urban Buildings | BETTER WORLD // ENGINEERING

Sosoljip is a Self-Sufficient Net Zero Energy House in South Korea | Inhabitat - Sustainable Design Innovation, Eco Architecture, Green Building

MenoMenoPiu Unveils Plans for Wind-Powered Alvar Aalto Campus Otaniemi | Inhabitat - Sustainable Design Innovation, Eco Architecture, Green Building

Kumbe ukiacha siasa unaongea points za nguvu

Hongera sana mama

"Jamani tuache siasa, tufanye kazi" - H.E. Dr. John Magufuli
 
Mikataba yote hiyo ni ya kinyonyaji kupindukia. Tanesco inaweza kuwa na mitambo yake na kuachana na kupe. Hata hivyo inabidi kwanza kuwakomesha mafisadi tanesco na serikalini wanaoingia mikataba kuwatoa damu wananchi. Tanesco ikiongozwa kiadilifu gharama za umeme zisizobebeka na wananchi zinaweza kushuka hata kwa nusu.

Shida sio TANESCO .... ni siasa kuingilia TANESCO ... hii imetokea kwenye maeneo mengi tu hasa awamu hii ya nne ...sio TANESCO tu,...elimu, TANROADS, etc
 
Mkurugenzi anatingisha kiberiti akipewa shea yake tuu kwisha chezea rostam wewe
 
inadaiwa bodi ya wakurugenzi ya tanesco imepania kuachana na mikataba ambayo inaonekana kuwa mzigo kwa shirika kati yake na makampuni ya symbion power na aggreko mwezi oktoba 2014, kutokana gharama kubwa zisizoshikika toka kwa makampuni haya.

Nini hatma ya tanesco?

Tunao mbadala wa makampuni haya?

Tutarajie mgao mkubwa kuelekea 2015?

Tumepata uhakika baada ya kupatikana kwa gesi?

ni majuzi tuu nilimsikia babra masoud akisema wanaendesha shirika kwa hasara maana wananua umeme kwenye mashirika tajwa kwa bei ya juu alaf ndio wana sambazia na akasema hawana jinsi wataomba gharama za umeme kupanda.

Mi nafikiri kwa hali hii sidhani kama tayari tunaweza kuitegemea gas kupata umeme.

Nadhani pamoja na hasara bado tuna yahitaji hayo mashirika sema tuna hofu gharama kupanda maradufu.
 
Hapa tujiandae kulipa zaidi kwaajili ya umeme na tanesco hawayovunja mikataba hiyo.
 
Jenerali kachachamaa baada ya kuchefuliwa na katibu?hii vita ni zaidi ya tunavyosoma magazetini.

Invisible hebu malizia na hayo uliyoficha bhana,usiogope humu hawasomagi kwi kwii!hata hivyo nawaunga mkono wakurugenzi.

Nadhani maamuzi yao ni technical yenye tathmini sahihi kuliko hawa politicians wa wizarani. Hofu yangu watakapokuja na alternative yao huenda wakahujumiwa kama watapuuzia nguvu ya politicians hapo Ubungo.

Nchi ngumu hii, mezani mnadiscus rotors, transformers, cables, finances huku kichwani mnafikiria namna ya kumdhibiti mheshimiwa asilete zake, kazi ipo!
 
Wakiweza kuvunja hii mikataba tutafungua ukurasa mpya, lakini wasiwasi wangu ni kama tunao mbadala wa makampuni haya ambayo kiukweli yanatia hasara kubwa sana japo yanasaidia.

Kabla ya kuwa na wasiwasi kama tunao mbadala wa makampuni hayo, tujiulize kwanza hiyo mikataba inaisha lini?

Kama inaisha baada ya Oktoba 2014 halafu tukaivunja kabla ya hapo, implications zake ni nini hasa? Possibly ni breach of contract.

Now, tutakuwa tayari kuwaunga mkono bodi ya wakurugenzi ya Tanesco pale makampuni hayo yatakapoamua ku-exercise that important arbitration clause kwenye hiyo mikataba na kuishtaki Tanesco for damages caused by such breach?

Mpo tayari kulipa hizo damages and all the costs associated with the arbitral proceedings?

By the way, zile za Dowans tumeshazilipa?
 
Kwani biashara ya utumwa ilikuwa na mkataba kwamba kuna siku ingekuja kukoma? Ukoloni ulikuwa na mikataba kwamba ungeisha miaka ya 1960s?

Ni uamuzi tu. Gharama za kuvunja mikataba ni nafuu kuliko kuendelea kuteseka hivi!

Fikiria nchi haina umeme, lakini katika kila 100% ya mapato, wamiliki wa mikataba hewa wanalamba 86%.

Tunaomba ushahidi wa hilo, isiwe wewe ndio unatupa takwimu hewa.
 
Nini hatma ya TANESCO?

