Tamko Rasmi la Wanafunzi wa Vyuo vya Dodoma

Tamko Rasmi la Wanafunzi wa Vyuo vya Dodoma

Kila mkipigwa bao na lowasa ndo mnajitokeza. msubiri tena cku ya mwisho akiapishwa kesho yake mjitokeze. akili ndogonyie
 
Hahaaa hizi sarakasi za kishamba za wasomi wa Dodoma na mazingaombwe ya kimasai kutoka kwa Fisadi Lowassa. Lowassa alikuwa anafanya maigizo lakini hata hili tamko nalo ni sehemu ya maigizo tu ila director ni mwingine

Nina uhakika hili tamko halijaandaliwa na wanachuo wenyewe bali ni shinikizo kutoka kambi fulani ya CCM dhidi ya Lowassa na kama ni wanafunzi wenyewe wameandaa basi watakuwa ni mataahira kabisa. Kwa sababu:
1/Tamko kinechelewa sana. Wanafunzi wa chuo walienda Jumapili iliyopita, tamko linatolewa leo(baada ya siku4), tena baada ya mwangwi wa ukosoaji kuwa mkubwa. Kwanini?

2/Tamko hili linawakana wanachuo wale kuwa hawakutumwa na vyuo vyao, lakini wanachuo wale waliokwenda kwa Lowassa hawakusema wametumwa na vyuo vyao, walisema walikwenda wao binafsi kwa uhuru wao na utashi wao. Kuna nini hapa?

3/Tamko hili linasema waliokwenda pale ni Idadi ndogo sana kulinganisha na wanavyuo wote Dodoma. Wanachuo
Waliokwenda kwa Lowassa walisema wao ni baadhi tu ya wanachuo(Representatives). Hivyo hamna logic yoyote katika tamko kuoanisha Idadi yao na Idadi ya wanachuo wote wa vyuo vya Dodoma. Kwanini tamko lijikite kwenye Idadi?

4/Tamko limewatuhumu waliokwenda pale walipewa pesa. Hichi ndio kichekesho kikubwa kuliko vyote. Kwanza
hawajatuambia ni kiasi gani walipewa, kwa namna gani walipewa, ushahidi ni upi nk.
Sasa Rais wa chuo anakuja hadharani kabisa kukiri kwamba wasomi wake wananunulika kirahisi sana na bado hajaona kama ni tatizo. Kwanini tamko litaje pesa tu na hapo hapo likwepe kabisa kuzungumzia mazingira ya hazo pesa?

5/Kwanini tamko limekwenda mbele zaidi na kukosoa uwezo wa kiuongozi wa Lowassa wakati lengo la kutoa tamko lilikuwa ni kukana mpango wa wasomi walioko vyuoni mwao kwenda kujipendekeza kwa wanasiasa na vyama vyao. Kwanini?

6/Mwisho tamko halijasema ni hatua gani zitachukuliwa dhidi ya wanachuo hao waliochafua taswira ya vyuo vyao. Kwanini?
 
Mkuu hili baraza usilifananishe na TEC, ingekua TEC pangechimbika ndani ya mda mfupi lakini hapa kuna rupia usitegemee tamko lolote.

Hao mmoja mmoja wanaweza kununulika lakini wakikaa wengi wataona aibu. Ngoja tusubiri.
 
Tunawalaumu wazungu lkn sasa hapana, msomi kununuliwa na elimu yake tena degree na mkulima sasa hana ishu pia msomi hana ishu km ndo hivi tamaa za kivyama!! Jitambueni na mbutuke!!
 
Lowassa mbona kila mtu anakukana? Kweli wewe mzee mnafiki na muongo sana.sasa tutachagua vipi rais muongo namna hii si utatuuza wewe? Huna hata aibu khaaaaa.
 
Pumbafu kabisa hawa viongozi.. Eti wanafunzi 150 hawawezi kuwawakilisha watu 35,000. Nyie wanafunzi nane (8) inawezekanaje mkawakilisha 35,000? kama mnatutaka tufikiri kwa akili zenu za dv 5?

