Mgomo wanukia vyuoni: UASU yatishia kugoma kisa CBA

Mgomo wanukia vyuoni: UASU yatishia kugoma kisa CBA

Ikariiah

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
246
Reaction score
294

Chama cha Wahadhiri wa Vyuo Vikuu vya Umma(UASU) kimetoa notisi ya siku 7 ya mgomo kufuatia kukwama kwa mazungumzo kuhusu Mkataba wa Pamoja wa Ajira(CBA) wa 2025 hadi 2029. Katibu Mkuu wa UASU Dkt. Constantine Wasonga amesema Wahadhiri wa Vyuo Vikuu vyote vya Umma wataanza mgomo Oktoba 2, 2026.

UASU inasema Serikali na taasisi zinazohusika bado hazijatoa ahadi ya kifedha kuhusu utekelezaji wa CBA hiyo, licha ya mazungumzo kuendelea kwa muda. Aidha wanataka mishahara na marupurupu ya wahadhiri yafadhiliwe kupitia hazina kuu ya Serikali (National Exchequer) badala ya kutegemea ada za wanafunzi.

Lakini suala hili si la mishahara pekee. UASU pia imeibua masuala mengine tata kama:

1)Uhaba wa wahadhiri katika vyuo vya umma.
2)Kuongezeka kwa utegemezi wa wahadhiri wa muda.
3)Mzigo mkubwa wa wanafunzi kwa mhadhiri mmoja.
4)Changamoto za ufadhili wa vyuo na majukumu ya kifedha kama pensheni.

Sasa hapa ndipo utata wote huu unamgusa mwanafunzi. Takwimu za Tume ya Elimu ya Vyuo Vikuu (CUE) zinaonyesha kuwa idadi ya wanafunzi katika vyuo vikuu nchini iliongezeka kutoka 628,541 mwaka 2024 hadi 707,150 mwaka 2025, ambalo ni ongezeko la 12.5%. Wakati huo huo, idadi ya wahadhiri iliongezeka kwa 6.8% pekee.

Kwa baadhi ya vyuo vya umma, uwiano wa wanafunzi kwa mhadhiri umeongezeka hadi viwango vinavyoweka shinikizo zaidi kwenye ufundishaji, usimamizi na hata usahihishaji wa mitihani(marking)

Kwa hiyo, kinachowekwa hatarini hapa si mishahara ya wahadhiri pekee, HAPANA! Ni pia kalenda ya masomo, mitihani, mahafali na uzoefu wa wanafunzi iwapo mgomo utaanza.

Sasa swali kubwa ni: Je, Serikali na UASU watafikia makubaliano kabla ya wahadhiri kugoma rasmi? Itakumbukwa Vyuo Vikuu Vya Umma vimekaribisha maelfu ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza (first years) wiki mbili tu zilizopita na maelfu wengine kurejea baada ya likizo ndefu(long holiday).
 

Attachments

  • 465.jpeg
    465.jpeg
    102.1 KB · Views: 16
Back
Top Bottom