Tunao mbadala wa makampuni haya?

Tutarajie mgao mkubwa kuelekea 2015?

Tumepata uhakika baada ya kupatikana kwa gesi?

-Hatma ya TANESCO ni kifo cha mende kama ilivyo kwa mashirika yote ya umma, ni wakati muafaka tukawachia makampuni binafsi yakazalisha, kusafirisha na kuuza umeme. Tumeona tulivyokuwa tunaumizwa na TTCL, ni hivyo hivyo tunaumizwa TANESCO.

-Mbadala tukiutaka tunao. Nakupa siri moja; kuna kampuni ya umeme iliyokuwa tayari kuwekeza kwa fedha zao kujenga damn ya kisasa. wakakubaliwa, baada ya kufanya feasibilty study iliyowagharimu kama dola million 3, walipiwasilisha kwa Mhongo hata hakuitazama wala kuisoma, akasema haifai.

Huo Mkataba waliokuwa nao (Memorandum of Understanding) inabidi Serikali iwalipe Dola Million 4, na wakienda mahakamani watalipwa zaidi kwani damn hiyo hiyo kwa sasa wamepewa Wachina waijenge (sub standard). Huo ndio Muhongo.

- Uhakika wa umeme si kwa gesi tu, gesi ni mojawapo na pia kuna mradi wa Steigler Gorge unaoendeshwa na Wabrazil, kuna mradi huo wa Wachina niliousema (haujaanza) lakini umesha sainiwa na Pinda alivyokuwa China juzi juzi, kuna mradi wa Wacanada na mwingine wa Wachina wa umeme wa Makaa ya mawe. Mbali na hii gesi ambayo bomba ndio linasambazwa.
 
TANESCO wangekuwa wanamiliki yale majenereta na kununua gesi kuzalisha umeme, haya matatizo hayangekuwepo. Hawa middle men wanaomiliki majenereta hayo na ambao wameingia mikataba ya kifisadi na TANESCO ya kulipa capacity charges na bei ya juu, ndicho chanzo cha hii shida! TANESCO wanunue majenerator yao wazalishe umeme kwa kulipia gesi tu na wataepuka huo mtego. Nadhani kuvunja mikataba ile sio rahisi. Imetengenezwa kwa masharti ya kifisadi. Itakuwa kama Richmond!
 
Kwani biashara ya utumwa ilikuwa na mkataba kwamba kuna siku ingekuja kukoma? Ukoloni ulikuwa na mikataba kwamba ungeisha miaka ya 1960s?

Mawazo kama haya kutoka kwa wenye nchi ni mfano mzuri kuwa tatizo lipo kwa hao hao wenye nchi.

Si juzi tuu mlivunja mkataba na Dowans? Humjamaliza hata kuwalipa kumbe tayari ulishaingia kwenye mikataba mingine ambayo unataka kuivunja tena.

Ni uamuzi tu. Gharama za kuvunja mikataba ni nafuu kuliko kuendelea kuteseka hivi!

Kama ni nafuu kwa nini mlikuwa hamtaki kuilipa Dowans? You think it is just simple like that kuvunja mikataba eh?

Juzi hapa tuu uliambiwa kuwa kama huwezi kumudu gharama za umeme ni vema ukaamua kuwasha kibatari au ukae gizani halafu bado unatarajia mikataba hiyo ivunjwe?

Fikiria nchi haina umeme, lakini katika kila 100% ya mapato, wamiliki wa mikataba hewa wanalamba 86%.

Sasa ukivunja hivyo mikataba ndiyo umeme utapatikana? Ndiyo watu wataacha kulamba hiyo 86 per cent?

Unless you address the root cause of the problem hata kama ukivunja hiyo mikataba bado wataendelea kulamba hizo per cent.

Hili tatizo halikuanza baada ya kuingia kwenye mikataba na hayo makampuni.
 
TANESCO wangekuwa wanamiliki yale majenereta na kununua gesi kuzalisha umeme, haya matatizo hayangekuwepo. Hawa middle men wanaomiliki majenereta hayo na ambao wameingia mikataba ya kifisadi na TANESCO ya kulipa capacity charges na bei ya juu, ndicho chanzo cha hii shida! TANESCO wanunue majenerator yao wazalishe umeme kwa kulipia gesi tu na wataepuka huo mtego. Nadhani kuvunja mikataba ile sio rahisi. Imetengenezwa kwa masharti ya kifisadi. Itakuwa kama Richmond!

Hata kama kama wakimiliki hayo majenereta na kununua gesi ya kuzalishia umeme wao wenyewe bado utakuwa haujatatua the underlying problem.

Sana sana itakuwa ni sawa na kubadilisha Division 0 kuwa Division 5 ili uweze kumiliki cheti.
 
Mhhhhhh!!!! a race to create 2 more Dowans in 2014!?
 
Back
Top Bottom