Jina lenu limeshachafuka sio tu leo, tokea zamani kwa kukubali kutumika kidini na kisiasa pamoja na Kikula wenu. Poor UDOM
 
kwani ni lazima wanaomuunga mkono Mh.ENL
wapate kibali cha viongozi wa serikali ya wanafunzi.?

Hizi serikali za wanafunzi ziko kwa ajili ya kutatua
matatizo ya wanafunzi na si kuwaamulia wanafunzi
ni wapi wanapaswa kuwa kiitikadi.
 
Tupo apa UDOM,
siku ile ya jumapili watu waliingia kwenye daladala zilizokuwepo hapa library wengine wakiwa wanajua wanaenda kwa mamvi ila wengine hawakujua mchezo wakadhani ni daladala za siku zote,safari ikaanza bila hata watu kudaiwa nauli na moja kwa moja hadi kwa mamvi,sasa nachoshangaa hapa waliokuwepo wengi ni viongozi wa ii UDOSO na wafuata mkumbo wengine...wametudhalilisha sana hawa wajinga

Hawakujua?? Kwahyo nyie ni rahs sana kutekwa!!!?
 
Hili tukio lilishashtukiwa kuwa kuna watu la akina Membe na Pinda kuwatumia wanafunzi wa kuwahonga mamiliini ya Pesa ili wakanushe.

Ushahidi huu hapa

PINDA, MEMBE WAPANGA KUMUHUJUMU LOWASSA

Ni wazi sasa kuwa kambi ya Mizengo Pinda na Bernard Membe wameanza kupanga mbinu chafu za kumchafua Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa.

Pinda na Membe wamepandwa na hasira zaidi mara baada ya kuona wananchi wa kada na rika tofauti wakienda nyumbani kwa Lowassa maeneo ya Area D, Dodoma na kumuomba atangaze nia na kisha achukue fomu ya kugombea urais.

Wale watu mbalimbali ambao wameshiriki kwenda kumuomba wameanza kuandamwa na kambi ya Membe na kambi ya Pinda kwa kuanza kuwarubuni kwa kuwapa rushwa waitishe vyombo vya habari na wapindishe uhalisia wa tukio.

Watu hao wanapewa pesa ili waseme kuwa Lowassa amewapa pesa, chakula, malazi na usafiri wa kwenda pale na wala hayakuwa malengo yao na wamefuata pesa tu.

Wanaorubuniwa kwenda kusema maneno ya ovyo ni wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma, masheikh pamoja na wachungaji ambao asilimia kubwa wamegoma kwenda kuisaliti mioyo yao kwa kusema uongo tofauti na uhalisia ulivyo.

Mathalani upande wa vyuoni, Vijana waliopewa kazi ya kuhakikisha hili swala linatekelezwa Ni Mwenyekiti Wa UVCCM wilaya ya Katavi(Jina linahifadhiwa).

Wanafunzi walioahidiwa kupewa fedha ili wafanye harakati hizo chafu Ni Rutagibwa, ikumbukwe Rutagibwa Ni miongoni mwa baadhi ya wafuasi Wa Membe ambao wamebaki watiifu Kwa Membe baada ya kutengenezewa trip ya kwenda China kati ya marais 25 waliopewa bongo hiyo ya safari
kimkakati ili kuwekeza ushawishi vyuoni kutoka UDOM.

Wengine ni Rais Wa Chuo cha Madini Bwana Magesa F. Magesa. Na Rais Wa chuo cha St. John. Hawa ndio wa Ratiba Wa mkakati pale Udom dhidi ya siasa chafu ya kikachero na kuhonga wanafunzi fedha ili waandamane kupinga ushawishi juu ya Nguvu ya EDO chuoni.

Ili kukamilisha mkakati wao hawa makachero wanaoibuikia wamejipanga Kwa mbinu zifuatazo:-

1. Upo ushahidi Wa baadhi ya viongozi Wa serikali za wanafunzi kupigiwa simu na kuobwa wakanushe taarifa zao kwenye hadhara. Kwamba kuandamana kwao kwenda Kwa EDO walishinikizwa. Japo viongozi hao hakuna aliekubali hadi sasa.

2. Wako baadhi ya wanafunzi wanaoaminika kuwa Ni kwenye ushawishi wamepigiwa simu wakiombwa wataje dau ili wasaliti kambi ya EDO hata hivyo namna aliekubali hadi sasa.

