MTAZAMO
JF-Expert Member
- Feb 8, 2011
- 19,643
- 33,427
Siku ambayo utaacha kutegemea mawazo ya wanasiasa yakuongoze huko unakotaka kwenda ndiyo siku ambayo utakombolewa kifikra.
Seriously, hatuhitaji mawazo ya mwanasiasa kufahamu matatizo yanayotukumba, hasa hili tatizo sugu la umeme.
Mkuu upepo wa kisiasa usikufanye uchukie wanasiasa wanapoombwa mawazo yao.
Tatizo la umeme halihitaji ufafanuzi wa Mnyika lakini kama waziri kivuli wa wizara husika tena kwa muda mrefu nategemea mawazo mapana zaidi kutoka kwake kama mwanaJF.
Kumtaja mtu humu ni njia tu ya kumualika kwenye mjadala kama ambavyo nimewahi kukutaja wewe sidhani kama maana yake ni kuongozwa kwa kutegemea fikra zako.