Wako baadhi ya wanafunzi wameitwa kwenye vikao vya kikachero na kujadili na kupanga bajeti itakayo kizi kuwezesha kupata usafiri yaani kukodi magari na posho za wanafunzi ili wakusanywe mahala na wafanye maandamano ili kupinga kile ambacho watanzania wote tulishuhudia wanafunzi waliminika Kwa EDo kushauli atanhaze nia.

Pia wako wanafunzi walithubutu kuonesha misimamo yao kufa pamoja na EDO wametishiwa kufanya vibaya licha ya kuwa haijawekwa wazi Mpango wao je, Ni kuwateka au la?

Kuna ujumbe umenaswa ukienda kwa Mwenyekiti wa wanazuoni ili awasiliane na Mwenyekiti wa UVCCM katavi ampeleke kwa Mh. Pinda.

Mwenyekiti huyo ameambiwa endapo atakubali kufanya mchezo huu mchafu wa kuigiza kuwa wanampinga Lowassa wamehaidiwa kupewa kiasi cha Tsh. Milioni 50 za uratibu na kumaliziwa kiasi cha Tsh. milioni 30 za ahsante.

Wakati watu wakifa mahospitalini kwa kukosa madawa wao akina Membe na Pinda wanateketeza mamilioni ya shilingi kwa ajili ya upuuzi tu.

Hizo fedha kwanini hawazitoi kwa ajili ya mapambano dhidi ya mauaji ya maalbino, ama kusaidia wahanga wa mafuriko kama walivyojitokeza Mbowe na Lowassa kuwasaidia wahanga wa Mwakata Kahama?

Mpaka sasa watu wamegoma kufanya hivyo na wamepandishiwa dau na endapo watagoma tena basi wameambiwa watafanyiwa kitu mbaya.
 
Kwanza hili tamka ukilisoma between line utagundua kuwa, hao vijana wamepata shinikizo kulitoa, maana wameliandika kiushabiki sana na kuegemea upande mmoja...kwa mfano...

"Eti uadilifu wake unatiliwa shaka na jamii" Ni jamii gani hiyo inayotilia shaka uadilifu wa Lowassa? kwa ushaidi gani?

Toka juma pili mlikuwa wapi kukanusha? mmekaa siku ngapi hadi leo?

Eti "Tunabebeshwa lawana..." na nani?

Ushahidi kuwa "Lowassa aliwapa fedha hao wanafunzi upo wapi?

Ninyi hamfai kuwa Marais wa hivyo vyuo, Nijuavyo, Vyuoni ni lazima Rais wa chuo awe au serikali yake iwe na"Intelligency personnel" ili kila jambo linalopangwa na dhidi ya chuo, serikali yake na wanachuo wenzake basi apate taarifa mapema ili kuepusha, kuwezesha, kusitisha, au kukanusha haraka....
 
TAMKO LA UONGOZI WA SERIKALI ZA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU DODOMA KULAANI KUHUSISHWA KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU VYA DODOMA NA KUMUOMBA MH. LOWASA KUGOMBEA URAIS.

Ndugu Waandishi wa habari, Tunapenda kutanguliza shukrani za dhati kwenu kwa kufika katika eneo hili kutusikiliza.Mbele yenu ni viongozi wa serikali za wanafunzi kutoka Vyuo vikuu mbalimbali vilivyopo mkoani Dodoma.Ndugu waandishi wa habari,si kawaida na wala mazoea kwa marais na viongozi wa serikali za wanafunzi kutoka vyuo tofauti kukutana kwa pamoja na kuzungumza na nyie wanahabari kama inavyotokea hii leo.

Ndugu wanahabari,siku ya Jumapili ya tarehe 22 mwezi huu wa 3,kundi la watu waliojitambulisha kama ni wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma walijikusanya nyumbani kwa mh; Lowasa na kutoa matamko mbalimbali ikiwa pamoja na kuutangazia uma wa watanzania kuwa sisi wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma tunamuunga mkono na tunahitaji Lowasa awe rais wetu sambamba kumchangia pesa.

Ndugu wanahabari,Tunapenda kukanusha kuwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma kwa ujumla wetu hatukuhusika na jambo lile na kama viongozi wa serikali za wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya mkoa huu wa Dodoma,Tunapinga na kulaani kitendo cha watu wachache kwenda kutuingiza sisi wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma katika jambo ambalo halituhusu na wala si lililotuleta hapa Dodoma.

Sisi kama wasomi ambao jamii inatutegemea kama kioo hatuwezi kuandamana na kujikusanya kwenye nyumba ya kiongozi na kumuomba agambee urais, wakati tunajua fika sisi hatuhusiki na uteuzi wa wagombea ndani ya taasisi yao.Kilichofanyika ni kuudanganya uma wa watanzania na taasiasi yake kupitia kivuli cha vijana wachache kutoka vyuo vya hapa Dodoma,waliolipwa pesa ili waweze kuwa kava la tukio lile.

Ndugu wanahabari,Mkoa wa Dodoma unavyuo vikuu visivyopungua 8,Na jumla ya wanafunzi wote tunaosoma katika vyuo vya Dodoma ni zaidi ya wanafunzi 35,000.Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) pekee yake kinawanafunzi wasiopungua 22,000.Idadi ya watu waliojikusanya nyumbani kwa Mh: Lowasa siku ya tarehe 22-03-2015 haizidi watu 230 wakiwemo Wamachinga na Wenyeviti wa Jumuiya za wazazi, kama vyombo vya habari vilivyoripoti.

Ukiwatoa Wamachinga na Wenyeviti wa Jumuiya za wazazi waliotoka mikoa mbalimbali,idadi ya wanafunzi waliokuwepo kwenye tukio lile hawazidi 150.Idadi hii ni sawa na asilimia 0.4 ya wanafunzi wote wanaosoma vyuo vikuu vya Dodoma.Ndugu wanahabari,kwa akili ya kawaida kabisa asilimia 0.4 ya wanafunzi wa vyuo vikuu ndio waliokuwa pale.Tunashangazwa na dhambi tusiyoitenda tunayobebeshwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma ambao kwa sasa tupo bize na msimu mpya ya masomo wenye changamoto mbalimbali.

Ndugu wanahabari,sisi kama vijana wasomi na watu tunaotegemewa na jamii zetu tutakusanyika katika kujadili na kuchambua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii yetu na sio kukusanyika kwa ajili ya mwanasiasa ambaye sifa zake na uhadilifu wake unatiliwa shaka katika jamii.Tunaomba mlijulishe Taifa, kuwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma hatujahusika na tukio lile isipokuwa wanafunzi wachache walitumika kwa kupewa pesa na wahusika wa tukio lile.Tunataka Taifa lijue hatupo tayari kutumia elimu zetu kulitia upofu taifa letu.

Waambieni mama zetu na baba zetu huku vijijini kwetu kuwa tumekuja kutafuta elimu ili ituwezeshe kuwakomboa wao na sio kutumika na Wanasiasa kwa malengo yao.Tunatambua haki ya mwanafunzi kuamua na kufanya shughuli za kisiasa nje ya maeneo ya vyuo, lakini hatukubaliani na wanafunzi wachache kuchafua na kuwapaka matope maelfu ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma ambao hawajahusika na tukio lile.Hii sio haki na haikubaliki.

Vilevile tungependa kutumia fursa hii kuwaasa wanafunzi wenzetu popote pale nchini, makundi mbalimbali ya kijamii (wakulima, wafugaji, wavuvi, wamachinga, wasanii, n.k), zikiwemo taasisi za dini kwamba watu wachache kuzungumza kwa niaba ya makundi juu ya mambo yanayogusa maamuzi ya mtu binafsi.

Mwisho tunatoa wito kwa wanafunzi wenzetu wote kujitambua na kutumie muda wetu kwa mambo ya msingi na muhimu kwa ustawi wa Nchi yetu. Na kuonesha jinsi wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Dodoma walivyokasilishwa na jambo hili, Tamko hili limesainiwa na wanafunzi 7821 toka vyuo mbali mbali vya Dodoma.Majina ya sahihi za wanafunzi zimeambatanishwa. Tusikubali kutumika na wanasiasa wa aina hii.

Asanteni

Mungu ibariki Tanzania,Mungu vibariki vyuo vikuu vya Dodoma.

Kwa niaba ya wawakilishi wa serikali za Wanafunzi Chuo cha Mipango,Chuo cha Madini, Chuo cha Hombolo,Chuo kikuu cha Dodoma(UDOM) na CBE.

DANIEL DANIEL -Rais wa Saint Jonh’s University

26/03/2015

Mwingine ni upuuzi tuu! mnaajifanya kutoa matamko fake mnamwogopa nani? mlitumwa na nani? wote tunawajua mliopokea hizo pesa,Wengi niwalikua viongozi wa UDOSO mlionekana hadi kwenye TV msipende kupotosha watu kwa njaa zenu.
 
Kwa hili la Lowasa ni fundisho tosha kuwa tuwekeze kwenye Elimu itakayotukomboa na Umasikini unaoambatana na ujinga.
 
Hili tukio lilishashtukiwa kuwa kuna watu la akina Membe na Pinda kuwatumia wanafunzi wa kuwahonga mamiliini ya Pesa ili wakanushe.

Ushahidi huu hapa

PINDA, MEMBE WAPANGA KUMUHUJUMU LOWASSA

Ni wazi sasa kuwa kambi ya Mizengo Pinda na Bernard Membe wameanza kupanga mbinu chafu za kumchafua Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa.

Pinda na Membe wamepandwa na hasira zaidi mara baada ya kuona wananchi wa kada na rika tofauti wakienda nyumbani kwa Lowassa maeneo ya Area D, Dodoma na kumuomba atangaze nia na kisha achukue fomu ya kugombea urais.

Wale watu mbalimbali ambao wameshiriki kwenda kumuomba wameanza kuandamwa na kambi ya Membe na kambi ya Pinda kwa kuanza kuwarubuni kwa kuwapa rushwa waitishe vyombo vya habari na wapindishe uhalisia wa tukio.

Watu hao wanapewa pesa ili waseme kuwa Lowassa amewapa pesa, chakula, malazi na usafiri wa kwenda pale na wala hayakuwa malengo yao na wamefuata pesa tu.

Wanaorubuniwa kwenda kusema maneno ya ovyo ni wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma, masheikh pamoja na wachungaji ambao asilimia kubwa wamegoma kwenda kuisaliti mioyo yao kwa kusema uongo tofauti na uhalisia ulivyo.

Mathalani upande wa vyuoni, Vijana waliopewa kazi ya kuhakikisha hili swala linatekelezwa Ni Mwenyekiti Wa UVCCM wilaya ya Katavi(Jina linahifadhiwa).

Wanafunzi walioahidiwa kupewa fedha ili wafanye harakati hizo chafu Ni Rutagibwa, ikumbukwe Rutagibwa Ni miongoni mwa baadhi ya wafuasi Wa Membe ambao wamebaki watiifu Kwa Membe baada ya kutengenezewa trip ya kwenda China kati ya marais 25 waliopewa bongo hiyo ya safari
kimkakati ili kuwekeza ushawishi vyuoni kutoka UDOM.

Wengine ni Rais Wa Chuo cha Madini Bwana Magesa F. Magesa. Na Rais Wa chuo cha St. John. Hawa ndio wa Ratiba Wa mkakati pale Udom dhidi ya siasa chafu ya kikachero na kuhonga wanafunzi fedha ili waandamane kupinga ushawishi juu ya Nguvu ya EDO chuoni.

Ili kukamilisha mkakati wao hawa makachero wanaoibuikia wamejipanga Kwa mbinu zifuatazo:-

1. Upo ushahidi Wa baadhi ya viongozi Wa serikali za wanafunzi kupigiwa simu na kuobwa wakanushe taarifa zao kwenye hadhara. Kwamba kuandamana kwao kwenda Kwa EDO walishinikizwa. Japo viongozi hao hakuna aliekubali hadi sasa.

2. Wako baadhi ya wanafunzi wanaoaminika kuwa Ni kwenye ushawishi wamepigiwa simu wakiombwa wataje dau ili wasaliti kambi ya EDO hata hivyo namna aliekubali hadi sasa.

Wako baadhi ya wanafunzi wameitwa kwenye vikao vya kikachero na kujadili na kupanga bajeti itakayo kizi kuwezesha kupata usafiri yaani kukodi magari na posho za wanafunzi ili wakusanywe mahala na wafanye maandamano ili kupinga kile ambacho watanzania wote tulishuhudia wanafunzi waliminika Kwa EDo kushauli atanhaze nia.

Pia wako wanafunzi walithubutu kuonesha misimamo yao kufa pamoja na EDO wametishiwa kufanya vibaya licha ya kuwa haijawekwa wazi Mpango wao je, Ni kuwateka au la?

Kuna ujumbe umenaswa ukienda kwa Mwenyekiti wa wanazuoni ili awasiliane na Mwenyekiti wa UVCCM katavi ampeleke kwa Mh. Pinda.

Mwenyekiti huyo ameambiwa endapo atakubali kufanya mchezo huu mchafu wa kuigiza kuwa wanampinga Lowassa wamehaidiwa kupewa kiasi cha Tsh. Milioni 50 za uratibu na kumaliziwa kiasi cha Tsh. milioni 30 za ahsante.

Wakati watu wakifa mahospitalini kwa kukosa madawa wao akina Membe na Pinda wanateketeza mamilioni ya shilingi kwa ajili ya upuuzi tu.

Hizo fedha kwanini hawazitoi kwa ajili ya mapambano dhidi ya mauaji ya maalbino, ama kusaidia wahanga wa mafuriko kama walivyojitokeza Mbowe na Lowassa kuwasaidia wahanga wa Mwakata Kahama?

Mpaka sasa watu wamegoma kufanya hivyo na wamepandishiwa dau na endapo watagoma tena basi wameambiwa watafanyiwa kitu mbaya.

lowasa amewaambukiza mpaka wafuasi wake maigizo.pole hasafishiki huyo.
 
kumbe wanafunzi wa vyuo vya Dodoma ni vilaza namna hii. Tamko gani hili utadhani limeandikwa na mtoto wa darsa la tatu? ndio maana wanasiasa uchwara wanayatumia sana haya madent ya Dodoma

Hilooo tamkooo uchwara waache kuleta usanii. Hapo chini kuna jina la rais wa st.john sasa yeye kama nani adi azungumzie mambo yanayohusu UDOM
Lakini pia kama ni kweli anatakiwa aandike icho kikao kilifanyika tarehe ngapi ukumbi gani.
Pia hatukutarajia tuone jina lake maana huo ujumbe wote unahusu UDOM si st.john jama ni hivyo atuambie hapa yeye kama nani hadi aweke huo ujumbe.
Ujingaa ujinga na chuo chetu hatutaki.
 
Nyie ndio mnaotumiwa na Nepi mje kuupotosha umma wa watz sio,kw hilo mmechelewa sana mnakumbuka shuka tyr kumekucha,watz ujumbe umeshafika kwao kwamba Makundi mbalmbali yana muunga mkono ktk mbio zake za kuwani urais tofauti na mtu yyte kwa sasa na El ndio tumaini la watz wengi,hizo propaganda zenu zimechelewa mno yan labda mngeanza kabla makundi kufika kwa EL huenda mngefanikiwa kuturubun huo ujingA wenu,Lowassa ndo habar ya mjin aisee bnafsi cjaona mbadala wake labda ww mleta mada nan unaona anacfa za kutuongoza zaidi ya EL

hivi huyo Nepi neuye ye ni nan hasa nchi hii,hili tamko la wanafunzi wanajifanya kuja na porojo na kujidai kuyasemea makundi mengine inamaana nepi haoni tamko limekaa kikbi pinzan ya lowasa au anakua kipofu kwa wavizia kugombe wengine.hayo matoto ni zero kabisa haya wakachukue mgao wao kwa nape alokabidhiwa na team mgombea raisi wake,na hakika huyu nepi anaidhalilisha hasa ccm na kuongeza tension ya kutaka kujua kitakachojiri kwa El pindi kipenga kikiunguruma
 
St. John's University???? Hiki nacho ni chuo Kikuu???

Tafuteni vyuo vingine vya kusoma vijana.
 
Back
Top Bottom